Like jengo limesimamishwa kwa sababu limejengwa kimakosa pale ni sehemu ya mto na alitumia pesa kupata kibali kujenga eneo ambalo alistahili kabisa itakuwa madiwani wa Chadema wamelizuia.
Hapana mkuu sio kwa sababu jengo lipo karibu na mto, na klama ndio hivyo mbona jengo la TRA na Hotel ya Naura Spring zimeruhusiwa kujengwa karibu na mto?
Alafu kwa habari za ndani na zakudhibitika huyu jamaa (MATHIAS) amenunua eneo kwa upanuzi wa Hoteli yake kwa thamani ya bilioni 2, kwani anataka kufanya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa kisasa kwa kuwa ameaidiwa kuwa tenda zote za mikutano ya kiserikali zitakuwa zikifanyikia hapo pindi tu EL akiingia magongoni.
huyo ni tajiri mmoja keshapata dili je hao wengine
Ila kwa masikini huyu jamaa atawapa T-shirt na kanga maana hana muda na ninyi
Hapo ndio atakua hana hofu ya chochote. Kama kusota kesha sota .... Time to do the right thing for this nation and NOT for his tummy.
I salute you mzee Mang'ula.
Mimi sina chama lakini wakiwaengua hawa waroho wa vyeo, nitajiunga na CCM....
Hakuna kuondoka Lowassa pigania haki yako ya kuwa rais kupitia ticket ya ccm maana si wakabila na wana democrasia pana. Tunajua wanaokupinga ni wale kundi la vijana waliotumwa wakukatae kwakuwa unatokea kaskazini. Hayo ni mambo ya kikabila wakati wewe ni mwamba wetu. Kila siku ccm mnaimba cdm wanamtenga Zitto iweje na nyinyi ccm muige ya cdm. Lowassa usingoje muda wala nini democrasia inakuruhusu kukutana na yoyote,popote na wakati wowote kupanga mikakati ya ushindi.
Mkuu alipokuwa anahutubia siku moja alisema sasa wanaotaka urais wanaweza wakaanza kupita pita, alimaanisha nini? yalikuwa yake aliyoyaongeza juu ya akili za wengine au ilikuwa ni azimio la chama? Kama ni hivyo basi mwenyekiti wa chama alisema hivyo na chama hakikutoa tamko kupinga basi Lowasa yuko sahihi tena kachelewa. Kwanza kina Nape na Mangula wanatapatapa hakuna wa kumshinda Lowasa wala kumtikisa . . . rafiki yake Kinana kakaa kimya wao ndio wanaleta mdomo domo tutaona mwisho wao. . . .
Mkuu alipokuwa anahutubia siku moja alisema sasa wanaotaka urais wanaweza wakaanza kupita pita, alimaanisha nini? yalikuwa yake aliyoyaongeza juu ya akili za wengine au ilikuwa ni azimio la chama? Kama ni hivyo basi mwenyekiti wa chama alisema hivyo na chama hakikutoa tamko kupinga basi Lowasa yuko sahihi tena kachelewa. Kwanza kina Nape na Mangula wanatapatapa hakuna wa kumshinda Lowasa wala kumtikisa . . . rafiki yake Kinana kakaa kimya wao ndio wanaleta mdomo domo tutaona mwisho wao. . . .
Mangula hajajifunza. Kauli kama hizi zilimgharimu sana wakati jk anataka urais. Alimshambulia kweli. Jk akaibuka mshindi. Mangula akapoyelea kwenye kilimo cha nyanya hadi jk alivyomsamehe. Naona kamuanza laigwanani. Nahofu yasijempata yale yale ya jk. Ni ushauri tu.
Kweli ccm hawana aibu, Lowassa kutangaza nia yake ya kugombea urais wanasema tayari amepoteza sifa na kwamba wako tayari kumchukulia mtu yeyote hatua kali ikithibitika, Ila kwa upande mwengine Zitto alivyotangaza nia ya kugombea urais na kuanza kufanya mipango ya siri ili kupindua uongozi wa chama cha chadema walimpa heko tena wakasema akili kubwa haiwezi kuongoza akili ndogo ili hali wao hawawezi kukubaliana na upuuzi wa Zitto kwenye chama chao ila kwa chadema ni sawa.
Zitto ondoka chadema kwani wanachama hawakutaki nini unangangania, na wanao ku support wao wenyewe huko ccm hawana huo utaratibu unaotaka wewe.
Lowassa kuzunguka kwenye nyumba za ibada ni moja ya imani yake pia waumini wa dini zote wamjue rais 2015 kosa likwapi akitaka uongozi ajifungie nyumbani kwake? Jamani acheni mungu anamleta na elimu bure na maji bure.
Unaweza kusema sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kumfungia kazi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa baada ya jana Makamu Mwenyekiti wake (Bara), Phillip Mangula kusema kuwa wanachama wake walioanza mbio za kuwania urais mwaka 2015 watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Mangula alisema kama wanachama hao wasipochukuliwa hatua watakifanya chama hicho kupoteza mvuto katika medani ya kisiasa nchini;
"Wapo watu wanataka waichanechane CCM kwa sababu ya uroho wao wa madaraka, uroho wa udiwani, ubunge na hata urais. Kuna makundi ndani ya chama kazi yake ni kuwabomoa wenzao, kamwe hatuwezi kuyafumbia macho."
Akifafanua hilo Mangula alisema: "Tutawaita wote walioonyesha nia ya kuutaka urais 2015 na kuwahoji kwanini wanafanya hivyo wakati muda bado haujafika. Tumeshawachunguza katika mikutano wanayoifanya, tumebaini kuwa wanatoa misaada na kusafirisha watu, tunajua dhamira yao ni nini."
Mangula ametoa kauli hiyo ikiwa imepita siku moja tangu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kusema mwanachama yeyote wa CCM anayetangaza nia ya kuwania urais kabla ya muda mwafaka kutangazwa atapoteza sifa za kugombea.
Nape alitoa kauli hiyo baada ya Lowassa siku mbili zilizopita, kutangaza nia ‘kimtindo' akisema anaanza rasmi safari aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo pia itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.
Lowassa ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani ya kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli.
Mangula aliwashukia vigogo wa chama hicho wanaoutaka urais jana katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Kamati ya Siasa tawi la Ofisi ndogo za chama hicho Lumumba, wakati akitoa salamu za mwaka mpya kwa wanachama wote wa CCM nchini.
Ataja kanuni za uongozi
Katika mkutano huo Mangula alisaidiwa kusoma kanuni za uongozi na maadili ya chama hicho, kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali na Katibu Tume ya Udhibiti wa Nidhamu ya Viongozi wa CCM na wanachama taifa, Masoud Mbengula.
Moja ya kanuni hizo inasema "Ni mwiko kwa kiongozi wa CCM kutumia dini yake au kabila au rangi au jinsia au eneo analotoka, kama sifa ya kushawishi wapiga kura wamchague ama yeye mwenyewe ama mgombea anayemuunga mkono."
Mangula alisema kwa mujibu wa kanuni za chama hicho, mwanachama anayefanya mambo kinyume na kanuni huitwa msaliti na hafai kuendelea kufumbiwa macho kwani anaweza kukiangamiza chama wakati wowote.
Japo sifa ya kugombea uongozi haitokani na wingi wa fedha alizonazo lkn Mzee Mangula anatakiwa na anajua kuwa kumpata mgombea Urais ndani ya Ccm lazima uwe na fedha nyingi kuliko wengine.
Sio fedha za kuhonga ndani ya vikao vya ndani ya chama tu bali hata fedha za kuhonga wanapigakura.
Kitendo cha Mzee Mangula kumshambulia Lowassa kwamba kitendo chake cha kutangaza nia na kugawa fedha ni kumnyima raha Jk ni sawa na kusema kumnyima nafasi Lowassa ya kutangaza nia ni kuwanyima raha Uvccm.
Mzee Mangula amuulize Jk kilichotaka kumtokea pale Dodoma walipotaka kumfukuza Lowassa au alipotaka kuifuta Uvccm aliambiwa nini.
Kauli za Mangula juu ya Lowassa ni janga kwa ccm hata Kinana analijua hilo.
Tema mate,sixgates,mwichange,lizaboni,faiza foxy someni hapa na mje na majibu kwanini makamu wenu mwenyekiti wa chama anasema haya au ni halali kwa ccm ila ni haramu kwa chadema na wewe bethelem soma hapa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.