Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

Acha tuendelee kuchochea kuni kavu ili moto ulipuke kabisa......cc Ritz
 
Unalinganisha na waraka wa ushindi 2013 by Samson mwigamba?lakini hawa wenzetu hawatawafukuza wala kuwavua vyeo vyao akina fisadi EL na wala hawatawaita wahaini
 
Lowasa akiupata urais Mangula atarudi kulima viazi Njombe. Siamini kama fisadi kinana (Mtendaji mkuu wa ccm) anaweza kumtosa fisadi mwenzake Lowasa.

Inaonekana Mzee Mangula hajui aina ya mapepo na majini anayoyatumikia na yaliyomzunguka ndani ya ccm.
 
wewe tumia akili mangula anapinga nini?mwekundu maana kila kitu amesema Mangula sasa mnao mtetea ZZK,na Dr Kitila na Mwigamba mpo wapi?ccm mlimfukuza Mansoor Himid mwakilishi wa jimbo la kiembe samaki kisa anaunga mkono serikali 3 sasa leo wafukuzeni wakina warioba kisa wametoa tena kwenye rasimu ya 2 ya katiba mnatetea ujinga yie vijana wa lumumba njooni hapa leo jamvini mmpingeni Mangula
 
Nape alianza na ishu ya kujivua gamba akawataja LOWASA Rostam na Chenge kuwa nimagamba na kidai watavuliwa uanachama muda wowote baada ya kuhojiwa

Kilichoendelea baada ya Nape kumtaja Lowasa na hao pacha wenzake LOWASA alienda kwa mwenyekiti Kikwete na kumuliza kuwa wewe ndiye uliye mtuma Nape anitukane yeye na Mukama
Wakaongea waliyo ona

Baada ya muda tukaambiwa kujivua gamba inaanzia ngazi ya tawi mpaka taifa swala lakujivua gamba likaishia kimya kimya


Uchaguzi wa ndani ya chama na jumuia zake rushwa ilikiwa nje nje wagombea wamelia hadi basi MANGULA alipopewa nafasi ya makamu mwenyekiti aliahidi ndani ya miezi sita atakuwa amewafuta wote waliyo shinda kwa rushwa mpaka leo imekuwa story

Ushauri wangu kwa MANGULA na NAPE
 
...
Mangula alisema kwa mujibu wa kanuni za chama hicho, mwanachama anayefanya mambo kinyume na kanuni huitwa msaliti na hafai kuendelea kufumbiwa macho kwani anaweza kukiangamiza chama wakati wowote.
...

Duniani kote, kwenda kinyume na kanuni za msingi za taasisi, tena kwa kificho, taasisi ambako wewe ni mwanachama au kiongozi, neno sahihi ni USALITI; hakuna jinsi wala namna nyingine ya kukiita kitendo cha namna hiyo. Nashangaa hao wanaoilaumu Chadema kwa kuchukua hatua lakini taasisi nyingine kama CCM zikichukua hatua wanaona ni sahihi. Hivi ni taasisi gani itakayokubali kuwa na mamluki wa kuimaliza yenyewe?
 
mkuki siku zote ni kwa nguruwe lakini kwa binadamu ni mchungu.
 
EL ni wa Kaskazini, Tena anaurafiki mkubwa na viongozi wa CDM, na habari zinazoenea mtaa wa ufipa ni kuwa akipigwa chini huko aliko basi atapewa mikoba ya kupeperusha bendera ya CDM come 2015.
 
Siasa ya bongo ni kma nyumba ukiwa nje unatamani uingie ndani na ukiingia ndani tu yale yote uliyoyapanga unayaacha nje na unakutana na mapyaaa.
 
kama walivyomtuma zitto kuvuruga cdm na ndivyo lowassa anavyowavuruga ccm,atleast el hasaliti chama chake na hajakimbilia mahakamani asifukuzwe.
 
Unalinganisha na waraka wa ushindi 2013 by Samson mwigamba?lakini hawa wenzetu hawatawafukuza wala kuwavua vyeo vyao akina fisadi EL na wala hawatawaita wahaini


Na hicho ndicho kilichoifikisha hii nchi hapa ilipo. Unashangaza unavyotetea ujinga. Mangula mwenyewe kasema kufanya mambo kama hayo, kwa kanuni za Chama, ni usaliti; halafu hatafukuzwa kwenye chama! Labda neno usaliti lina tafsiri tofauti huko magambani au ni mwendelezo wa unafiki ambao kama kawaida makao yake makuu ni umagambani?
 
Ni nani humu ndani ya CCM ni msafi?nape akakaa kimyaaa Kama kameza priton nashangaa Siku 90 za kuvua gamba na kujitoa sumu Hadi za mbinguni zimeshaisha
 
Mangula makamu mwenyekti wa CCM Taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya Edward Lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na CCM kama mgombea wake wa Urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa CCM labda chama kingine!

Kayasema hayo leo mchana Lumumba CCM Sub HQs!

-------------------------

Ni blah blah za kawaida...angekuwa anamaanisha anachosema basi angetaja na majina. Ni unafiki wa halo ya juu.
 
mwekundu soma content ya ujumbe wa Mangula ndio useme mengine amesema nini kuwa watawaita na kuwahoji na hatua za kinidhamu zitachukuliwa,sasa chadema wao wametenda kipi bora?
 
wewe tumia akili mangula anapinga nini?mwekundu maana kila kitu amesema Mangula sasa mnao mtetea ZZK,na Dr Kitila na Mwigamba mpo wapi?ccm mlimfukuza Mansoor Himid mwakilishi wa jimbo la kiembe samaki kisa anaunga mkono serikali 3 sasa leo wafukuzeni wakina warioba kisa wametoa tena kwenye rasimu ya 2 ya katiba mnatetea ujinga yie vijana wa lumumba njooni hapa leo jamvini mmpingeni Mangula

Sasa hapa unataka tujadili nini?Hivi uliishia darasa la ngapi vile?Isijekuwa tunajadiliana na standard seven graduate hapa!
 
ccm hakukaliki ila wako busy kuiyukana chadema..

CCM inabidi wawe waangalifu sana na Mtandao huu wa Nchimbi, Mwigulu. ZZK, Hamad Rashid, Kafulila. Jan Makamba, Sophia Simba na sasa wamemwingiza na Fenella kukamata media. waangalie sana na wasimpuuze nape. hii ya CDM ni sehemu ya huo mchezo uliopangwa
 
Back
Top Bottom