Mangula ahamia rasmi kambi ya Urais ya Lowassa!!

Mangula ahamia rasmi kambi ya Urais ya Lowassa!!

Kikwete, mkewe na mwanae wako kambi ya Membe! Huu ni mpambano mkali!
 
kama siyo dr. wetu
heri lowassa kuliko membe mara alufu.

Madam, nilikuwa nakukubaki kwa mda mrefu sasa, ila hii post yako inaanza kunipa wasi wasi, yaaaaani EL awe rais wa nchi hii ? siamini na sikutarajia ujumbe huu kutoka kwa kamanda kama wewe. Mie nasema ni vyema kila mtu akawa na serikali yake, kuliko Mzungu kuwa rais wa Tanzania.
 
huwezi kuusemea moyo wa mtu.

Madam, nilikuwa nakukubaki kwa mda mrefu sasa, ila hii post yako inaanza kunipa wasi wasi, yaaaaani EL awe rais wa nchi hii ? siamini na sikutarajia ujumbe huu kutoka kwa kamanda kama wewe. Mie nasema ni vyema kila mtu akawa na serikali yake, kuliko Mzungu kuwa rais wa Tanzania.
 
Mkuu LumumbaDar,

Hadi hapo tunachoweza kusema ni kwamba sawa kabisa jamaa yangu nimekusoma Mkuu tena ukizingatia kwamba wote ni Walutheri na Lowassa lakini mwache Mzee Filipo Mangula naye akajikie hizo BAKSISHI anazomwaga ovyo Mzee Lowassa makanisa.

Kila mtu TAJIRIKA NA HELA MENO YA TEMBO CCM ila kura zote ni kwa CHADEMA 2015.

Kifupi ni kutoka kwa watu wawili(Majina yao siweze kuyataja hapa JF), mmoja ni mtumishi ndani ya Ofisi ya CCM makao makuu na mtu wa pili ni kutoka kambi moja ambaye mtu wao alishindwa katika uchaguzi wa UVCCM na bado alikuwa na Imani angepata haki yake ngazi za juu za Chama(Huyu amesema huenda atazungumza na waandishi wa habari ndani ya wiki tatu kutoka sasa)
 
ndio maana nikakwambia humfahamu kinana,kamuulize huyo huyo kibanda wako ambae ni mpambe wa lowassa kwanini alipoteuliwa kinana kushika wadhifa alionao aliweweseka sana na kuandika makala ndefu ya jinsi anavyomuogopa kinana?
Nitajaribu kukujibu kwa hoja.
*Simfahamu Kinana kwa ukaribu yeye kama yeye lakini namfahamu kisiasa(Tangu akiwa mbunge wa Arusha mjini) na pia kikazi (wakati akiwa Red Cross). Simfahamu Kibanda zaidi ya kumsoma na kumsikia kwenye vyombo vya habari tu. Hivyo sina access ya karibu kabisa na hao watu kwa sasa

*Sifa kuu za kinana kisiasa ndani ya CCM:
1/Mnyemerezi(Opportunistic)

2/Mwoga sana(Jaribu kumgusa uone anavyokasirika na kunywea haraka)

3/Myeyushaji(Silencer)

*Siku zote Kinana atakuwa mnyonge ndani ya CCM kwa sababu ya ukweli fulani fulani unaomhusu yeye mwenyewe(Ambao pia ulimwondoa katika siasa za Arusha), ambao unaweza kumgharimu wakati wowote hata sasa.
Ni vizuri ukamuuliza Jenerali Ulimwengu(Alikuwa na Kinana bega kwa bega 1995 katika kampeni za urais za Mkapa) nini kiliwahi kumkuta na CCM wakati alipoanza kuchokonoachonoa?

*Embu jiulize ni vipi Msekwa aonekane ni Kambi ya Lowassa sasa, wakati ni Lowassa huyo huyo aliyeratibu mpango wa kumng'oa kwenye Uspika 2005?
Ni vipi Mkama aje aonekane yuko kambi ya Lowassa wakati aliweka makusudi kuwatoa mafisadi watatu?

Mary Nagu alikuwa ni kampeni manager wa Sumaye 2005 leo yupo kambi ya Lowassa, vipi tena?
Betrice Shelukindo naye vipi tena? Kamwacha wapi Sitta?

Ni kwanini Kinana anaogopa kabisa kuzungumzia kufukuzwa kwa mafisadi ndani ya CCM? Anaogopa nini kumtaja Lowassa kama ni fisadi ndani ya vikao vya CCM?

*Swali la kwanini Kinana na Mangulla wapo kwenye Secretariety hii mpya.
Jibu ni rahisi sana. Ni Mkapa alifanikisha mpango huo baada ya kumlobby Kikwete.

Vipi kuhusu uhusiano kati ya Mkapa na Lowassa?

*Swala la Salim Ahmed Salim kuwa mgombea urais wa CCM 2015, hilo sahau kabisa. Kwa CCM hii hilo HALIWEZEKANI kabisa.
Ilishindikana kwa Salim kuwa mgombea urais wa CCM mwaka 1985, Ikashindikana 1995, Ikashindikana 2005. Sijui itawekanaje 2015?

Jifunze siasa za CCM utazielewa tu.
 
Kuelekea 2015 tutasikia mengi kutoka kwa waroho wa madaraka ndani ya CCM. Sijui kambi za uraisi ziko ngapi sasa hivi?
  1. Kambi ya Lowasa
  2. Kambi ya Sumaye
  3. Kambi ya Membe
  4. Kambi ya Sita
  5. Kambi ya Asha Rose Mingiro (mtake msitake lazima atakuwepo mwanamke atayechukua form)
  6. Kambi ya Dr. Salium
  7. Kambi ya Hussein Mwinyi
  8. Kambi ya..............................

Lakini pamoja na zote hizo bado kambi yenye nguvu zaidi haijatajwa; namaanisha yule ambaye atakuwa chaguo la JK. Habari nilizonazo toka ndani magogoni ni kwamba JK ana mtu wake na kwa bahati mbaya bado hazungumzwi na vyombo vya habari. Amini usiamini chaguo la JK ni Tyson, AKA:

View attachment 92306

Ni kweli ndo chaguo lake
 
Nyie maboi wa Ridhwani mna kazi kweli kweli!!! Mangulla sio mtu wa mchezo ambae huyo kilaza wenu anaweza kumchezea eti tu kwasababu baba yake ni Mwenyekiti!!! Mangulla anakifahamu chama chenu cha magamba kuliko baba MwanaAsha anavyokifahamu hivyo basi hizo propaganda za huyo kilaza Ritz haziwezi kumyumbisha huyo Mzee!!! It has been proven that you need him more than he needs you.

Mkuu kutoka kulima viazi hadi mamlakani si mchezo!
 
Kuelekea 2015 tutasikia mengi kutoka kwa waroho wa madaraka ndani ya CCM. Sijui kambi za uraisi ziko ngapi sasa hivi?
  1. Kambi ya Lowasa
  2. Kambi ya Sumaye
  3. Kambi ya Membe
  4. Kambi ya Sita
  5. Kambi ya Asha Rose Mingiro (mtake msitake lazima atakuwepo mwanamke atayechukua form)
  6. Kambi ya Dr. Salium
  7. Kambi ya Hussein Mwinyi
  8. Kambi ya..............................

Lakini pamoja na zote hizo bado kambi yenye nguvu zaidi haijatajwa; namaanisha yule ambaye atakuwa chaguo la JK. Habari nilizonazo toka ndani magogoni ni kwamba JK ana mtu wake na kwa bahati mbaya bado hazungumzwi na vyombo vya habari. Amini usiamini chaguo la JK ni Tyson, AKA:

View attachment 92306

This world is full of creative minds!!!
 
Hivi kumbe Chui na Paka ni maadui? Do you mean Paka na Panya?

Try to read between the Lines ndio utanielewa.

Nani alikwambia Kinana na Lowassa ni maadui?
Inawezekanaje Mtu awe adui yako kisiasa lakini wakati huo huo apambane na maadui zako wa kisiasa lakini pia ashirikiane na marafiki zako wa kisiasa?

Jaribu kumuuliza Kibanda kuhusu Kinana ni kambi ipi?

Mwaka 2005 wakati Salim Ahmed Salim akichafuliwa na kuvuliwa nguo hadharani na kambi ya wanamtandao, Kinana alikuwa wapi mpaka ashindwe kumtetea?

Sote tusubiri tuone.


LumumbaDaR

Yuko wapi leo UVCCM ARUSHA?
Manake naona umetuletea news bila yeye leo....
Hongera kwa Habari
 
Baada ya kushindwa kumchacua kinana, sasa mnaamia kwa mangula. Poleni sana na hapo ni pagumu sana

Kweli siasa zimeharibu watu, hata kutoa comments zenye mantiki mnashindwa, shame!
 
Nikirejea historia ya utendaji wake,na maamuzi yake,Lowassa jembe,tuseme walimwahi na fitina,wengine sauti zao za kukemea hazitoki sana,unabisha?
 
Wakati umefikwa Tanzania kuongozwa na bepari. Masikini wenzetu wametuangusha sana kwa tamaa za kujilimbikizia mali kupita kiasi. Bora Lowassa awe Rais kwa kuwa anajulikana kuwa na mali za kutosha kabla hata ya kupata Urais... kina mtoto wa Mkulima na kina ------ njaa tu na tamaa ya kuwa na vyote kwa wakati mfupi
 
Back
Top Bottom