Mangula ahamia rasmi kambi ya Urais ya Lowassa!!

Mangula ahamia rasmi kambi ya Urais ya Lowassa!!

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
552
Kukiwa kunafikia miezi sita tangu kuchaguliwa kwa Mangulla kuwa makamu mwenyekiti wa CCM tanzania bara, Simanzi kubwa imeingia kwa kambi za Urais za Sitta na Membe baada ya Kuvuja kwa habari za kiongozi huyo (Philips Mangula) kuhamia rasmi kambi ya Urais ya Lowassa.

Huku kukiwa kumebakia wiki mbili tu ili kuisha kwa muda alioutoa Mangula kwa kujiapiza kuwa ni lazima atafukuza ndani ya miezi sita makada(Mafisadi) wote ndani ya CCM waliopita kwa rushwa kupata nafasi za uongozi ndani ya CCM, mpaka sasa hakuna hata kada mmoja aliyefukuzwa kwa kosa la Rushwa.

Tetesi hizo zilianza baada ya kuwepo habari za Mangula kuonekana katika vikao vya siri vya kambi ya Lowassa lakini pia mwenendo wake usieleweka hususani wa kukataa au kuchelewa kuchunguza au kuwaita kuwahoji watuhumiwa wa Ufisadi ndani ya CCM ambao tuhuma zao ziko mezani kwake.

Msumari wa moto kabisa alioupigilia Mangula ni kitendo chake cha kupinga kitendo cha baadhi ya viongozi wa juu wa CCM makao makuu kuwahoji viongozi waandamizi wa UVCCM kwa madai ya rushwa wakati wa Uchaguzi wa ndani wa jumuiya hiyo mwaka jana.

Mpango wa kuwahoji ulishinikizwa na kuratibiwa na Ridhwani Kikwete kwa nia ya kutaka kuibeba kambi ya urais ya Membe.

Inasemekana Mangulla alihoji kwa ukali kwanini hakujulishwa na pia kwanini watu hao waitwe kuhojiwa wakati yeye akiwa hayupo kikazi ofisini(Mangula alikuwa kwenye Fungate la ndoa). Tetesi zinasema mafaili yote ya mahojiano hayo kayafungia kabatini na punde huenda yatatupwa.

Habari hizi zimeonekana ni neema na ushindi kwa kambi ya urais ya Lowassa, kwani kwa sasa kambi hiyo ina karata kubwa karibu zote za ushindi, ikiwemo Makamu wenyeviti wote wa CCM taifa(Bara na visiwani), Katibu mkuu wa CCM, Wenyeviti wote wa jumuiya za CCM(wazazi, vijana na wanawake), Zaidi ya 70% ya wajumbe wa NEC, Zaidi ya asilimia 65% ya wenyeviti wa CCM wa mikoa, zaidi ya asilimia 60% ya wabunge wote wa CCM(Akiwemo Spika na manaibu wake wote).
 
mmeshatufanya watoto wadogoo! mnajipanga tu mtafikiri mtawaonhoza nanii zenu tutaona !
 
Naam, master plan ikiratibiwa vizuri na kusimamiwa ipasavyo...hutoa matokeo/mafanikio mazuri sana.
 
Nyie maboi wa Ridhwani mna kazi kweli kweli!!! Mangulla sio mtu wa mchezo ambae huyo kilaza wenu anaweza kumchezea eti tu kwasababu baba yake ni Mwenyekiti!!! Mangulla anakifahamu chama chenu cha magamba kuliko baba MwanaAsha anavyokifahamu hivyo basi hizo propaganda za huyo kilaza Ritz haziwezi kumyumbisha huyo Mzee!!! It has been proven that you need him more than he needs you.
 
wanaoafiki waseme ndio..."ndioo" wasioafiki waseme sio.."sioooooooooooooo" HOJA IMEPITA!!
 
Kuelekea 2015 tutasikia mengi kutoka kwa waroho wa madaraka ndani ya CCM. Sijui kambi za uraisi ziko ngapi sasa hivi?
  1. Kambi ya Lowasa
  2. Kambi ya Sumaye
  3. Kambi ya Membe
  4. Kambi ya Sita
  5. Kambi ya Asha Rose Mingiro (mtake msitake lazima atakuwepo mwanamke atayechukua form)
  6. Kambi ya Dr. Salium
  7. Kambi ya Hussein Mwinyi
  8. Kambi ya..............................

Lakini pamoja na zote hizo bado kambi yenye nguvu zaidi haijatajwa; namaanisha yule ambaye atakuwa chaguo la JK. Habari nilizonazo toka ndani magogoni ni kwamba JK ana mtu wake na kwa bahati mbaya bado hazungumzwi na vyombo vya habari. Amini usiamini chaguo la JK ni Tyson, AKA:

Stephen.jpg (Edited for fairness' sake, mods)
 
Wewe Lumumba,madhara ya akili za kushikiwa na wachezesha disko na wazinzi,ndo hayo,unatunga tu ujinga ujinga,shame on you cdm.
 
Du Massm bwana!!! Ila kwa hakika ukiangalia kwa makini ni nani hasa kwa upande wa SSM anaweza kusimama urais ambaye hana harufu ya ufisadi? Kwa kuwa wote ni mafisadi ni bora basi kuweka hata fisadi ambalo linachapa kazi, na si mwingine ni ......................................................
 
Mkuu, hebu tupe tafsiri nzuri ya hilo, sijaelewa uhusiano wa kuoa kwa Mangula na uhuru alioupoteza!
Mheshimiwa hii si kwa mzee wetu tu bali ni kwa kila mmoja wetu. Unaweza ukawa na msimamo wako na mwenzawako akawa na msimamo tofauti na wako. Ukiwa peke yako situation kama hii haiwezi kutokea uko huru, lakini ukiwa married lazima umalizane kwanza ndani ndiyo utoke nje inategemea na jinsi yalivyoisha ndani. nilimaananisha hivyo :mvutaji:
 
Baada ya kushindwa kumchacua kinana, sasa mnaamia kwa mangula. Poleni sana na hapo ni pagumu sana
 
Kukiwa kunafikia miezi sita tangu kuchaguliwa kwa Mangulla kuwa makamu mwenyekiti wa CCM tanzania bara, Simanzi kubwa imeingia kwa kambi za Urais za Sitta na Membe baada ya Kuvuja kwa habari za kiongozi huyo (Philips Mangula) kuhamia rasmi kambi ya Urais ya Lowassa.

ACHA UJINGA NA USIUPOTOSHE UMMA yaani mtu asitende kazi zake tu, mnaanza kudai yuko kambi hii mara ile.
usimfanye Mang'ula hajui upuuzi wenu na kukiangusha CHAMA,
Kwa nini machochea makambi au mnalipwa?
Huyu Makamu mnajua ni nini kilimkera hadi kutoa Masharti ya kuukubali hicho Cheo
  • Kwa nini alimtaka Kinana arudi
  • Kwa nini alitaka jamaa yako asiwepo katika CC
  • Kwa nini alitaka CC iwe na vijana zaidi? na isiwe kambi yako?
acha kushikiwa akili hapo Lumumba njoo Makao Makuu
 
Back
Top Bottom