Nitajaribu kukujibu kwa hoja.
*Simfahamu Kinana kwa ukaribu yeye kama yeye lakini namfahamu kisiasa(Tangu akiwa mbunge wa Arusha mjini) na pia kikazi (wakati akiwa Red Cross). Simfahamu Kibanda zaidi ya kumsoma na kumsikia kwenye vyombo vya habari tu. Hivyo sina access ya karibu kabisa na hao watu kwa sasa
*Sifa kuu za kinana kisiasa ndani ya CCM:
1/Mnyemerezi(Opportunistic)
2/Mwoga sana(Jaribu kumgusa uone anavyokasirika na kunywea haraka)
3/Myeyushaji(Silencer)
*Siku zote Kinana atakuwa mnyonge ndani ya CCM kwa sababu ya ukweli fulani fulani unaomhusu yeye mwenyewe(Ambao pia ulimwondoa katika siasa za Arusha), ambao unaweza kumgharimu wakati wowote hata sasa.
Ni vizuri ukamuuliza Jenerali Ulimwengu(Alikuwa na Kinana bega kwa bega 1995 katika kampeni za urais za Mkapa) nini kiliwahi kumkuta na CCM wakati alipoanza kuchokonoachonoa?
*Embu jiulize ni vipi Msekwa aonekane ni Kambi ya Lowassa sasa, wakati ni Lowassa huyo huyo aliyeratibu mpango wa kumng'oa kwenye Uspika 2005?
Ni vipi Mkama aje aonekane yuko kambi ya Lowassa wakati aliweka makusudi kuwatoa mafisadi watatu?
Mary Nagu alikuwa ni kampeni manager wa Sumaye 2005 leo yupo kambi ya Lowassa, vipi tena?
Betrice Shelukindo naye vipi tena? Kamwacha wapi Sitta?
Ni kwanini Kinana anaogopa kabisa kuzungumzia kufukuzwa kwa mafisadi ndani ya CCM? Anaogopa nini kumtaja Lowassa kama ni fisadi ndani ya vikao vya CCM?
*Swali la kwanini Kinana na Mangulla wapo kwenye Secretariety hii mpya.
Jibu ni rahisi sana. Ni Mkapa alifanikisha mpango huo baada ya kumlobby Kikwete.
Vipi kuhusu uhusiano kati ya Mkapa na Lowassa?
*Swala la Salim Ahmed Salim kuwa mgombea urais wa CCM 2015, hilo sahau kabisa. Kwa CCM hii hilo HALIWEZEKANI kabisa.
Ilishindikana kwa Salim kuwa mgombea urais wa CCM mwaka 1985, Ikashindikana 1995, Ikashindikana 2005. Sijui itawekanaje 2015?
Jifunze siasa za CCM utazielewa tu.
Humfahamu kinana kwa ukaribu lakini unazifahamu sifa zake duuuh,we mkaree..
Mzee unaonekana uko too much on speculations na mambo ya zamani pia kuliko facts,hili ni tatizo la watu wengi wa kizamani kwenye siasa za ccm,we moderate we think diffrerent.FACTS:Kama lowassa angekua na ushawishi kiasi hicho jina lisingekosekana kwenye kamati kuu ambayo upatikanaji wa wajumbe wake sijui kama unaujua,na pia asingekwenda kugombea ujumbe wa NEC kule wilayani cuz yeye ni heavy weight kule alishapita angepambana huku na kina Tyson,Membe,J.Makamba,Shyrose Bhanji n.k. unaweza kunijibu yeye na Chenge ambae last time aliongoza kwa kura huku kwenye kapu la viti vya bara y this time walirun away na kwenda kushindia uzito wa unyoya wakati wao ni heavy weight?
Jk kweli ni dhaifu lakini mkubali mkatae anayo maarifa yanayomkwaza lowassa na kundi lake ndio mana mzee mpaka sasa hana raha hata ukimtazama afya yake na kwa taarifa tu anajiandaa kuelekea upinzani soon cuz hakuna njia ya kupita ccm ili afike anapopataka,jitihada zake za kuunganisha nguvu na membe na sitta zimeendelea kuzorota,hawaaminiani baada ya kusalitiana 2015 kwenye mtandao wao,membe kufanywa waziri mdogo wa mambo ya ndani hataisahau ile maishani mwake!
Kina Beatrice na huyo mwenzake wao ni watu wa kubebwa tu maskini ya mungu,hawana ushawishi wowote na wanapenda wawemo kwenye system,i told you kinana hana shida ya ukuu wa wilaya wala ubunge wa kuteuliwa brither/sister ndio mana hawezi kumtetemekea mtu kama lowassa wala jakaya,ni wao ndio wanamhitaji kwa kuwa wanaelewa ana akili nyingi sana na ni bonge la strategist na kwa taarifa yako tu aliyesisistiza kutaka kinana awe katibu mkuu ni mzee mangula na hilo ndio lilikua sharti lake ili aikubali nafasi aliyopewa but kikwazo kikubwa alikua ni kinana mwenyewe ambae mara kadhaa even before katibu mkuu aliepita mukama(lowassa ndio alimpa ulaji wa ukatibu mkuu wa wizara) jk amekua akimbembeleza bila mafanikio amsaidia kazi za ccm kama katibu mkuu and then alimbembeleza sana awe spika kumrithi sam six but kinana alikataa,you know why alikua akimchomolea mara zote hizo?????ni kwa kuwa alikua hana imani na jk linapokuja suala la lowassa na rostam,he told us even best bite on that day kwamba jakaya anawapenda sana swahiba zake hao na yeye anaona ni ngumu kufanya kazi na jk katika hali hiyo cuz hao ndio wanaoiyumbisha ccm na serikali-hicho ndiocho anachoamini kinana mpaka kesho,na alimwambia said kwamba wao wana habari ndio wamsaidie jk,said akauliza how?jibu la kinana lilikua ni kwa kuandika maovu ya kina lowassa bila kuchoka then hiyo itasaidia kumstua jk usingizini,akasisitiza otherwise mtamuona lowassa kwenye cabinet ijayo akiwa na maana cabinet mpya iliyoanza kazi baada ya uchaguzi wa 2010.
Nasisitiza tuache speculations za ajabu,tutafute facts,hon.zitto kabwe anapenda kusema "ukweli hautengenezwi bali unatafutwa" hawa watu wote tunaowazungumzia hapa wapo hai,you just take trouble tu kuwafuatilia utajua kila kitu.