Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,231
- 17,997
"Mwenye Ku- mobilize alikuwa ni Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati huo tunajenga CCM Kirumba, Mwanza nilikuwa wilaya ya Kwimba.
"Tuligawana kila wilaya itafute wadau na Chama kitafute watu kwa ajili ya ujenzi. Tulianza kuchangia. Tulifanya kampeni tulizunguka wilaya nzima. Watu walichangia ng'ombe.
"Katika wilaya yetu tulichangia ng'ombe 800. Tulijenga ule uwanja kwa ajili ya wanajeshi watu waliokuwa wakipigana vita ili watakapo rudi mashujaa kutoka vitani tuwapokee pale. Kwa hiyo wazo na Msimamizi alikuwa Chama Cha Mapinduzi"- Mzee Philip Mangula, Mstaafu wa nafasi ya katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa CCM.
Soma pia:
- Uhalali wa CCM kumiliki viwanja vya michezo
- Khalifa Said: Mali zote CCM inadai kumiliki ziliporwa kutoka kwa Watanzania, na ni muda sasa mali hizo zirejeshwe Serikalini
- Mali za CCM zilizotokana na makato kwa raia wote wakati wa chama kimoja ni haki ya nani?