Maneno ya mwisho ya marehemu Sajuki kuhusu Wastara

Maneno ya mwisho ya marehemu Sajuki kuhusu Wastara

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
MillardAyo in News

Mwigizaji Dinno alikua rafiki mkubwa sana wa Marehemu Sajuki na ndio alikua analala hospitali na Sajuki pale Muhimbili.


Ameongea Exclusive na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutoa maneno ya mwisho ambayo aliyasikia kutoka kwa Sajuki akimzungumzia mke wake ambae ni Wastara.

Kwa haraka haraka mwigizaji Wastara amesifiwa sana na watu mbalimbali kwa moyo wake wa ushujaa wa ukweli wa upendo kwa Sajuki japo walipitia matatizo makubwa na mengi kwenye maisha yao.

Millard na Dinno.

Masanja

Tukirudi kwa Dinno, namkariri akisema "tulipokuwa Arusha sisi watatu tu Sajuki alionyesha ishara ya kukata tamaa, siku moja tulikua hotelini usiku kama saa tisa hivi Wastara alikuja kuniamsha kwenye chumba changu nikaenda kwa Sajuki, alikua anaumwa sana akamwambia Wastara naomba mpigie mama niongee nae, Sajuki akamwambia mama yake mzazi kwamba Wastara nampenda sana, kanizalia mtoto mzuri anaitwa Farhini, naomba msimsumbue naomba msimpe shida yoyote amenisaidia sana, naomba mumwachie Farhini amlee amtunze mtamuona, yalikua maneno mazito sana mpaka machozi yakawa yananitoka"

Kwenye mstari mwingine Dinno amesema jambo jingine ambalo Sajuki aliliongea mwishoni ni kuhusu upendo miongoni mwa wasanii wa movie Tanzania, namkariri akisema "alikua ananiambia hebu jitahidi kuwa unakaa na wasanii, unajua sisi hatupendani Dinno ila mimi iko siku nitakuja kuropoka nikae na watu niwazungumzie tuweke upendo pamoja, tukishapendana tutafanya kitu Dinno"
1236838992_sajuki.jpg

Enzi hizo kabla hawajafunga ndoa


Lucky+Bride.jpg



Mr+and+Mrs+2.jpg

Siku ya ndoa
Wastara.jpg



sajukiWEB.jpg

Baada ya Ndo


(C)Millard Ayo website
 
MUNGU ampe nguvu mama huyu! ni pigo kweli kuondokewa na mume! inauma mnooooooo cant imagine! MUNGU atupe maisha marefu tuzilee familia zetu, amen!
 
Rest in peace Juma. Wastara,just like I said two years back.. I like the woman.
 
Hakuna kitu inauma kama kumuona mtu anakufa hivi hivi na huwezi kumsaidia....mungu awape moyo familia yake
 
Wastara ananifanya nilie kiukweli. Sijui yupo katika hali gani. Mungu ampe ujasiri wa kukabiliana na hali hii. RIP Sajiki
 
pole sana Wastara. ni huzuni sana.
 
upumzike kwa amano sajuki mungu kakupenda zaidi na pole kwa wasyara mungu akupe nguvu kipindi ichi kigumu unachopitia
 
Back
Top Bottom