Maneno aliyoniambia mama siku naoa

Maneno aliyoniambia mama siku naoa

Vijichangamoto vipo,sema mkishajuana haisumbui, akikushika hapa unakua mpole Yanaisha,nawe unajua utamshika wapi. Yaishe,mcheke,mcheke!

Nilichojifunza maisha ya ndoa ni zaidi maisha kama watu mtaelewana. Unakuta humchoki mwenzio.
Ukitaka story unataka upige na yeye,
Kucheka ucheke na yeye,
My wife is more than a friend.
Yani hivyo,kanishika hadi napenda!
Siku yakikutokea puani ndo utajua ndoa zilivyo,
Tunaziweka kumbukumbu zako hapa.
 
hahaha mkaushie broo!
[emoji1] [emoji1] [emoji1] Yale yalikua masihara! Ndio maana uzi upo jukwaa jokes mkuu.

Vp kazi ishapatikana nije nianze mkuu? Kazi kwanza story baadae, nambie mkuu, nsije nkapoteza fursa!
 
Maisha sio mapenzi tu hivyo vyote vinavurugwa na mavyuma kukaza siku hizi
Binafsi Kilele cha furaha yangu nakipata katika mapenzi.
Kama Kazi nafanya, pesa ya kula napata, burudani zingine natumia. Marafiki ninao,vyote hivyo vinanipa furaha lakini hakuna Mahala nafikia Kilele cha utulivu wa nafsi Kama nikiwa na mke wangu.
May be watu tunatofautiana mkuu!
 
Dakika za mwisho kabisa za shughuli, kabla kila mtu hajachukua njia yake.
Mama aliniita pembeni na kuniambia,"najua umeshaambiwa mengi sana mwanangu, naomba uyazingatie na haya nitayokwambia pia;

Jambo la kwanza aliloniambia ni hili, 1."usiwe na muda maalumu wa kurudi nyumbani, namna utakayomzoesha mkeo siku ukibadilisha hata kwa dharura italeta matatizo. Ni bora usieleweke muda wako wa kurudi tangu siku ya kwanza ya ndoa, naye atazoea na ataheshimu hivyo.

2. Mpe kipaumbele na msikilize mkeo yeye kwanza kabla ya mwanamke mwingine yeyote, labda niwe mimi mama yako. Mimi sitakusumbua kabisa, labda iwe imebidi. Naona umemnunulia simu kubwa kweli, lile sio pambo, tumia simu yako kuwasiliana na yeye mara kwa mara. Kabla hujamuoa ulishamzoesha kumpigia, kuchati naye, kutaniana naye mara kwa mara ulikua na kazi lakini ulipata muda wa kuchat na kuongea naye kupitia simu. Usiache kuyafanya hayo kwa kisingizio cha ubize.
Hawezi kutumia simu kucheza tu gemu na kuongea na ndugu zake. Anahitaji kuongea na kuchat na wewe kuliko mtu mwingine yeyote.

3.Mpe zawadi. Unajua nini mkeo anapenda, popote utakapokiona kama una kimudu mnunulie, hata kama ni kidogo atashukuru na atafurahi.

4.Wakumbuke wazazi na walezi wake pia. Najua mtakua mnakuja kunisalimia. Lakini pia usisahau kwenda kuwasalimia wakwe zako. Mkeo atafurahi, atajisikia kujaliwa.

5.Unapompa chochote hasa pesa ya matumizi mpe mkononi. Hata kama kalala muamshe umpe, usizoee ukiamka unaacha hela kabatini au mezani. Atakua anaiwaza meza kuliko wewe. Labda kama ni surprise.

6.Mwitikie wito, akikwambia kakumiss, akikuhitaji usichelewe, usimkatili. Usimtafutie sababu za ubize wala nini. Fanya haraka umuone, umsamdie, atulie maana hana mwingine wakumwambia shida zake ila wewe.

7.Muelewe na umvumilie mkeo. Kuna wakati wanawake huwa wanachoka na hawezi kuwa sawa kwa kukuona wewe kila siku. Hawezi kukwambia kuwa kachoka. Usimuhisi vibaya, tafuta safari au yeye mtafutie safari ili aje kwangu au kwa wazazi wake siku mbili tu ashakukumbuka na mambo yanaanza upya.

8.Usiache kumwambia unampenda. Kama ulivyokua unamtakia kabla hujamuoa, endelea na ikiwezekana zidisha kumtakia.
Ikipatikana fursa ya kuongozana naye sokoni, ibadani au popote fanya hivyo. Atajisikia raha na kujivunia wewe hata ukiwa mbali naye.

9.Mfanye mkeo rafiki yako pia msapoti na umsaidie ikiwa anataka kuanzisha au kufanya jambo lolote lenye faida kwake, kwako na familia. Ukifanya hivyo atakuwa muwazi kwako, hatokuficha lolote.

10.Mwisho nataka nikwambie mwanangu. Mwanamke ni mzuri sana katika kulipa, hivyo usimfanyie ubaya kabisa mkeo. Mfanyie wema kadri unavyoweza. Mwanamke yeyote ambaye ni mke,ukimfanyia wema kwa 10% yeye atakufanyia wema kwa asilimia 90%.
Na kwenye ubaya ndio hivyo, ukimfanyia baya asilimia 10% atakulipa kwa kufanyia ubaya 90%.
Na dhambi mbaya katika ndoa ni usaliti. Ukimsaliti na akajua. Utalea mtoto au watoto wasio wako.

Pia usiache kumuomba Mungu ajaalie na adumishe riziki, utulivu na furaha mliyoanza nayo. Nakutakia maisha mema na Mungu awe pamoja nanyi.


barikiwa katika ndoa yenu daima msitindikiwe, mama hongera kwa busara ulizozitoa kwa mwanao Mungu akujalie maisha marefu uone na vitukuu.
 
Vijichangamoto vipo,sema mkishajuana haisumbui, akikushika hapa unakua mpole Yanaisha,nawe unajua utamshika wapi. Yaishe,mcheke,mcheke!

Nilichojifunza maisha ya ndoa ni zaidi maisha kama watu mtaelewana. Unakuta humchoki mwenzio.
Ukitaka story unataka upige na yeye,
Kucheka ucheke na yeye,
My wife is more than a friend.
Yani hivyo,kanishika hadi napenda!
Safi sana mkuu. Umenifurahisha sana. Ila tambua watakuja wale 'waliojeruhiwa' kukudisappoint kutokana na experience za maisha ya ndoa zao, usiwasikilize! Mapenzi ni Matamu na Ndoa ni tamu zaidi iwapo tu MTAELEWANA. Sasa wale WASIOELEWANA huwa wanataka (na wanaombea pia) wale wanaoelewana WAVURUGANE kama wao. Huo ni USHETANI. Acheni vijana wafurahie maisha ya ndoa bwana. Kama ulikosea kuchagua au kuchaguliwa, pambana na hali yako, usitake wenzako wapitie kama unayopitia wewe!!
 
mababa yanaibukaga wakati wa matatizo na kusawazisha mambo yanapokwenda kombo!!!
Sio mzee wa mimi asee, niliwahi pata tatizo moja hivi,(mke wangu aliteleza akavunjika mguu ile nimetoka toka tu kuoa,afu sikua vizuri,nikamcheki mzee, akaniambia,kwani hukujiandaa na hilo,njoo kesho jioni tuangalie. A ananiambia njoo kesho wakati mimi shida yangu ilikua muda huo huo afu yuko serious!

Nikafanya michakato mingine faster nikafanikisha lengo.nilivyompigia simu kumwambia nimeshafanikisha,akaniambia tu, vizuri! Akaja hospital kutuona akatusaidia pia.

Ila nilimuelewa mzee, hakuwa na nia mbaya kabisa, kuna kitu alinijenga kupitia jambo lile.namkubali Sana kwa action zake.
 
Baba hakukushaur.......? Baba ndiye mwenye ushaul Wa kiume.....jambo la kumiliki Mke nadhani kwa mwanaume ni vema ashauliwe na BABA pekee..mama awashaul watoto Wa kike
Mzee wangu sio mtu wa maneno kabisa mkuu. Alinisapoti mwanzo mwisho. Kikubwa alikua anasisitiza kazi ndio kila kitu katika maisha.
 
Ukizoea kawaida tu! Unajikuta unafanya mengi Kama sio yote unconditionally mkuu!
Tatizo huwezi kujua mwanamke anataka nini. Kwa mujibu wa wanasaikolojia na ni kweli. Utamnunulia gari lakini litaendeshwa na brazamen, utamshindisha ndani atazaa na Muuza urembo au Muuza koni, aargh ni mengi ya kuchosha.
 
Hahaa lakini usizoee sana wakijua umeoa hukuwachukua wao wivu unawaingia wanazidisha manjonjo, hujawahi ona ke akipata mchumba au kuolewa ndiyo wengine wanajitokeza eti wanampenda wakati siku zote walikuwa wanamuona [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
Mara nyingi Siku za sikukuu ndio huwa tunaenda kusherehekea kwa wazazi, tunachagua leo twende kwa nani. Anasukumiziaga mimi ndio niamue. Nami huwa nabalansi tu,hii huku ijayo Kule.

Japo hata siku za kawaida huwa inatekea mara moja moja.

Sema mimi kwa wazee wangu ndio naenda Sana tu mara kibao nikijisikia tu. Najua hata yeye huwa anaenda,na nimempa hiyo ruhusa,akijisikia kuwamiss anambie tu na aende.
Sema wazazi wake huwa wanampiga biti asiwe anaenda enda,afu ananiambia kila kitu alivyo mzembe kwangu huyu binti.hata mama mkwe akimtania utani ambao hawezi kusema mbele yangu,lazma nambie,
Namuangaliaga tu,afu nacheka, afu napenda! Afu najisemea kimoyo moyo,hiyo ni moja ya sababu ninayokupendea mke wangu, hujui kunificha kitu!
 
May be it's true what you are saying Lakini kwangu now haipo hivyo, nilikuwa nafunua funua Mahali unconsciously nikafunua page ya wosia wa mama. Nikawa interested Sana kiasi cha kuamua ku-shere.

May be umeni-quot hivyo kwa sababu nimeandika nikiwa na furaha Sana Kiasi hadi umeni-notes vice versa!


Mkuu huo wosia wa mama uliuandika ukiwa wapi hasa?

Maana nataka nione ukiwa harusini wanapotoa wosia mtu anapata muda wa kuchukua notebook na kuandika eti wosia?!!!It is really beyond me!

Nachojua harusi zetu hizi za kiswahili,siku ya sherehe pale mbele,no one has that time ya kuchukua notes!

Nina wasiwasi na authenticity ya hiyo note-taking activity to begin with!
 
Safi sana mkuu. Umenifurahisha sana. Ila tambua watakuja wale 'waliojeruhiwa' kukudisappoint kutokana na experience za maisha ya ndoa zao, usiwasikilize! Mapenzi ni Matamu na Ndoa ni tamu zaidi iwapo tu MTAELEWANA. Sasa wale WASIOELEWANA huwa wanataka (na wanaombea pia) wale wanaoelewana WAVURUGANE kama wao. Huo ni USHETANI. Acheni vijana wafurahie maisha ya ndoa bwana. Kama ulikosea kuchagua au kuchaguliwa, pambana na hali yako, usitake wenzako wapitie kama unayopitia wewe!!
Asante mkuu
 
Tatizo huwezi kujua mwanamke anataka nini. Kwa mujibu wa wanasaikolojia na ni kweli. Utamnunulia gari lakini litaendeshwa na brazamen, utamshindisha ndani atazaa na Muuza urembo au Muuza koni, aargh ni mengi ya kuchosha.
Labda ni kweli unachosema. Ila nahisi inategemea amelelewaje.
Mfano Mimi nilikooa,yeye ndie mtoto wa mwisho. Kaka na Dada zake wote wameolewa na kuoa.

Kila akienda kwa mama yake kumsalimia, akirudi nikimuuliza kakwambia nini mama.moja ya neno ambalo lazima aniambie ni kuwa kamwambia, atulie kwenye ndoa,nisiwe nakukaripia hata ukinikosea, niongee na wewe taraatibu na vitu Kama hivyo.
Na hata akikutana na Dada zake ni hivyo hivyo.

Kweli inahitaji akili sana kuishi na mwanamke lakini malezi nafikiri yanachangia pia japo sina uhakika Kama ni malezi Tabia binafsi.
 
Back
Top Bottom