Kasoro zipo mkuu, kununiana,kuulizana maswali ya ajabu.
kama navochelewa kurudi huwa hapendelei Sana na huwa anasema ndio uzuri wake.
kama leo lazima tu ntachelewa sababu ya game ya Barça na Chelsea. Hivyo huwa hapendi sana navyorudi usiku Sana.
Pia leo ili nisimkere Lazima nile naye chakula,nipige naye story kidogo ndio naende kibandani kucheki mpira.
Yeye ndio sababu hata game ya jana sikuangalia.
Siku nyingine huwa ananigomea namsikiliza,siendi.natulia tu home tunaangalia movie zake za kikorea au kihindi. Kama kuna mechi nakua naangalia kumridhisha.sitaki kum-dictate japo najua naweza,ila soioni sababu ya kufanya hivyo. Sitaki kushindana naye,kuepusha matatizo. Maana yeye pia ni msikivu na muelewa kwangu. Na nina furahia hivyo.
Binafsi sitaki kuupa mpira thamani zaidi ya ndoa. Sitaki hata awe anacheza nani, binafsi sitaki.
japo siku nyingine mwenyewe huwa ananiambia nenda kaangalie wenzako wasije sema nimekupa limbwata bure.namjibu,waseme mara ngapi!? Tunacheka yanaisha.
Mambo mambo yapo mkuu. Me naona kawaida.