Pablo Blanco
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 7,328
- 6,656
Mzima???I wish yule jamaa apite huku
Mzima???I wish yule jamaa apite huku
Awwww. Mama watoto yuko wapi mkuu?Katika video niliyoangalia mara nyingi ni ya harusi yangu...napomkumbuka mama watoto wangu huwa naangalia.
Mama yangu aliniambia maneno mazuri sana..alisema hiyo ndio ndoa yangu pekee atakayoshiriki.
In Heaven for sure.Awwww. Mama watoto yuko wapi mkuu?
Pole sana jamani. Aendelee kupumzika kwa amani wifi.In Heaven for sure.
Mkuu alitoa jibu kwa hili?Baba hakukuambia kitu?
Niko poa kakaMzima???
Pole,May her soul rest in eternal peaceIn Heaven for sure.
😀😀😀😀😀😀Kila cku kuwafurahisha wanawake tu! hebu weka na jins ya kumfurahisha mume
Pole sanaIn Heaven for sure.
mama yako ni genious i salute her!Dakika za mwisho kabisa za shughuli, kabla kila mtu hajachukua njia yake.
Mama aliniita pembeni na kuniambia,"najua umeshaambiwa mengi sana mwanangu, naomba uyazingatie na haya nitayokwambia pia;
Jambo la kwanza aliloniambia ni hili, 1."usiwe na muda maalumu wa kurudi nyumbani, namna utakayomzoesha mkeo siku ukibadilisha hata kwa dharura italeta matatizo. Ni bora usieleweke muda wako wa kurudi tangu siku ya kwanza ya ndoa, naye atazoea na ataheshimu hivyo.
2. Mpe kipaumbele na msikilize mkeo yeye kwanza kabla ya mwanamke mwingine yeyote, labda niwe mimi mama yako. Mimi sitakusumbua kabisa, labda iwe imebidi. Naona umemnunulia simu kubwa kweli, lile sio pambo, tumia simu yako kuwasiliana na yeye mara kwa mara. Kabla hujamuoa ulishamzoesha kumpigia, kuchati naye, kutaniana naye mara kwa mara ulikua na kazi lakini ulipata muda wa kuchat na kuongea naye kupitia simu. Usiache kuyafanya hayo kwa kisingizio cha ubize.
Hawezi kutumia simu kucheza tu gemu na kuongea na ndugu zake. Anahitaji kuongea na kuchat na wewe kuliko mtu mwingine yeyote.
3.Mpe zawadi. Unajua nini mkeo anapenda, popote utakapokiona kama una kimudu mnunulie, hata kama ni kidogo atashukuru na atafurahi.
4.Wakumbuke wazazi na walezi wake pia. Najua mtakua mnakuja kunisalimia. Lakini pia usisahau kwenda kuwasalimia wakwe zako. Mkeo atafurahi, atajisikia kujaliwa.
5.Unapompa chochote hasa pesa ya matumizi mpe mkononi. Hata kama kalala muamshe umpe, usizoee ukiamka unaacha hela kabatini au mezani. Atakua anaiwaza meza kuliko wewe. Labda kama ni surprise.
6.Mwitikie wito, akikwambia kakumiss, akikuhitaji usichelewe, usimkatili. Usimtafutie sababu za ubize wala nini. Fanya haraka umuone, umsamdie, atulie maana hana mwingine wakumwambia shida zake ila wewe.
7.Muelewe na umvumilie mkeo. Kuna wakati wanawake huwa wanachoka na hawezi kuwa sawa kwa kukuona wewe kila siku. Hawezi kukwambia kuwa kachoka. Usimuhisi vibaya, tafuta safari au yeye mtafutie safari ili aje kwangu au kwa wazazi wake siku mbili tu ashakukumbuka na mambo yanaanza upya.
8.Usiache kumwambia unampenda. Kama ulivyokua unamtakia kabla hujamuoa, endelea na ikiwezekana zidisha kumtakia.
Ikipatikana fursa ya kuongozana naye sokoni, ibadani au popote fanya hivyo. Atajisikia raha na kujivunia wewe hata ukiwa mbali naye.
9.Mfanye mkeo rafiki yako pia msapoti na umsaidie ikiwa anataka kuanzisha au kufanya jambo lolote lenye faida kwake, kwako na familia. Ukifanya hivyo atakuwa muwazi kwako, hatokuficha lolote.
10.Mwisho nataka nikwambie mwanangu. Mwanamke ni mzuri sana katika kulipa, hivyo usimfanyie ubaya kabisa mkeo. Mfanyie wema kadri unavyoweza. Mwanamke yeyote ambaye ni mke,ukimfanyia wema kwa 10% yeye atakufanyia wema kwa asilimia 90%.
Na kwenye ubaya ndio hivyo, ukimfanyia baya asilimia 10% atakulipa kwa kufanyia ubaya 90%.
Na dhambi mbaya katika ndoa ni usaliti. Ukimsaliti na akajua. Utalea mtoto au watoto wasio wako.
Pia usiache kumuomba Mungu ajaalie na adumishe riziki, utulivu na furaha mliyoanza nayo. Nakutakia maisha mema na Mungu awe pamoja nanyi.
Ujumbe mzuri.
Umeona eee be careful yaani niafadhali uonekane umetaliwa na mke lakini wewe unalo moyoni ufanyalo, na amani niyako wewe na familia yako hao siku mambo chumvi hutawaona wataanza tulijua tu wanawake hawaaminiki kumbe chanzo ni mme hakusimama katika nafasi yake wengine tupo humo humo tumiaka twingi tu milima na mabonde tunavuka tumeziba pamba fanya unachoona kina kupeleka mbele na kupata amani yenu basi.Kweli kabisa mkuu, asilimia kubwa ya matatizo yanasababishwa na ushauri mbaya wa makundi yetu,baadhi ya marafiki zetu hata ndugu.
Laiti Kama ningekua nasikiliza maneno ya watu wa nje, sijui Kama leo hata ningekua na ndoa.ni kushauriana Ujinga tu.mwanzoni Ilinipa kidogo kukabiliana nayo.
hasa ukikaa sehemu ambayo wengi wanakujua/wanawajua kelele za nje zinakua nyingi kidogo, kiasi msisimama imara zinaweza zikamchukua mmoja went au wote na kuwapoteza.
Kukaa mbali na Mahali unapojulikana kunaheshima kidogo. Asilimia kubwa kunapunguza vioja.
kila mtu anakua na lake na unaheshika kiasi chake. Japo changamoto bado zitakuwepo sio sawa na sehemu watu wanaokujua Sana. Mazoea na watu wa nje ya taasisi yakizidi nayo sumu.
ila bado msimamo na kujua nini unafanya na nini unataka ndio nguzo nafikiri,nahasa Kama wote mnaelewana.
Fanya kama umekosea umuwekee karibu asome ila walivyo wabishi jamani[emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39]I wish yule jamaa apite huku
Kumbe umeoa si ulinambia ndiyo unasakanya, [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hongera hajambo my wiKatika video niliyoangalia mara nyingi ni ya harusi yangu...napomkumbuka mama watoto wangu huwa naangalia.
Mama yangu aliniambia maneno mazuri sana..alisema hiyo ndio ndoa yangu pekee atakayoshiriki.
Pole sana nilikuwa sijafika huko R.I.P , Mungu akupe faraja tena ila yeye ndiye ajuaIn Heaven for sure.
Sijui nicopy afu nimpestie uko wasap then nijifanye nimekosea kutuma,[emoji23]Fanya kama umekosea umuwekee karibu asome ila walivyo wabishi jamani[emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39]
Daaa!!!! We jamaa kama Mimi kabisa,katika vitu ambavyo sipendi ni harusi huwa naona kama ni ushamba flani hivi,hahaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Sikufanya harusi mkuu, nilifanya ndoa tu kawaida.
Binafsi sikutaka kabisa harusi huo ni mmoja katika msimamo wangu niliouandika katika kitabu changu cha kumbukumbu.japo ingelazimu ningefanya harusi. Ila nilimwambia wife usishangae nkakuacha peke yako kati kati ya shughuli. sijui ni kama ni sababu ya umasikini au ushamba wangu ndio maana naliogopa kufanya harusi, sijui!
sikuwa napenda mambo ya harusi kabisa mkuu.hata nikiona watu wanafanya harusi nilikua nawaza Sana, hivi namimi kuna siku itakua hivi. Nafsi yangu ilikataa!
japo nilijua itakua hivyo ila wife naye nilimpanga ikiwezekana kikombe hiki kituepuke. nilimpanga naye akaniunga mkono.
na hata mama kabla sijaoa nilikua namwambiaga,sipendi kufanya harusi.
Mzee yeye hakua na shida kabisa,hanaga maneno.
Nilikua nawaza wazazi wa wife, na watu waliolikwa kwenye vikao vyao watakubali???
Kama utani tukatoa Kama wazo au ombi kwa mshenga.sikutegemea Kama tungeeleweka,sijui mpaka leo aliwafikishiaje na walijadiliana vipi. Lakini Mungu mkubwa,haiwi Haiwi ikawa. tukakubaliwa.
Hakukua na kwenda ukumbini wala kukodi Magari.na mwisho wa shughuli kila mtu alichukua njia yake, kabla hatujawaaga wazazi wetu wote kwa mara ya mwisho ili kila mtu akalale kwa mwenzie official kwa mara ya kwanza ndio mama akaniita na kuniambia hayo maneno.
Japo watu walioalikwa changanya na wapita njia walikua wengi wengi lakini haikuwa ile ya kuuzishana sura kiviiile! Jambo ambalo nilikua silipendi.
Sidhani Kama ilikua harusi ile. Me huwa naona ni ndoa nikifananisha na wanaofanya harusi.
Maneno hayo ya wosia niliyaandika nikiwa home siku chache baada ya ndoa.sababu ni kawaida yangu kuandika vitu tangu niko shule sec,ndio nilikorithi hiyo tabia.
Baada ya ndoa nilichukua kitabu changu nikaanza kujikumbusha na kuandika yaliyotokea siku ile na niliyoambiwa siku ile.
Kifupi mi napenda kuandika. Chochote kitakachonitokea kikanigusa lazima niandike.
Sijui Kama nimekujibu kidogo mkuu?