Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Namkumbusha hamis77 na genge lake kwamba mwamba tunaye hata baada ya sikukuu.
Ila kiasi flani machale yananicheza maana kuna liverkuu tunacheza nao kabla ya christmas.
oya 7hag alishakamilisha vigezo vyote vya kufukuzwa, kilichobaki Sisi Kama wahafidhina wa EPL ,tunamuombea abaki ili muendelee kuteseka


Kwasasa tunafunga na kuomba asifukuzwe


Ukweli tayari umeshajulikana Hakuna asiyejua humu ERIK 7HAG Ni kocha mwenye uwezo mdogo


Kuna anayebisha humu


Nawatakia kila la kheri dhidi ya Liverpool jumapili
 
MAN UNITED IPO JUU YA KILELE CHA ANGUKO LAKE:

((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((((

Kundi lenye timu za Copen hagen FC, Galatasaray, Bayern Munich na Man u yenyewe. Tusi chafu ni United kumaliza wa mwisho akiwa na point 4 pekee. Safari ya United UEFA champions league imekuwa na hitimisho la fedhea.

United imefungwa goals 15 katika mechi 6. Imefanikiwa kushinda mechi moja na kutoa sare moja.

Hata kama "Ten Hag" akifunguliwa mlango wa kutokea. Atakuwa ametolewa tu kama mbuzi wa kafara. Tatizo la Manchester United limejificha katikati ya msemo huu.

"You can't be a champ for life, one day you'll go off and some else will come." Yaani, "huwezi kuwa bingwa milele, lazima siku moja uondoke ili bingwa mwingine aje."

Kuna mashabiki anguko la timu wanalifungamanisha na wamiliki kutotoa pesa nzuri ya usajili. Hii ni "dhana potofu" ambayo haitakiwi kupata nafasi ya kuishi kwenye masikio ya mtu mwenyewe utimamu wa fikra.

Hii dhana inakufa "KIFO" cha asili kwa fact hii. Katika misimu 10 iliyopita, United ipo katika top three ya vilabu vilivyotumia pesa ndefu kwaajili ya usajili kwa timu za England.

Vipigo mfululizo inavyokutana navyo United kila kukicha. Kwa mwenye jicho lililobeba utukufu wa kisoka. Ile ni ishara ya Man u kuwa juu ya kilele cha anguko lake. Kila timu duniani huwa inapitia anguko hili.

Liverpool ilikaa miaka 30 bila ubingwa wa EPL. Mancity miaka 44, Chelsea miaka 50, Arsenal ina ukame huu mwaka wa 19 sasa.

Madrid na ubabe wake wote kwenye soka la ulaya. Amewahi fikisha miaka 7 mfululizo bila laliga, na miaka 12 bila ndoo ya UEFA champions league.

Leo simanzi imejenga ngome old Trafford, kwa kuwa "UTUKUFU" hautaki tena kuwa sehemu ya Manchester United.

Halafu wikiend hii Manchester United yupo ugenini huko kwenye uwanja mgumu "Anfield" ili kuweza kuibiri Liverpool ambayo msimu huu ipo

Kila lenye mwanzo lina mwisho. Ila mwisho wa anguko la Manchester United umekuwa wa kuumiza sana kama yalivyo maisha ya chid Benzi.

Imeandikwa na Benjamin Bruce Sport's

Tu-Follow Benjamin Bruce Sport's
 
Kitendo Cha Man u na Newcastle kuburuza mkia kinafanya nafasi ya Ligi ya Uingereza kupata nafasi ya kupeleka nafasi ya 5 UCL ipotee ,Sasa inabaki kwa Germany na Italy

Only top 2 get a 5th place in UCL

1. Germany, 13.36
2. Italy, 13.14
3. England, 12.13
4. Spain, 12.06
5. France, 10.42

Manjesta na Nyukasto mmeitia aibu Ligi ya malkia
 
Hizi ndio timu zilizofuzu hatua ya 16 bora kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya 2023/24.

Walioongoza Makundi
Bayern
󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Arsenal
Real Madrid
Real Sociedad
Atlético
Dortmund
󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Man City
Barcelona

Waliomaliza nafasi ya pili katika Makundi
Copenhagen
PSV
Napoli
Inter
Lazio
PSG
RB Leipzig
Porto

Walioburuza Mkia

1.Manjesta
2.Nyukasto
 
Mr.Era comes to an end

Apewe muda zaidi View attachment 2841269
JamiiForums1150051858.jpg
JamiiForums-2004347002.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Liverpool Tulijiandaa kuwakaribisha wenzetu wa Man utd huku Yuropa ili tujipigie vibonde kwa pamoja ila nasikia Wamepata ajali mbaya sana maeneo ya Mlima Uefa na wamekufa hapo hapo miili haitamaniki. Poleni kwa wafiwa
 
Back
Top Bottom