Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Alejandro Grimaldo alikuwa mchezaji huru mwezi June mwaka huu baada ya kumalizana na SL Benfica, baadhi ya vilabu vikawa vinazubaa tu - Xabi Alonso akamuona akamchukua mwezi wa saba.

Grimaldo ni fullback ya kuogopwa sana sababu ana uwezo mzuri wa kukaba na kupanda na kupiga mipira ya adhabu, kwenye faulo ni mchawi sana.

Amecheza michezo 9, goli 3, pasi 3 za mwisho.

Jonas Hofmann ana miaka 31 amecheza muda mrefu pale Borussia Monchengladbach, kumbe release clause yake ilikuwa ni €10m tu.

Xabi Alonso akaomba pesa kipengele hicho kikavunjwa akamchukua.

Jonas Hofmann yupo kwenye ubora mkubwa sana na ni mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Xabi Alonso, mpaka sasa amecheza mechi 9 na kufunga mabao 5 na kutoa pasi 3 za mwisho kwenye Bundesliga msimu huu.

Wakati mnawazungumzia akina Victor Okoh Boniface, Florian Wirtz, Exequiel Palacios, Edmond Tapsoba, Jeremie Frimpong, Granit Xhaka - msiwasahau hao sababu nao wamechangia Leverkusen kuwa kileleni mpaka sasa.

Xabi Alonso things.

Man U tumerogwa na nan?

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Tumchukue huyu au

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Vitu ambavyo kocha wa man united Ana tetewa kua amekuta wachezaji wabovu mwamba amekuta leverkusen ina wachezaji wale wale walio kua ktk bad seasons zilizo pita ila ame ongeza baadhi ametengeneza pattern yake ya uchezaji watu Wana flow nayo Ana tumia mbinu ambazo zina fit kwa wachezaji alio wakuta ameongezea vitu vichache tu
Km kwenye high pressing
Kupiga pasi ktk shape ya pembe 3 kwenye space za mpinzani
Full back uhusika ktk build up ya ushambuliaji
Wachezaji ku switch position wakati game ikiwa in flow kwenye ushambuliaji
Kusaidiana kufanya coverage pale mchezaji husika akiwa out of position hasa ktk back line
Kila mchezaji uhusika kwenye mashambulizi team ikiwa Ina mpira na kuzuia team ikiwa haina mpira wanafanya quick covering kwenye njia na huku wakifanya 1v 1 marking
. Vitu vipo wazi na vinaonekana kabisa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Uko sahihi brother, Huyu kocha kafanya makubwa sana na AJAX AMSTERDAM na soka lililokuwa linapigwa pale AJAX kwa tuliokuwa tunafuatilia soka la UHOLANZI tuliliona. Basi tu Manchester United nako kuna changamoto zake nyingi tu.

Bodi yenyewe inatangaza kuiuza timu na Wanunuzi tena wa maana kabisa wanajitokeza kuinunua timu ghafla bodi hiyohiyo inabadilika haitaki kuiuza.

Manchester United haikuwa timu ya kushindwa kutwaa taji la EPL kwa miaka yote hiyo zaidi ya 10. Makocha wote walioingia baada ya mzee Fergie kuondoka ina maana wote kuanzia David Moyes ni wabovu kiasi cha kushindwa kuipa taji timu?

Huyu Louis Van Gaal kabla ya kuitwa timu ya Taifa ya Uholanzi alitoka kuipa Bayern Munich ya Ujerumani mataji ya Bundersliga, Huyu huyu kocha wa sasa wa Manchester United amekuja United akitoka kuipa taji AJAX AMSTERDAM.

Mimi naamini pamoja na maswahibu anayopitia kwa sasa kocha huyu, lakini pale Manchester United kuna kitu hakiko sawa.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Nimependa uchambuzi wako ,
 
Ten Hag: "I want to play from the back and we try that in every game, but like against Man City, if they are good at pressing, it's a good option to go direct. We want to press, then go direct, because we have the players who are very good at it."
 
Ten Hag: "I want to play from the back and we try that in every game, but like against Man City, if they are good at pressing, it's a good option to go direct. We want to press, then go direct, because we have the players who are very good at it."
Ni kama Ten Hag ameshaanza kushout hawelewi wachezaji wake
 
Ni kama Ten Hag ameshaanza kushout hawelewi wachezaji wake
Hakuna kocha hapo. Anajisifu msimu uliopita alicheza vizuri wakati ni game za kuhesabika tu. Huyo kocha alikuwa mzuri kwa league ya watoto huko Uholanzi huku kasha fail.

Bodi ya Man u wasichelewe kufanya maamuzi walete kichwa kingine.
 
Hakuna kocha hapo. Anajisifu msimu uliopita alicheza vizuri wakati ni game za kuhesabika tu. Huyo kocha alikuwa mzuri kwa league ya watoto huko Uholanzi huku kasha fail.

Bodi ya Man u wasichelewe kufanya maamuzi walete kichwa kingine.
Sahihi kabisa ,Game alizocheza vzr zinahesabika

Utofauti wa last season na msimu huu

Ni Rashford kuwa form

De gea kuokoa Sana

Mashabiki wengi wanaangalia matokeo tu ndio maana hawakushtuka last season ,Ni wachache ndio walijua hili bomu litamlipukia soon sababu Rashford haeleweki na tayari alishaanza kumpiga Vita Degea

So Rashford arudi default settings ,pia muondoe Degea , unaipata Hii man u ya Sasa
 
Ni Nini Cha Kawaida Kati Yao? Walizungumza Ukweli kuhusu Manchester United na walikosolewa...


Louis van Gaal: "Man Utd ni klabu ya kibiashara, tofauti kabisa na Bayern. Kwa Bayern soka ni kitu muhimu zaidi, si pesa, kama ilivyo United."

Louis van Gaal : "Katika Bayern, watu wanaosimamia soka ni wanaume. Nilifurahia hilo kila mara. Kwa upande mwingine, huko Manchester United, ed Woodward alitawazwa kama mkurugenzi mkuu - mtu asiyeelewa kabisa soka ambaye hapo awali alikuwa benki ya uwekezaji. ."

Alexis Sanchez : "Baada ya kikao cha kwanza nilirudi nyumbani - nilimwambia wakala wangu 'huwezi kuvunja mkataba ili kurejea arsenal?' Wakati mwingine kuna mambo ambayo hutambui mpk najiuliza nilifika vipi man utd, na nakumbuka kipindi cha kwanza cha mafunzo nilichokuwa nacho, niligundua mambo mengi."

Zlatan ibrahimovic : "Kila mtu anaifikiria Man utd kama klabu ya juu, mojawapo ya matajiri na yenye nguvu zaidi duniani na nikionekana kutoka nje ilionekana hivyo kwangu. Lakini mara nilipokuwa huko nilipata mawazo madogo, yaliyofungwa. "

Jose Mourinho : "Mojawapo ya kazi nzuri zaidi ya maisha yangu ilikuwa kumaliza rasmi nafasi ya pili nikiwa na man united katika ligi kuu. Ninaendelea kusema hivi kwa sababu watu hawajui kinachoendelea nyuma ya pazia."

Cristiano Ronaldo : "Manchester Utd haikupiga hatua. Real Madrid na Juventus zilifuata teknolojia ya hivi majuzi, miundombinu. Kila mara walijaribu kusonga mbele hata katika masuala ya mazoezi, lishe na jinsi ya kupata nafuu kutokana na michezo. Man United iko nyuma ya klabu kama hizo."

Cristiano Ronaldo : "Naitakia klabu bora, mashabiki wanastahili ukweli. Una mambo ndani ya klabu ambayo hayasaidii Man Utd kufikia kiwango cha juu kama Man City, Liverpool na hata sasa Arsenal."

MAWAZO?
 
Tutaongea lugha moja tatizo la United ni kubwa kuliko tunavyodhani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…