Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Wengine muwe mnaenda kulima njegere tuu
 
Na katika hali kama hii...kinachofuata ni kukaziwa adi na watoto wadogo yaani apa kina palace na wolves wale....maana wanaamin wakikomaa kwako wanachukua points vizur tu kwakuwa wanajua hivi sasa Man Utd ni papatu papatu na hamshindi kwa uwezo wa timu kama timu.

Dah!...hii timu yenu ni bora ingeuzwa tu, mie sio shabiki wa united lakini na Stick na hoja ya G.Neville...kuwa shida ipo kuanzia hierach adi kwa wamiliki wa timu.

Yani...Carragher anasema wachezaji ndo wenye shida lakini NACHOKIONA NI KUWA WACHEZAJI WENU HAWAWEZI KUFANYA ZAIDI YA PALE TULIPOONA...tukiaanzia mechi zote na mahasinu wenu mlizopigwa 6-3 kwa city, ile ya 7-0 kwa liver(tena ilikuwa ni liver ile mbovu) na ata jana 0-3 kwa city pale OT. Na adi kufikia timu kubwa kama united kuwa na wachezaji wasioendana na hadhi ya timu...inatokana na POOR SCOUTING NA RECRUITMENT DEPARTMENT YA TIMU YENU(Ambapo ndio apa alipomaanisha NEVILLE...YAANI TATIZO LA KIUONGOZI)...Hapa naenda mabali zaidi kwa kusema Either MNASAJILI WACHEZAJI WA KAWAIDA WASIOOENDANA NA PROJECT YA CLUB au WANAOSAJILIWA HAWAJAKIDHI MAHITAJI YA FALSAFA(STYLE YA UCHEZAJI) YA MAKOCHA WENU....MAANA UKIANGALIA KATIKA MECHI ZOTE HIZO ZA 6-3, 7-0, ile ya madogo Copenhagen ushindi wa papatu papatu na ata ile jana kupigwa na City OT 0-3....WAEZA UKAONA KABISA UNITED HAIELEWEKI INATUMIA FALSAFA/STYLE GANI YA KIUCHEZAJI...NA KOCHA KAMA TEN HAG NI KOCHA MKUBWA NA AMBAYE KAPITA KWENYE TIMU KADHAA ULAYA IKIWEMO BAYERN NA AJAX....TOKEA ALIVYOKUWA BENCHI LA UFUNDI BAYERN....HIVYO HUWEZ SEMA ETI HANA FALSAFA YAKE SIO KWELI, ISIPOKUWA HAPO WACHEZAJI WAMESHINDWA KUENDANA NA FALSAFA YAKE YA KIUCHEZAJI NAHISI.
 
Maisha yanitese na Man U initese pia.??.

Nimeamua kurudi nyuma kidogo..mechi zetu hata hazina mzuka tena
Mkuu sio mzuka tu KIUKWELI MANCHESTER DERBY...haivutii tena maana ni ONE SiDED FOOTBALL mshindi anafahamika....na sio ilo tu Man united wanashindwa ata kuonyesha kandanda safi dhidi ya wapinzani wao Man City...

Hivyo DERBY YA MANCHESTER IMEPOTEZA MVUTO KULINGANISHA NA DERBY NYINGINE PALE ENGLAND KAMA NORTH LONDON DERBY...Na tatizo ni nyie Hampo tena katika Level ya kiushindan mliyokuwaga nayo pale EPL.

Wee ona pamoja na chelsea kuwa vibaya lakini atleast kampa arsenal Game nzuri ile juzi...Derby yao ilivutia kiukwel.

Kiukwel naona atakayempa city mchezo wa kiushindani msimu huu ni LIVERPOOL na mchezo utakuwa mkali maana LIver nao wamerud kwenye viwango vyao kulinganisha na msimu uliopita...kwa arsenal sidhani washukuru walishinda ile mechi ya pale kwao Emirates ila Etihad watapata tabu wale pia....ukizingatia KDB atakuwa kesharudi
 
Tena uyo dogo wenu PELLISTRI Ndo aliongea pumba kabla ya mechi ya jana....kuwa "Akitokaga na girlfrend wake kuzunguka pale jijini manchester haonagi mtu ata mmoja akiwa amevaa jezi ya City"....Pep alivyoulizwa ilo swali na pundit nae akajibu kisiasa kuwa " Atajaribu kuwauliza Puma kwanini jezi za Man City zimeisha madukani pale manchester".

Ukitizama apo...unaona kabisa yule dogo aliropoka...kuridhisha media lakini sio kweli kwamba uzunguke jiji lote la Manchester eti usione raia aliyevaa jezi ya City....No tena BIG NO....Maana kiasili hizi timu zina mahali zilipoanzishwa MFANO ATA PALE MERYSEYSIDE...INAFAHAMIKA KUWA LIVER NDIO MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA NA MAKOMBE MENGI LAKINI BADO EVERTON WANA MASHABIKI/WAZAWA WAO JAPO SIO WENGI kulinganisha na LIVERPOOL...Sasa how Come useme Hakuna shabiki wa City katika jiji la manchester??....Na wale wanaoingiaga Match Days za kila weekend pale etihad wanatokaga wapi??...

KWANZA JIJI LA MANCHESTER LINA VITONGOJI VIKUBWA VIWILI...ACHILIA VENGINE VIDOGO VIDOGO KAMA SALFORD...NAVYO NI STRETFORD...AMBAPO HAPO NDO MAN UNITED ANA NGOME NA WAZAWA WENGI WA HAPO NI UNITED LIA LIA....PIA STOCKPORT ALIPOZALIWA FODEN...AMBAPO WAZAWA WENGI WA HAPO NI CITY

Pia yule mtoto anataka kutuaminisha haoni jezi za City Jijini Manchester...Na hawa watu wote hapo chini wanaishi wapi labda??...au sio MANCHESTER HII HAPO PICHANI...NA KAMA HAPO NI MANCHEATER SASA INAWEZEKANA VIPI USIONE JEZI YA CITY KATIKA JIJI LA MANCHESTER KAMA ALIVYOJINASIBU PELLISTRI.


 
Ten hag kutimuliwa amepewa odds 10 πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 

Attachments

  • Screenshot_20231030_102718_1xBet.jpg
    65.4 KB · Views: 8
Tuliwaambia mpira wa janja janja ni mbio za sakafuni

Mkasema 7Hag nomaaa
Wazee wa gengeni
 
ETG kipara feki

Ni tapeli, jasusi au profile zote hizi anazo?
Mgunda yupo vizuri kuliko huyu muhuni
 
Kutoka kwa Privadinho

Leo kiukweli Ten Haag ameniudhi. Kwanza amenifanya niwe na wasiwasi mkubwa na capabilities zake as coach

Mimi sina uwezo mkubwa kiukufunzi kuliko yeye lakini naweza kufanya tathamini ya kile ambacho ameleta mezani

Leo amesema John Evans ameanza mbele ya Varane kwa sababu za kimbinu, akamweka Regulion bench ambaye ni Natural left back huku akianza Lindelof upande huo.

How dare against Man City? Ina fact kuna kiburi kipo nyuma yake. Nahisi kuna sura ua Ferguson anataka kuivaa.

For me its too early kwa Ten Haag hata kuvaa soksi chafu za Fergie achilia mbali viatu vyake.

Ukitazama mentality ya wachezaji wa Man United wapo so stressed. Mtazame Anthony alivyoingia? Ni kama aliingia na jazba? Why? Tazama drama za Sancho?

Haya rudia tena Interview za Ronaldo na Dressing room ya Ten Haag. Kuna kaubabe au niseme kajeuri ambako Ten Haag anajipa.

Kitendo cha management kumwamini na kumpa mamlaka Ten Haag sidhan kama kina afya kwa Ten Haag

Naelewa why Management ya United ilimpa mamlaka Ten Haag, ni kwa sababu kulikuwa na presha kubwa kwa Ex coaches wa United walilalamika kuwa hawasikilizwi.

For its bad timing, wamefanya jambo sahihi, ila they are having average coach.

Tazama sajili zake, angalia game plan zake. Hata kwenye sub binafsi zinaambatana na ubabaishaji au ubahatishaji.

For me Ten Haag is not right man for the Job. Anatumia leseni ya babu yake kuendesha gari.

Atatuua kwa stress huyu baba. Hana character wala personality ya kubeba image ya United kwenye tough moment. We need strong and gaffer with amazing exposure.

Credit: Privaldinho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…