Nimeona watu humu wakimshukia Onana kama mwewe. Niseme tu timu yetu ina matatizo mengi sana ukimaliza kusolve tatizo hili linaibuka hili. Tulianza na beki tukaja kiungo, tumekuja staiker leo tumepata kiungo na straiker beki zimekuwa mbovu.
Kwa uwezo wa shoot stopping naweza sema De gea hakuna kipa anamfikia Duniani. Ila kuna aina ya mchezo De gea hawezi na ndio maana De gea wa utd na De gea wa timu ya taifa ya Espain ni watu wawili tofauti. Hicho ndio kilichomfanya apoteze number timu ya taifa rejea fainal za kombe la dunia kule kwa Putin.
Kuhusu Onana ni mtu asiyejua mpira pekee ndiye anamuona kipa mbaya. Onana kacheza na ajax yenye mafanikio, amecheza fainal ya europe legue 2017 dhidi ya utd, amecheza intermilan tumeona kiwango chake hadi fainal ya UEFA na tuliona jinsi city walivyoteseka siku ile. Onana anabahati mbaya ya kucheza na beki mbovu ya utd bahati mbaya zaidi wale beki wenye nafuu wanaandamwa na majeruhi.