Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ni kweli mkuu Antony watu wanamdharau sana ila ki ukweli timu yetu kule mbele yote haikuwa vizuri.Antony alijitahidi sana kubalance timu na ndio maana mechi zote alizofanyiwa sub tulipoteza au tulidroo. Sikumbuki mechi yeyote ambayo Antony alifanyiwa sub na tukashinda au kutoa droo na maanisha aliyeingia badala yake alitusaidia kusawazisha magoli au kushinda mechi, nipo tayari kusahihishwa.
 
Akitua Ambrat nina uwakika msimu ujao tutatoa upinzani mkali nmo kwa Man City naamini hawatakuwa na hamu ya kukutana na sisi. Kwa kikosi hiki kila mchezaji atahimarika.
Msimu ujao bingwa siyo Man City. Bingwa itakuwa kati ya Man United, Arsenal au Liverpool.
 
Kwa hii winga selfish Rashford na Antony Ten hag asipoangalia huyu Hojlund atahangaika kuzifumania nyavu.
hatumtegemei Rashford kututengenezea nafasi, msimu uliyopita Bruno aliongoza EPL kwa hilo
 
basi itakuwa humjui Robben au yule sio wa kizazi hiki?
 
Antony pamoja na kuwa hana hatari kiasi hicho ila ni msaada kwetu kwa ule upande Sancho au Rashford hawakabi wakicheza kule, pili beki timu hawezi kupanda kushambulia kama akiwepo Antony upande ule hiyo ni faida kwetu
 
hatumtegemei Rashford kututengenezea nafasi, msimu uliyopita Bruno aliongoza EPL kwa hilo
Kumbuka main man alikua Rashford sehemu ya kupiga pasi analazimisha kufunga nadhani wote tuliona namna
Weghorst alivyosua sua kufunga.

Tumepata striker Hojlund inabidi Rashford na Antony wapunguze uchoyo vinginevyo Hojlund tutamuona wa kawaida.
 
Antony pamoja na kuwa hana hatari kiasi hicho ila ni msaada kwetu kwa ule upande Sancho au Rashford hawakabi wakicheza kule, pili beki timu hawezi kupanda kushambulia kama akiwepo Antony upande ule hiyo ni faida kwetu
Kabisa mkuu dogo mimi huwa namtizama kwa jicho hilo mara nyingi akitoka uwanja unainama sababu mabeki wanakuwa huru sana refer ile mechi na Arsenal alivyotoka tu Zenchenko akaanza kupanda na kutoa assist.

Nilichogundu washabiki wengi wanatupia mchezaji mmoja mmoja lawama kwa kuwa timu huwa haishindi, ila timu ikaanza kucheza kitimu na kushinda huwezi kuona hizi lawama.

Man u tumekuwa na matatizo yetu ambaye yamechangia kuua viwango vya wachezaji, Sancho, Martial, Antony, Maguire, Van Debeek walikiwasha kule walipotoka kwa nini kwa man u wamefeli? Binafsi naona tatizo lilikuwa mfumo wa uchezaji na ulichangiwa na kipa. Tusubiri msimu ujao.
 
Wazee wa ngwasuma tunaludi Tena kwa Mara nyingine kugawa burudani majirani wote karibuni sana mpate burudani kabambe.

Manchester United inacheza na dunia nzima ina furaha


Dortmund 2 vs Manchester United 4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…