Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Najua watakupinga kina Flano na genge lake ,ila point yako ya kumtimua 10hag ni ya msingi Sana , huyo kocha toka amefika hajaendeleza kipaji chochote au aliowakuta , hata waliombeba last season ni wale wale wa toka enzi za ole na Mourinho ( Bruno ,degea na Rashford)

Sajili zake za kubahatisha Sana , Anthony,malacia , viwango duni, Casemiro haijulikan ata step up Tena au ndio maji ya jion sawa na eriksen ,

Anadai kina Sancho,Fred,mctominay,Maguire,n.k ni flop hakuna aliyemtoa point A to B,

Anasubiri miujiza Tena ya Rashford na Bruno ,anasahau Rashford ni Kama uyoga leo mboga kesho sumu , anasahau Degea hayupo Tena .


Alimfukuza Cr7 akamleta shemeji yake Weghost ambaye Hana goli hata moja

Kamleta malacia akiamini Luke Shaw ni flop mwisho wa siku malacia kawa Kama Yahya mbegu ,
 
Acha upumbavu kijana kama Maguire tafuta Kocha wako wa kumuendeleza hivyohivyo pia kwa Sancho.

Shaw,Rashford na Bissaka ilifika wakati walishachokwa kila mtu akitamani wauzwe ila wamekuwa stabilized ni mzee wako ndio kawabadilisha viwango?

Malacia sio mbaya shida yake ni kama Bissaka mzuri defensively tu ila kwa umri wake taratibu atabadilika kama ambavyo Bissaka anabadilika sasa.

Na kila mtu anaelewa namna alivyojaribu kumrudisha Sancho mchezoni kwa kumpeleka kwa wataalamu kuwekwa sawa ila Muingereza ni Muingereza tu hata wewe si huwaga unamponda why now unajifanya kama upo upande wake?Hypocrite mkubwa!

Weghorst asingekuja kama si Martial kuumia na kocha angepewa hata €80m kwa ajili ya striker na ubongo wako wenye kutu unadhani angemleta Weghorst?
Halafu Weghorst asiye na goli hata moja ndip alikuwa na impact kuliko hata huyo Mzee Mpili asipofunga anageuka mzigo

Yupo wapi saa hizi?

Fred na Scott hata kabla ya Ten Hag mashabiki washawachoka hawanaga improvement yoyote viwango vya homa za vipindi.
Hakuna mchezaji mwenye potential ambaye kocha anataka kumuuza.

Wachezaji wamefundishwa na makocha 3 huko nyuma ila hawabadiliki then tuje tumuangushie mzigo Ten Hag,hata Ralf alishasema ni uozo huo unahutaji replacement.

Kila shabiki wa maana kaona up and downs zilizotukumba majeraha na suspensions still timu akaisimamisha vyema halafu anatokea mpuuzi mmoja anabinua mdomo eti hafai.

Ndio madhara ya kufuatilia mpira livescore haya kila kitu ujuaji

Note:Hata ETH akileta Waholanzi/aliofanya nao kazi kikosi kizima tutamsapoti tu kikubwa walete impact uwanjani,tutamuwajibisha timu ikifanya vibaya,hakuna sehemu imeandikwa ni crime hata makocha wengi hufanya hivi ila kafanya yeye nongwa.

Kuhusu CR7 alishapitia files za Ralf pengine hata kaushari kidogo alikafanyia kazi.

Atoke Ten Hag aje Baba ako?
 
Grazzer wapo Sana

| There has been no communication between the sellers of #mufc and any potential buyers since Sheikh Jassim’s last bid for the club in early June.
Ndio vizuri waendelee kuwepo ili ndoto ya bwege flani isitimie hata robo.

Kama hela ya usajili watatoa hakuna shaka kikubwa kocha asiyemtaka ndio ana maamuzi ya mwisho nani asajiliwe.

Ole angekuwa na nguvu kama hii hadi leo tungekuwa nae maana aliingiliwa majukumu akaletewa killer button ya project yake

So wabaki tu hata Sir Jim ajikate tu
 
Mkuu Al-Hadidy punguza hasira kidogo, huyo Mc Hamisi Masingeli ni mtani wetu wa jadi twende nae taratibu tu.
Haina haja ya kutumia nguvu kubwa maana yeye mwenyewe ni fan mkubwa sana wa Ten Hag tokea kipindi yupo Uholanzi.
 
Mkuu Al-Hadidy punguza hasira kidogo, huyo Mc Hamisi Masingeli ni mtani wetu wa jadi twende nae taratibu tu.
Haina haja ya kutumia nguvu kubwa maana yeye mwenyewe ni fan mkubwa sana wa Ten Hag tokea kipindi yupo Uholanzi.
Angekuwa fan wa Liverpool au City nisingekasirika.

Tangu lini Gunners wakawa wajuaji mbele yetu ama kufuzu Champions League baada ya miaka 7 ndio kunawafanya wajione wana uwezo kama wa City
 
Angekuwa fan wa Liverpool au City nisingekasirika.

Tangu lini Gunners wakawa wajuaji mbele yetu ama kufuzu Champions League baada ya miaka 7 ndio kunawafanya wajione wana uwezo kama wa City
one season wonder tu hao.
Msimu ujao watakua kulekule kwa ndugu zao Leicester City.
Ila huyu Mc hamis77 ana kitu, angekua ni fan wa Man Utd angefika mbali.
 
UEFA KILICHOBAKI NI KUWASHUSHA DARAJA

Manchester United fined €300,000 by UEFA's Club Financial Control Body after being monitored for FFP breaches. UEFA said #mufc reported 'minor break-even deficits' covering the financial years 2019 to 2022 @TyMarshall_MEN
 
one season wonder tu hao.
Msimu ujao watakua kulekule kwa ndugu zao Leicester City.
Ila huyu Mc hamis77 ana kitu, angekua ni fan wa Man Utd angefika mbali.
One season wonder ni Kama manjesta mlikuwa mntembea na upepo wa Rashford Degea na Bruno ,

Arsenal ilikuwa ni timu nzima ndio maana tuna wachezaj pale karibu 5 kila mmoja ana goals 10+

Umeshajiuliza Nini kitatokea iwapo Rashford akarudi kwenye default settings?

Vipi ushajiuliza ile mi sevu ya Degea je onana atahimili?

Vipi Bruno ambaye huwa anakata tamaa mapema


Ukijiuliza maswali hayo Basi akili itakujia hata top 6 itakuwa ngumu kutoboa
 
Hamis kinye...na arsenyeto yako ni kama azam fc tu ya hapa bongo..tunaku-zoom tuu na taarab zako hapa kweny uzi wa mabingwa.
 
Kwema ndugu.....na username yako hiyo...namkumbuka jamaa angu mmoja nae ni fan galagala wa arsenyeto kama wewe..alikua anaitwa hamis bomela mtambo wa gongo kama wewe. Hua mnaongea sana
Arsenal fans na man u fans sifa zao wanaongea Sana
 
Kwema lakini ndugu?

Mm sipigi taarabu ,nyie watan lakin Kuna muda inabidi tuambiane ukweli
Mkuu hivi inawezekana team ukawa huipendi lakin kutwa 24hrs unaiongelea?

Binafsi naona haiwezekani wewe utakuwa unaipenda Man U.

Kule Arse8 kwenu huwa nakuja mkifungwa tu napotea hata miezi miwili ndio narudi.

Litimu lenu halivutii mashabiki ni kama city tu kachukua treble lakin hamna anaewafuatilia kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…