Ni afadhali Manchester United itolewe mapema tukibahatika kuvuka raund hii tukakumbana na Bayern au Real watatufanyia mauaji ya kutisha.Manchester ilistahili kufungwa kwasababu zifuatazo.
1. Timu imekosa vipaji binafsi,hakuna mchezaji anayeweza kuibeba timu inapozidiwa ni kisema kipaji binafsi namzungumzia mchezaji kama Ronaldo,Messi......Aina ya wachezaji hii inakosekana katika kikosi cha Man.Mchezaji kama Robin body language inaonyesha ameathirika kisaikologia.Timu imekosa malengo,timu haina speed pass.
2. Mfumo wa kulazimisha kupanga washambuliaji wawili Robin na Rooney katika mechi moja umesababisha Man kuwa predictable.Mfumo wa 4 4 2 umeshindwa kufanyakazi hata katika mechi nyingi za EPL sioni sababu zinazomfanya Moyes kulazimisha mfumo huu kwaajili ya kuwafurahisha Robin na Rooney.Timu nyingi zinacheza na mshambuliaji mmoja Man washambuliaji wawili kunasababisha kupwaya kiungo hasa sehemu ya kati kati.
3. Mimi ni mpenzi wa Man lakini sijawahi kumwamini T Cleverly hata siku moja nilipomwona kati list ya wachezaji watakao anza nikajua tumeumia.Ukweli ni kwmba Tom ni mchezaji wa kiwango cha chini sana hastahili hata kukalia bechi la Man ningekuwa na mamlaka angekuwa mchezaji wa kwanza kuuzwa hawazi kupigachenga,hawezi kukaba vizuri,hawezi kufunga......Ni mchezaji ambaye kamwe asingeweza kucheza kama angekuwa Chelsea,Arsenal au Man City lakini Man United anapangwa katika mechi kubwa siajabu hata kidogo tunashikilia nafasi ya sita.
4. Moyes anachelewa kufanya substute mfano mechi ya jana Cleverly alichemka mwanzo mwisho badala ya kumbadili dk za mwanzo aliachwa mpaka timu inafungwa magoli mawili ndio anastuka.Valencia alikuwa mchezaji mzuri sana lakini baada ya kuumia vibaya mpaka leo ameshindwa kurudisha kiwango chake cha zamani cross zake nyingi zinazuiwa mapema kabla hazijatua kwenye box kuna siku nilikuwa naangalia mechi ya Man Valencia alipiga cross 8 kati ya hizo cross 6 hazikufuka kwenye box zilizuiliwa mwanzoni kabla ya kuleta madhara.