Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hiyo €120m ni intial nimeweka maelezo juu kwamba wakiuza wachezaji kadhaa inaweza kuongezeka hadi hata €300m.
Hapo wanaweza kupata wachezaji hata 5/6.

Tatizo kikwazo ni takeover maana ingekuwa Mwarabu akiinunua timu anaanza kazi haraka labda tungeweza kufanya sajili zote hata July kwa hela yake.

But sasa cha kushtua ni kwamba inatakiwa approval toka kwa Premier League ambayo inaweza kuchukua wiki 8-12 na kwa mahesabu ya haraka ligi inakuwa ishaanza na hata dirisha la usajili linakuwa limefungwa.

Nadhani tuanze kupigia maesabu hela ya mmiliki mpya kuanzia January mwakani.
 
Aaah sawa
 
Kaka tuanze kwanza na mapungufu ya mchezaji mmoja mmoja de gea ni mbovu sana huna cha kumtetea juu ya performance yake tena hata izo unazosema anaokoa mara nyingi unakuta makosa ni yake...kuna namna ww unaangalia mpira kwa angle isiyo sawa
 
Ishatoka hiyo njia pekee ya kumpata ni kumsajili kwa dau zaidi ya walilooffer Bayern na mshahara zaidi tena hijacking ihusike kama tulivyofanyaga kwa Martinez na Malacia
Usajili wa Min-Jae ni atakayeweza tu kumshawishi mchezaji maana ana release clause itakuwa activated July.

Sasa kama Bayern watampa mshahara sawa na sisi sioni akiacha ofa nzuri zaidi kutoka timu ambayo ina project ya kueleweka na inapambania makombe.
 
Habar za leo ndugu zangu, leo naomba nichangie kidogo kwenye hili jukwaa baada ya kimya kirefu.

Kitu cha kwanza ambacho inabidi tukubali ni kwamba kwa sasa tupo nyuma sana na washindani wetu wakubwa kwenye Ligi achia mbali UEFA, na ni ngumu kupata timu ya kugombea ubingwa kwa msimu ujao( kama tutaendeleaa kuwa chini ya Glazer). Kama Muarabu atachukua timu safari yetu itakuwa fupi,

Maelzo yangu ni assumption kama timu haitaenda kwa mwarabu kabla diriaha halijafungwa

Kwa dirisha hili la usajili kwangu naona litakuwa limekwenda vizuri endapo tutakuwa tumepunguza wachezaji mizigo( wasio na msaada) kuliko hata kusajili wachezaji wapya wengi.


Wachezaji kama Wanbissaka(Sababu Dalot katoka kupewa mkataba) ,Maguire,Mctominay,Martial,Elanga,Brandon Williams,Van de beek unaweza ukawauza kwa pesa za nyanya ukakusanya ukapata mchezaji mmoja au wawili wanaoweza kuwa na impact kubwa kuliko kundi kubwa la wachezaji wasio na faida.

Kwangu ni bora kubaki na Maino na Zidan kuliko kumtegema Mctominay auu Fred.

Kwa mtazamo wangu natamani tungepata kipa zaidi ya Degea, ila kwa bajeti hii ya maandazi sioni hili likitokea. Kwa hiyo Dean angerudi ili agombanie namba na De gea,(uzuri wa Ten Hag) ana uwezo wa kumuweka benchi mchezaji yoyoye ambaye ana under perfom. Ila ili uweze kumuweka benchi ni lazima unaye mpa nafasi awe bora kuliko unaye muweka benchi. ( hii ingeleta chamgamoto chanya kwenye nafasi ya golkipa) tungeweza kusogea kidogo.

Halafu hela zote zile zitazopatikana kwa kuuza wachezaji wa mafungu zingeelekezwa kwenye nafasi ya Ushambuliaji (Tungepata Striker mmoj wa maana) na mchezaji kiraka mmoja mfano wa Caicedo. Ukipata mchezaji kama huyu unakuwa ni kama una wachezaji wawili au watatu. Anaweza kucheza kwa ufasaha zaidi ya nafasi mbili.



Binafsi naona Ten Hag amefanya kazi nzuri kwa msimu wake wa kwanza ila kama hatapewa support ya dhati tutarud pale pale kwamba kocha hafai.
 
Mchukue ilkay gundogan then mpatie mkataba wa miaka miwili.

Fuatilia ukuaji wa kobbie mainoo na zidane Iqbal ndani ya hiyo miaka miwili.

We need controller eneo la midfield, hao akina kim min jae wala hawaniumizi kichwa sana ukilinganisha na eneo la midfield
 
Msenge kama huyu aliyecheza mechi chache kuliko werghost ndio akupe ubingwa,

Kwa kazi gani aliofanya hadi awe na mapumziko ya ulaji bata kama haya
View attachment 2660044
Wa kuuza huyu,kwanza sura yake akiwa uwanjani ni kama kalazimishwa kucheza.

9 gani hajui hata kupiga mipira ya vichwa na goigoi si kitoto.
 
Msenge kama huyu aliyecheza mechi chache kuliko werghost ndio akupe ubingwa,

Kwa kazi gani aliofanya hadi awe na mapumziko ya ulaji bata kama haya
View attachment 2660044
Soka la sasa hivi ubishoo na uvivu ndiyo vinaongoza. Martial, Sancho, Rashford huwa naona kama ni watu wanaojaza nafasi tu United. Siyo watu wa kutegemea kabisa.

Martial unaweza kumtetea kwa injuries lakini haonyeshi hali ya kujituma uwanjani ni kama hajali.

Sancho ubisho na bata vinamaliza kipaji chake. Msimu umeisha tayari kawahi Jet na kupiga soft drinks. Naweza kusema pesa nyingi ktk umri mdogo ndiyo sababu.

Rashford ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu lakini ni kama ame-stuck mahali. Ujana na kutojituma 100% ndiyo tatizo lake. Rashford ni mchezaji ambaye pesa na umaarufu havijaichota akili yake ila naona kama kwenye 100% uwanjani anafanya 70% akiamua kufanya kazi yake ipasavyo ni mchezaji mzuri.

Mfano mzuri ni pale Man City, Haaland na Alvarez ni watu wa kazi lakini mtu kama Foden ana mambo mengi na ndiyo tabia ya Waingereza wote. Hata Rooney alikuwa mlevi ila hakuwa na utani uwanjani.
 
Kwa ufinyu wa bajeti tulionao inatakiwa kuwa na plan B endapo Glazers hawaachia timu mapema. Wengi wetu tulishawishika na project ya mwisho ya 10Hag pale Ajax akiwa na makinda wengi kwenye timu yake na ilikuwa inacheza mpira mzuri sana.
Ni wakati sasa akatafute vipaji visivyo na majina uko S/A,Asia,Afrika na hata ligi za ulaya mashariki zisizo na majina lakini kuna talents nyingi. Pesa tuliyo na uhakika nayo tununue proven striker na tuuze magalasa yetu tumtafute De Jong ashikilie dimba na Casemiro.
Mapengo mengine uwanjani tuzibe na hizo talents toka kusikojulikana ili tuwashangaze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…