Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kwa soka la sasa ni lazima,De Gea nyakati zile za SAF ndio aina ya kipa waliokuwa wanahesabika bora sio miaka hii ya build up za kuanzia nyuma.
Upo sahihi ,niliangalia mechi ya FA manjesta vs Mancity niliona Kuna buildup mlizifanya nyingi tu na zilifanikiwa , Sasa pale mtoe muweke Onana ,means Kama kwa timu Kama city buildup zilifanikiwa ,Basi kwa middle teams una uhakika wa kushinda mechi nyingi na goals nyingi

Kuna watu hawajui umuhimu wa buildup kwa soka la kisasa ,ndio maana ukiwaambia Degea hafai hawakuelewi ,

Unapofanya buildup ukatoka chini salama kwa usahihi ,shepu ya timu pinzani unaikuta imepangaranyika sababu walikuja ku press wakashindwa kufanya turnover

Wasipo press ,Basi wanakuwa wamerudi nyuma kuzuia ,means mpira mtakuwa nao muda mrefu mkiwasaka

Hii inaongeza Percentage kubwa ya kushinda mechi ,

Ndio maana kocha Kama Conte,Mourinho, Simeone ,hawawez kutoboa EPL kwasasa ...even hata Ancelot .

Ferguson mwenyewe kwasasa angekiona Cha Moto,

Treble ya 1999 , Alibeba EPL na points 79 tu , wakati leo Liverpool points 97 anakosa EPL, Arsenal points 84 tunaonekana hatujafanya kitu .
 
Watu wanaomtetea De Gea wakaangalie mechi 2 tu za msimu huu: Barcelona - Old Trafford & Sevilla - Pizjuán Stadium.

De Gea ni shot stopper mzuri lakini yeye ndiyo sehemu ya magoli mengi tunayofungwa. De Gea shots nyingi anazozuia huwa ni matatizo anayojitengenezea yeye mwenyewe.

De Gea akiwa golini anazubaa sana hata zikipigwa cross huwa hafuati.

Wapinzani wameshajua udhaifu wa De Gea wanachofanya ni ku-press tu kitu kinachomfanya De Gea kubutua mpira na timu kupoteza possession kizembe.
 
Ni mechi nyingi sana msimu huu tumetoka uwanjani "kwa asante De Gea" , team imeoza kuanzia mabeki, viungo, huko mbele ndio viazi kabisa.


Hizo game zote ulizotolea mfano tulifeli kwasababu ya hesabu za kocha katika sub, wala haikuwa kawasababu De Gea alikuwa anapoteza possession.

Mechi kama ile tuliyopigwa goli 4 na BENTIFORD utasema ni kipa? Ila ya Liverpool tuliyokula goli 7 utasema ni kipa? Zile goli 6 za City utasema ni kipa? Ile game tuliyosuluhu na Crystal palace licha ya kuongoza goli moja tulipigwa msako mkali sana tukapona kwasaabu ya De Gea.

Mechi zetu dhidi ya Spurs, Sevilla, Barca, ARSENAL (ile ya 3-2) na nyingine nyingi, ni mechi tulizopoteza kipumbavu licha ya kutangulia kwasababu ya ujinga wa Ten Hag kwenye sub zake. Ni mara chache sana Ten Hag apige hesabu za kufanya sub kisha zifanikiwe.

Kwa mfano wa mechi ulizotoa bado sio sawa kumtupia lawama De Dea.

ITAFUTWE SABABU NYINGINE GENUINE, SIO KUSEMA DE DEA NI KIPA MBOVU.
 
No No No ile game na Sevilla tuliyopigwa 3 si mapema kabisa alichomesha yeye goli la kwanza,sub ilihusika vipi hapo?Hata la 3 ilikuwa ni uzembe wake anatoka hadi pale halafu anashindwa hata kupiga mpira kimahesabu hapo utamlaumu vp kocha.

Game ya Brentford ilikuwa hivyo pia alichoma goli kwa pasi zake kama miguu imepinda

Game ili tunapigwa na West Ham nayo alichoma ila bahati mabeki wakawahi fasta.

Hizo game tulizopigwa nyingi ilikuwa ni full team mistakes ila yeye kama yeye ana individual mistakes nenda kaangaie makipa wenye errors leading goals utaona yeye na Pickford wanaongoza ila ni mabingwa wa kufanya saves

Na hizi saves ndio zinatufanyia brainwash ila wote hao hakuna wa kupata namba kwenye timu za top 6 hata benchi tu.
 
Hakuna anayesema De Gea ni mbovu ila kama walivyo wachezaji wengine ana mapungufu yake na hayo mapungufu ni udhaifu kwenye mfumo wa Ten Hag.

Halafu mechi ya Brentford uliyotolea mfano ndiyo De Gea alifanya uzembe wa hali ya juu. Bora ya 7-0 au 6-3 ni timu nzima ilizingua.

Nimetolea mfano mechi ya Barca kwasababu kuna kosa moja alifanya ambalo litakupa picha kwanini hafai kwenye mfumo wa EtH: De Gea alikuwa na space ya kutosha golini kwake, mabeki wakiwa wametanua pembeni na alishindwa kutoa pasi badala yake akampasia mpinzani.

Mechi ya Sevilla mapema tu akachomesha (Maguire naye alihusika) dk za mwisho akajaribu kutoka ili kuokoa akaukosa mpira tukafungwa goli la 3. Haya ni makosa ambayo yanaigharimu timu na kipa kama De Gea ni wazi ameshindwa kuyarekebisha.

Kwenye ulimwengu wa soka ambao unapata kipa anayezuia na aliyetulia mguuni ni kwanini tumng'ang'anie De Gea? Mimi nitaelewa tu DDG kuwa backup GK na siyo #1 msimu ujao.
 
Angalia hii 👇

Mechi ya Real Betis alifanya kosa hilihili na yote alitoka salama. Mechi zote za msimu huu distribution yake imeigharimu timu kupoteza possession. Mpira umebadilika, DDG ni kipa wa zamani. Kudaka siyo tatizo ila uchezaji wake una-influence aina yetu ya uchezaji kwa % kubwa sana.
 
Huyo huwa anachoma sana ni vile akina Martinez huwa wanafuta mistakes zake na hiyo kitu akaendeleza akiwa na akina Maguire ambao hawana ubora.

Makosa hayo tayari ni udhaifu na hauvumiliki,naomba tu July ifike haraka tuone mustakabali
 
De Gea huwa anasifiwa akidaka ila mara nyingi yeye ndiyo huwa chanzo cha tatizo.

Unakuta anabutua mpira mbele mpinzani ana-win mpira timu inashambuliwa linapigwa shuti anadaka (watu wanaanza kumsifia) ila ukirudi sekunde 30 nyuma unakuta yeye mwenyewe ndiyo alianzisha tatizo kwa kushindwa kupiga pasi au kupeleka mpira mahali sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…