"Kilichobaki ni kula maandazi tu."
We're not serious as a club. Kuanzia wamiliki, kocha na wachezaji.
Tumewapa City treble. Mechi ya FA Cup wachezaji wetu walichoweza ni kuongea tu vitendo sifuri. Walijisifu kuwa tutazuia City kushinda treble (Rashford) lakini hakuna wanachojali kuhusu hii timu. Garnacho pekee ndiyo alionyesha kujali na kuipambania jezi ya United.
Baada ya fainali ya FA Cup, De Gea alipaswa kuonyeshwa mlango wa kutokea ila bado kocha anaruhusu aongezwe mkataba.
Mchezaji kama Sancho ana mfululizo wa misimu mibovu ila jana kaonekana tayari anawahi vacation.
Hatuwezi kuwafikia City bila kuwa na wamiliki walio na mpango kazi na wapo tayari kuwekeza kwenye mawazo ya kocha na kuwa na watu wenye viwango na ushindani ktk nyadhifa mbalimbali ndani ya club.
Hatuwezi kuwafikia City tukiwa bado tunawategemea wachezaji kama De Gea, Martial, Maguire, Fred, McTominay, Elanga, Sancho.
Hatuwezi kuwafikia City tukiwa na kocha asiyefanya maamuzi magumu. Kumpa mkataba De Gea ni kosa la kwanza. Tutalipa mishahara mikubwa kwa watu kukaa bench na hawana uwezo.
United ni lazima ikubali kumalizana na wachezaji hasa legends, huwa ni ngumu sana sisi kuwatimua wachezaji. Madrid wamemuachia Benzema ingekuwa ni sisi angebaki tutafute backup yake. Siyo kazi ngumu kujua kuwa De Gea muda wake ktk top level football unamalizikia.