Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kama €250m ya uhakika ipo tuachane na Kane.

ST: Rashford / Hojlund
RW: Antony / Amad / Pellistri
LW: Sancho / Garnacho
View attachment 2646385
Context:

Mount anakuja kucheza kama right sided no 8.

Timber siyo overlapping RB so tutamhitaji Mount ku-link na Antony. Pressing yao itakuwa ya hatari sana.

Kwenye build up tutaweza kucheza na back 5 (3-2) ya Martinez, Min-Jae na Timber wakitengeneza 3 at the back kwasababu Timber ni mzuri kuanzisha mashambulizi kutokea nyuma. Shaw inverted kuwa pivot pamoja na Casemiro.

Pia tunaweza kucheza na 2 CBs mbele yao kukiwa na 2 mids. Tukiwatumia FBs Shaw na Dalot (overlapping RB)

Costa kama ball playing GK.

Hojlund kama backup striker, hapo tutapata a balanced team bila hivyo £100m kwa Kane timu itakuwa na matobo mengi.
 
Hatuwezi kusajili beki wa kati wawili labda mmoja tu
 
Kibibi kizee cha turin juventus lazima apite na mmoja hapa
 
Ww unaliona hilo likitokea? Progress yetu haiendii kwa haraka kiasi hiko...
Naliona likitokea maana usajili wa Mount una tija zaidi tukimpata Timber.

Baada ya kumkosa De Jong, Timber ni ball carrier mzuri wakati Mount akiwa RCM anafanya underlapping runs & Antony akiwa juu kulia kutengeneza space.
 
Naliona likitokea maana usajili wa Mount una tija zaidi tukimpata Timber.

Baada ya kumkosa De Jong, Timber ni ball carrier mzuri wakati Mount akiwa RCM anafanya underlapping runs & Antony akiwa juu kulia kutengeneza space.
Mmh hatuwezi kusajili beki wa kati wawili na wakati huo huo tunasajili kipa nafikir wataangalia sehem muhimu zaid...alafu saiv Manchester imebadilika sana kulinganisha na misimu ya nyuma kwenye soko la usajili hatuna tetesi nyingi kama ilivyokuwa awalii..hizi tetes za mount huenda ni za kuongeza thaman ya mchezaji lakn sizani kama ni za uhakika maana ndio Kinachofanyika sana mchezaji anahusishwa na Manchester kumbe ni kwania ya kuongeza thaman yake sokoni
 
Tetesi za Mount ni za kweli, anahitajika na EtH. Tunahitaji sana no 8. Tukicheza na double 8s Harry Kane ni striker atakayetufaa sana kwa uwezo wake wa ku-drop deep na kuwa kama no 10 tatizo ni budget bado Madrid nao msimu huu wataingia sokoni kutafuta striker wanaweza kutuharibia mipango yetu.

Kitu kinachonipa matumaini ni jinsi EtH anavyosahili wachezaji watakao-fit kwenye system yake na siyo kama zamani United ilikuwa ni kuokota tu watu.
 
Graza kinachowaponza wametoa Uhuru mkubwa watu washike nyadhifa ambazo Ni muhimu Sana ,

Nikweli wanabeba pesa mingi Sana, lakini bado kile kidogo wanachokitumia kwa usajili Ni kikubwa ,hamjawahi kuwa na tatizo la kusajli wachezaji wa €80-100m

Kama Ni hivo tatizo lipo kwa uongozi, Graza hawajui mpira inajulikana , walipotoa mianya waletwe watu wa mpira bado hawakuletwa watu wampira

Leo timu akichukua muarabu bado mtasajili wachezaji wa Bei zile zile ambazo alikuwepo Graza ,

Siku mtakapoleta watu Kama kina Van der sar , Luis ocampos ,na watu wanaofanana mitazamo Kama hai, Katika uongozi wenu , hamtaona ubaya wa Grazzer.

Hivi unajua pale city wachezaji wao ukimtoa jack Ni wa Bei €30-60m tu ,
 
Madrid naona wameweka nguvu kwa Kane ,wamebakiwa na Rodrigo na Vini Jr tu kwenye attacking yao

Na Kane Sion akiuzwa chini ya €150m kwa timu za EPL

Hapo una Disturbe bajeti yote

Diogo Costa ana release clause ya €75m

Kim ana release clause nadhan kwenye €50m

Hapo Chelsea Wanataka €70-80m kwa mount
 
Halafu timu zinajua United ni sehemu ya kuchota pesa. Mpaka sasa haieleweki pesa ya usajili ni kiasi gani.
 
Glazers msimu huu ndiyo wanatupoteza kabisa maana kama kuuza timu kwa muda uliobaki ni mchache sana.

Sasa hivi ilitakiwa EtH awe ashajua budget yake na kuanza kumalizana na wachezaji mapema.

Liverpool tayari wameshamalizana na Mac Allister, msimu ujao ushindani utakuwa ni mkubwa sana.
 
Kikosi hiki unaweza kuchukua ubingwa wa epl na kuleta ushindani UEFA? sidhani kama itawezekana kwa Man u, unless wanataka kuwa wasindikizaji.
Tatizo ni pesa. Hiki kikosi siyo chini €350m. Kama mashabiki kuna muda inabidi tuwe realistic, United kubeba ubingwa wa EPL msimu ujao ni ngumu sana.

Kile kikosi cha mwanzo kinafaa sana maana kipo balanced ila kama pesa ipo hiki ni cha ubingwa kabisa.
 
Manjesta shida Ni management ,Chelsea Wanataka wawauzie mount kwa €80m halafu wao hiyo hiyo hela wakamchukue Caicedo kwa £75-80m (€80-85m)

Wakati huo huo manjesta unaona kabisa wanamuhitaji mtu Kama Caicedo ,

Umri mdogo, anacheza #8 ,#6 anacheza inverted RB , Ni press resistant

Kitu kingine Caicedo anatoa priority kwa timu inayocheza UCL ,


Kituko Sasa Manjesta wanakomaa na mount ambaye kwa misimu miwili amekuwa na kiwango duni
 
Liverpool Wana bajeti finyu Sana lakini kwa usmat wao wamempata MacAllister kwa less than £60m .

Timu itakayompata Caicedo itasumbua Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…