Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mkuu mimi nina mtazamo tofauti kidogo.

Naamini tumepiga hatua ingawa si nyingi kama tulivyotarajia.

Mzunguko wa pili tulikuwa tunaongelea habari ya ubingwa.Mambo yalianza kwenda ndivyo sivyo baada ya red card ya Casemiro na kuumia kwa Lisandro,Varane & Martial.

Tuna hitaji wachezaji 4 au 5 tu ili tuweze kukimbizana na City.Mlinzi wa kati,Kiungo na mshambuliaji wa kati.Tunaweza kuongeza mlinzi upande wa kulia na mshambuliaji kulia.

Team kwa mara ya kwanza imejitahidi ingawa bado kidogo.Tuna hitaji kuondoa magarasha yote na nafasi zao kuzibwa na wachezaji sahihi.

Tumpatie Mwl muda na zaidi ya yote tushukuru Mungu top four ipo ndani ya uwezo wetu.
 
Nimeangalia timu yangu leo nikawaza ni timu hii itaemda kukutana na City kwenye fainali ya FA au kuna nyingine?
 
Hata Hatuna best 11, tukishaipata hio ndio tuanze depth kama ya City.
 
kila timu na falsafa yake Liverpool amechukua ligi kwa style yake mbna...
 
Hii timu kama atapewa mwarabu naamini msimu ujao utakua ni wamafanikio makubwa, ila kama timu itaendelea kubaki kwa Wamarekani Mambo yatabaki kua vilevile tu.
 
Majeruhi alikua Ericksen tu,wengine ilikua sio kiivo,labda zile card za Casemiro
Yes card ya Case ikachangia mno, majeruhi ya Ericksen, Varane, Rashford na Matinez na Garnacho ndio yaliyimuharibia kocha plan.Ujio wa Martial ukamfanya Werghost kuanzia bench hapo ndio ikiwa balaa zaidi.
 
Tetesi za kusajili fullback wa kulia ni kama vile zimekufa,

Je tutaendelea na huduma ya dalot na wan bissaka?

Dalot anaelekea kupewa mkataba mpya,
Sijafurahishwa na huu uamuzi wa diogo kutengezewa mazingira ya kupewa mkataba.
 
Sijui mnatoleaga wapi huu uchambuzi wa ajabu ajabu, yaani badala ya kumpongeza kocha kufikia hii hatua na wachezaji wavivu wavivu kama Martial, Sancho na Rashford wewe unaanza kutabiri vitu vya ajabu. Nionavyo mimi ETH ni bonge la kocha na msimu ujao utajionea, kwa majeruhi aliyopata ya wachezaji wake muhimu plus card za Casemilo ingekuwa ni enzi ya Ole tingekuwa nafasi ya 10. Pamoja na timu kuwa mbovu namuona ETH kafanikiwa zaidi kuliko Arteta hivyo tumuheshimu japo kidogo tuwe watu wa shukrani.
 
Nawakumbusha tuna rekodi nzuri ya kununua averages player kwa bei ghali kuliko kuuza wachezaji wetu hata kwa bei nafuu.

Wale munaoamini tuna uwezo wa kusafisha banda endeleeni kujipa matumaini.

Nawaona telles, bailly, martial, fred, maguire na mctominay tukiwa nao mwezi August 2023.
 
Hatuna wachezaji tu.

Kucheza mpira kama wa city ni uongo, tunahitaji wachezaji wanaotafuta ushindi kwa udi na uvumba. Hao wachezaji hatuna hasa strikers na midfield hata kipa.

Arsenal sio mara yao ya kwanza kucheza mpira waoacheza.
 
Upo sahihi.

Tungekuwa na majembe kwenye zile key areas sahivi tungekuwa kwingine kabisa.
 
Hii timu kama atapewa mwarabu naamini msimu ujao utakua ni wamafanikio makubwa, ila kama timu itaendelea kubaki kwa Wamarekani Mambo yatabaki kua vilevile tu. View attachment 2629103
Mipango ya usajili inatakiwa iwe imeshaanza sahivi. Na tushaanza kusaini.

Ila mpaka sasa hatujui kama hao Glazers watauza au la.

Mchakato ni mrefu kidogo hata kama Glazers wakisema wanauza leo. Ambapo mafanikio ya kweli tuyafikirie baada ya msimu ujao.

Sio msimu ujao.

Tuanze kuwaza kuuza wachezaji wa kawaida kwanza. Tukimaliza kusafisha tuwaze makubwa zaidi.
 
Me too mkuu.
Kule tunaenda kujikatisha tamaa tu. Ni heri tungeweka mipango ya makombe ya ndani kwanza kabla hatujawa vizuri kugombea UCL.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…