Grazzer dirisha lililopita si walitoa hela ya usajili €245m Kama sikosei
Mnataka watoe kiasi gani mseme kweli wametoa pesa? Kumbuka Kuna FFP, wage bills , operation cost
1. Wameipa club deni. Kipindi wanainunua United ilikuwa haina deni.
2. Hawajaboresha miumdombinu ya timu tangu wameinunua United.
3. Hawajaboresha uwanja (Old Trafford) na kuweka huduma za kisasa kuendana na kasi ya Teknolojia, ikiwemo upatikanaji wa Internet (Wi-Fi) kwenye uwanja mzima.
4. United ndiyo timu pekee kwenye EPL inayotoa gawio. Katika miaka 7 ni £155m zimetolewa kwenye gawio.
5. United inaendeshwa kwa misingi ya kibiashara zaidi hivyo watu chini ya Glazers hawana nguvu ya maamuzi zaidi ya Glazers wenyewe.
6. United inajiendesha yenyewe, hiyo €245m unayoisemea ilitokana na mapato ya timu. Na Glazers hawajawahi kufanya uwekezaji wowote ktk timu.
7. Tokea 2006 United imetumia £1.1B (kwa report za 2021) kwenye financing.
£724m interest
£185m debt repayments
£149m dividends
Hiyo ni £1.1B ambayo ingeweza kuboresha United ktk miaka yote hiyo. Kwenye miundombinu, wachezaji, makocha, wafanyakazi wazuri na wabobezi ktk soka ila kwasababu ya Glazers pesa yote wameikomba.