Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kane ni bora zaidi ya osimhen
 
Casemiro akija arsenal si anapewa number ya Xhaka kiulaini tu akabie juu kama alivyofanya Madrid?
 
Mimi nilipoona sajili zile za kina Anthony, malacia nikajua huyu ni wale wale tu
Mashabiki wa arsenal mumejaaliwa utakatifu unaoambatana na majivuni yaliokithiri,

Miaka yangu 21 ya kushabikia mpira wa ulaya nimejifunza jambo hilo, mwanzoni nilidhani hiyo hulka ipo kwa mashabiki wa arsenal waliopo zanzibar tu kumbe ni Tanzania nzima.
 
Casemiro akija arsenal si anapewa number ya Xhaka kiulaini tu akabie juu kama alivyofanya Madrid?
Anacheza bila tabu, kwa timu iliyopo sasa arsenal atakuwa bora maradufu kuliko hapo united.. achilia mbali kadi nyekundu hizo za njano tu itakuwa nadra..
Timu kila muda mpira mnao nyinyi,timu nzima inakaba,kadi ataipatia wapi.. xhaka mwenyewe siku hizi mikadi imepungua.
 
Angekuwa Arsenal huyu jamaa ungekuta tushachukua ubingwa hata na hii Baki ya mechi 11 😆😆
.
 
Hamtaki kabisa tuongee uhalisia ,Basi tutaanza kuwapamba

Hivi ni uongo kwa Anthony mchezaji wa €100m kwa kiwango anachoonyesha ? Yule si mchezaji wa €25m ,hivi yule Anthony anamzidi Nini mfano Pellistri?

Kwakuwa hamtaki kukosolewa Basi mnataka tumpambe Anthony


Mchezaji wa €100m ,Epl ana Goli 3 assist 0
 
Hamtaki kabisa tuongee uhalisia ,Basi tutaanza kuwapamba
Umeninukuu vibaya, nimezungumzia tabia zenu zenye ufanano.

Kuhusu Thamani ya anthony imeshajadiliwa tokea mwezi wa 8 humu ndani, unachofanya wewe ni kelele za kasuku
 
Mimi nilipoona sajili zile za kina Anthony, malacia nikajua huyu ni wale wale tu
Usajili wa malacia una tofauti gani na sajili hizi

Tomiyasu - paundi millioni 15 hadi 19.
Tavares - paundi millioni 7.

Una uwezo zaidi ya huo brother, mambo hayo waachie jamii ya ollachuga

Jikubali.
jiwekee standard ya ushabiki
 
Kun Antony , sancho pamoj na kaka yao Bruno kun wanakuwa wangese Saan uwanjan
Waingereza wametupiga tena bakora ya chuma kwa usajili wa jadon sancho.
Potential ipo lakini dah!

Anthony tumeadhibiwa kwa ujinga wa mabosi wetu, tumekwenda kuwavamia Ajax muda ambao wameshapoteza wachezaji wao muhimu watano huku tukifahamu fika sisi ni kichwa cha mwendawazimu kwenye ishu za usajili.

Timing, timing
 
Baadhi ya nyakati inaniwia vigumu kuzielewa injury za wachezaji wa ulaya.
Mzungu akipata muscles harudi tena uwanjani,

huku kwetu uwanja wa mao ze dong unakuta mchezaji kagongwa kwenye ankle anapumzika wiki moja then anarudi uwanjani kwa msaada wa barafu.

sijui ni matunzo mabovu ya wachezaji wetu au ubovu wa miili ya wazungu.
hata sielewi
 
Usajili wa malacia una tofauti gani na sajili hizi

Tomiyasu - paundi millioni 15 hadi 19.
Tavares - paundi millioni 7.

Una uwezo zaidi ya huo brother, mambo hayo waachie jamii ya ollachuga

Jikubali.
jiwekee standard ya ushabiki
Tomiyasu ambaye Arsenal anacheza wiki kila wiki LB, RB , unamfananisha na malacia? Ambaye alisajiliwa kuja kumtoa Luke Shaw tuliyeambiwa ameisha

Nuno tavares ni usajili ambao ulifeli ni wa Bei Chee £7m sidhani Kama unaweza kulaumu mchezaji backup wa £7m kufeli? Now ligue 1 ni winger ana Goli za kutosha
 
Mashabiki lawama huwa siyo wazuri mnakuwa hamna tofauti na wakina Schols, yaani timu ikishinda kocha mzuri ikipoteza point mnatafuta mchawi. Timu yetu bado inamapungufu hasa idara ya ushambuliaji na kiungo na tangu haumie Eriksen kocha amejitahidi kuziba pengo lake lakini kadri siku zinavyoenda aliowapa jukumu hilo wanazidi kudrop.

Straker sisi hatuna Rashford sio natural straiker, Sancho kiwango kibovu, Antony bado hajacheza kwenye kiwango chake Weghorst hakuwa kwenye mpango wa timu yetu alikuja kama dhali tu kuziba pengo la Ronaldo. Hivyo top four msimu huu itatutosha tukichukua na vikombe hata viwili. Ila msimu ujao baada ya usajili naamini huyu kocha mtamtaka radhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…