Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Yule "mbwiga" anasema hapa kila siku hajui Fred anafanya nini uwanjani sijui atakuwa wapi saa hii. Kwa taarifa yake tu ni kwamba katika wachezaji watatu bora wa Man U Fred ni mmojawapo.
 

Ukiwa na mawinga kama hao haimaanishi beki usipande. Narudia tena mpira umebadilika sana is why sikuizi hata beki wa kati ukamkuta mbele anashambilia mipira ya kona sometimes.
 
Sasa Mbona Trent, White, Cancelo, na Hakimi huwa wanapanda.
Mpira wa sasa unategemea FB kupanda.

Ili ku Overlap au Underlap.
 
Yule "mbwiga" anasema hapa kila siku hajui Fred anafanya nini uwanjani sijui atakuwa wapi saa hii. Kwa taarifa yake tu ni kwamba katika wachezaji watatu bora wa Man U Fred ni mmojawapo.View attachment 2533713
Martinez, Casemiro, Bruno na Rashford. Sawa ngoja niishie hapa maana hata eriksen ni majeruhi. Au umemaanisha wachezaji watatu bora wa Man U upande wa kiuongo?.

Ninavyo waelewa wanao msema Fred ni kuhusu kukosa muendelezo wakufanya vizuri mechi na mechi, wewe umeshindwa kuwaelewa unaleta mahaba niue
 
Nakubaliana na wewe ila msimu huu mechi ya Barca Camp Nou na nyingine baadhi za mashindano mengine AWB amekuwa akienda sana Kati na kuacha upenyo nafasi kama hakuna beki wa pembeni na yeye ni beki wa kati .Upande wake ukawa unapokea mashambulizi mengi hatari sasa sijui kama ilikuwa mbinu ya kocha au maaamuzi yake binafsi.
 
Boss ETH nasikia anataka usajili wachezaji wawili muhimu dirisha kubwa, mm naona atuletee vlahovic/ osmhen afu kiungo de jong/ Bellingham
Vlahovic hawezi kuwa na msaada epl.

Osimhen yupo vizuri ni central striker.

De Jong aachwe huko huko Barcelona yake haiendi United badala yake twende kwa Jude Bellingham, Joao Palhinha au Nicolo Barella.

I recommend Nicolo Barella
 
AWB mechi ya Barcelona alikuwa hatoki nafasi hiyo kwa kutojua au kutokana na mapungufu yake ila ilikuwa kutokana mahitaji ya mchezo.


Mechi ya kwanza alikuwa akibana uwanja ili kutengeneza narrow shape kwenye defence kuzuia kina Gavi na Pedri wasipige through balls nyingi eneo hilo.


Mechi ya Manchester Barca walianza na Sergio Roberto kama winger lakini alikuwa akicheza ndani kama ten na Bissaka ndiyo alitakiwa Kummark Sergio Roberto kila alimpomfuata akiingia kati ilikuwa inampa space Balde.

Baada ya Sergio Roberto kutoka hakukuwa tena na pattern hiyo ya uchezaji ndiyo maana alipoingia Dalot Balde hakupanda sana tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…