Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Jamaa katoa maon TU, Kuna muda tuacheni ujinga, tujadili football

Football sio uhasama, jamaa hajatukana Wala kukashfu ,why usimjibu kwa kumchallange hoja yake
Mkuu,uhasama uko wapi hapo? Wapi nimemtukana hapo? Halafu ni muda sasa umefika Watanzania mjifunze kusoma maandishi katika sauti ya mwandishi.

Halafu hizi ni kauli za kawaida sana kwenye majadiliano ya mpira,hata sioni kama kuna kitu cha kubeba kwenye kifua hapo.
 
ni haki yako kuwaza, lakini sina uhakika kuwa uwezo wa kocha upo kama unavyotaka kutuaminisha, muda ni mwalimu mzuri sana uwe na akiba ya maneno kidogo
 
Baada ya man u kumpiga Liverpool magoli manne pre season, walitamani msimu uanze sasa msimu umeanza wanatamani uishe, ndo kwanza kipigo kikubwa ni kutoka kwa Brentford tu na hajakutana na pep, jurgen k, conte na tomas T.
 
Ktk usajili kuna targets 3 kuu kwa ajili ya
  1. Plan za muda mfupi (30+ yrs) - hawa ni wale wenye experience na ni wa muhimu kwa immediate impact kwenye timu
  2. Plan za muda wa kati (23-29yrs) - hawa ni wa muhimu kuiwezesha timu iwe na continuity nzuri kutoka kwa academy hadi kwa wazoefu
  3. Plan za muda mrefu (<23 yrs)- Hawa ni kwa ajili ya plan za 10+ years to come
Timu ikifanya usajili bila kuweka hiyo mix, itakwama tu kwenye mashindano
Ndio maana sisi Chelsea kupitia uongozi mpya tumewekeza kwenye hayo malengo matatu niliyotaja
Hii mix Man U hamkuwa nayo kwa muda mrefu na ndio maana leo hii Man U imekuwa hovyo hovyo tu
 
Ndiyo apewe mkataba wa 4 + 1 years? Salary £300K pamoja na transfer fee ya €70M.


Ila kwa kile kiungo acha Casemiro aje tu lakini United kuna mahali wanafeli.
 
Yawezekana ni kweli ni panic buy chief, ila kwenda hizi match mpaka dirisha lijalo bila dm labda hututakii mema tu, tutapigwa hadi tushangae. Aje tu huku tunaendelea ku explore long term DM ajaye taratibu kuliko hii patner ya Mctominay na Fred
Hapo tupo pamoja ila shida nyingine ya United kwa sasa ni maamuzi ya kocha. Kuna wachezaji akiweza kuwa-drop bila kujali majina, uraia au status zao atakuwa na kikosi cha kwanza kizuri tu.
 
So kwa kauli yako ulitegemea tuchukue ubingwa mwaka huu???

Hata barca wanaoitwa wanajenga timu wamemuongeza robert lewo mwenye 33+,sumtime tusijitwike ukocha,wabongo tunaongea sana.

Hao glazers wasiposajili maneno meeeengi,hao viunge wakabaji wenyewe siku hizi wa kuokoteza,de jong katuvua nguo,acha tumcheki casemiro,na naiman kocha atamtumia iwezekanavyo.

Na nyie arsenal,hii ligi bado mapema saaana kuongea,maake naona mmeshaanza kuwatoa Liverpool kwenye ubingwa mmashindana na man city,shame.Miaka yote mnaanzaga ivi ivi zaidi mnaishia nafasi ya tano.

Acha iitwe panic buying lakini ni bora kuliko viungo tulionao wa kina macfred.
 
Binafsi usajiri wa casimiro na man u ya sasa. Naona ni usajiri mzuri kwa kiasi chake

Kama mtakua na kumbukumbu niliwai kusema humu ndani, mnahitaji kiungo mkabaji
Coz hakuna beki duniani akipelekewa moto mara nne mfululizo asipoteane.

Kama casimiro akipiga 6
Eriksen 8
Bruno 10
Kiungo kikiwa sold hayo mengine yatakaa sawa tu

Timu itakua na uhai apo kati kati na beki, hawatakua na pressure sana
Na points zitaokotwa za kutosha tu

De jong asingeweza kutibu tatizo la man u,

Ila de jong akitua Chelsea utakua usajiri mzuri coz pale wanae mtu anaeitwa Ngolo kante

De jong akitua arsenal itakua fresh coz tunae partey

Swali la kujiuluza,
kwanini 10 hang alikua anamng'ang'ania dejong wataki shida kubwa ni kiungo mkabaji?
Hapo ndipo ninapoona tatizo la huyu kocha wetu bwana 10 hang


City kuna fernandinho, rodri

Chelsea yupo Ngolo

Spurs bisuma

Arsenal partey

Je, man u. Yupo nani?
 
Liverpool wamemsajili Thiago akiwa na umri wa miaka 30. Usajili mkubwa.
Chelsea wamemsajili Thiago Silva akiwa na umri wa miaka 36. Usajili mkubwa.
LAKINI usajili wa #MUFC Casemiro akiwa na umri wa miaka 30 ni usajili mbaya kwanini mazee.


Acha wa sajili tu.
 
Mi nataka mkamilishe huu usajili mapema ili acheze mechi na Liverpool tuone kituko mlichoongeza kwenye timu yenu.

Yani hii timu wamiliki, wachezaji, kocha na mashabiki wote akili zao ni za ovyo sana.. mlipiga kelele kwa wadhamini sasa mmepulizwa mmeletewa DM mliekuwa mnamtaka, nina uhakika baada ya jumatatu mtataka wadhamini waondoke tena!

Hii timu hakuna wa kuiokoa hata awepo nani.. mpaka mjue mlipokosea. Timu yenu ni ya kufa tu kwa miaka 30, mtake msitake.. NIPO PALE!
 
De jong sio kama unavyo mchukulia yeye sawa ni Cm lakini anauwezo mkubwa wa kukaba ndio maana xavi aliwai kumtumia kama center back na pia aliwai kucheza kama centrel back mechi 13 akiwa ajax ambazo 10 walishina na 13 kutoa droo pia anauwezo wa kucheza midle zote ikiwemo CDM
 
Fred anashindwa kukaba uyo dejong ataweza kumkaba nani pale EPL uwanja ukichafuka

Unajua EPL wewe?

Imemshinda bakayoko
 
Fred anashindwa kukaba uyo dejong ataweza kumkaba nani pale EPL uwanja ukichafuka

Unajua EPL wewe?

Imemshinda bakayoko
Ability ya de jong katika ukabaji ni kubwa kuliko fred na ndio maana fred huwez kumchezesha CB pia D jong ukiwa nae atakuoffer vitu vingi kutokana na uwezo wake wa passing skills kubwa kuliko hao diffensive unao wazungumzia pia ten hag haitampa shida ku copy mfumo maana ni mtu ambae alishawai kufanya nae kazi kwa barcerona alikua hawez kuchezeshwa chin kutokana kuwepo kwa all time CDM sergio busquets
 
Aisee kazi ipo,so unataka umuone kwa game iyo moja tu??
 
Na unavojiita unajua mpira,casemiro ni kituko eeh,so hujawahi muona,ndo itakua mara ya kwanza kumuona sio
 
PUMBA
 
Fernandino yupo City ipi?

City center au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…