Manchester United (Red Devils) | Special Thread

"Lakini inaonekana bodi ya Man united haiko serious na usajili katika timu yao ni kama wanajaribu kubahatisha bahatisha."

Hapo ndiyo tatizo kubwa la United lilipo, shida kubwa inaanzia kwa wamiliki wao ndiyo walitengeneza mfumo wenye watu wasiojua mambo mengi kuhusu football. Watu hao ndiyo wakanunua wachezaji wengi wenye uwezo mdogo wengine wakaletwa kwasababu za kibiashara tu, wengine wala hayakuwa mahitaji ya makocha waliopita. Hayo yote ndiyo yametufikisha hapa tuna kikosi kimejaa majina tu. Hawa wachezaji ndiyo wanatutesa kwasababu hawauziki na hatuwezi kusajili bila kupunguza idadi ya wachezaji tulionao.

Na bado hiyo haitoshi wamiliki hawaweki pesa kwenye timu, wao wanachota tu faida. Msimu huu tumepata kocha mwenye malengo ya kueleweka lakini bado support ya wamiliki ni hamna kitu.

Hata hili la Ronaldo kubaki nina uhakika ni maelekezo kutoka juu, Ronaldo ni brand inayowasidia Glazers kutunisha mfuko. United siyo timu inayofanya cha maana uwanjani lakini bado inafamya vizuri kibiashara kwasababu ya akili wanayotumia Glazers kuliteka soko la mashabiki wa United.

Siku Glazers wakiondoka ndiyo itakuwa mwanzo mpya wa Manchester United. Mimi nimeshachoka kulaumu wachezaji, huu ndiyo uwezo wao walionao sisi tunataka wafanye kama thamani ya pesa tuliowanunulia ila hawa ni average players tukubali tu hali hilisi. Ila rebuild chini ya Glazers itakuwa ni kutwanga maji kwenye kinu.

Maneno ya Mourinho na Van Gaal yataishi milele.
 
Probably wanashindwa kufanya usajili mkubwa kwa kukosa imani na mwalimu.

Maana Mourinho na Van Gaal msimu wao wa kwanza walifanya usajili mkubwa ambao baadae haukulipa hivyo wanaona wampe muda kwanza mwalimu kama ataweza kudeliver kitu ndiyo wampe support sokoni.
 
duu
 
guys mnalalamika nini wakati statistics zina constant improvement. au mnataka ushindi kama enzi za ole. safari ni hatua.
 
Ronaldo auzwe tu hizi sasa ni dharau kwa wachezaji wenzake, mashabiki na timu kwa ujumla. Sababu ipi ya msingi imemfanya aondoke uwanjani kabla mechi haijaisha?View attachment 2310262
Hapo anwafundisha nn vijana huyu ndo anatuharibia team ,watu waliokuwa wanampinga walikuwa na sababu muhimu sana.

Kwa sasa aende tu ukizingatia hakuna alichobadilisha katika team ,hana mapenzi tena na club japokuwa mashabiki wanampenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…