Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Inasemekana yeye mwenyewe alikubaliana na uongozi wa juu wasiongeze mtu kikosini mpaka majira ya kiangazi hatma ya kocha wa kudumu ikiamuliwa. Priority ni top 4.

Hata negotiations za mikataba zote zimewekewa pending status. Wachezaji wanaotolewa kwa mkopo pia haijumuishi buy option clause kwa timu wanazojiunga nazo.
Akili poa hii.

Inatufanya tusiingie gharama zisizo na maana.
 
Nachojua dirisha dogo alijawai kuisaidia timu ikafanya vizuri ndo maana timu nyingi azionagi umuhimu wa kusajili dirisha dogo maana nikuja kuivuruga timu.
Kitu kikubwa watu wanachoshindwa kuelewa dirisha dogo lipo kwa lengo za kuziba nafasi za majereha ya muda mrefu ya wachezaji sio mipango ya muda mrefu.

Majira ya kiangazi mwalimu anakaa na wachezaji wote muda usiopungua wiki nane kabla ya msimu kuanza, hapa ndipo mipango mikubwa hupangwa.

Usajili unafanyika kipindi hiki huwa sio wa kuzima moto mara nyingi huwa unakaa kimipango sana.
 
Bruno Fernandez
Paul Scholes
Bruno usajili wake ulikamilika tu majira ya baridi ila alikuwepo ktk mipango ya timu ktk majira kiangazi ni viogozi tu walishindwa kukubaliana awali.

Paul Scholes ujio wake kama unakumbuka vizuri viungo wetu wote walipata majeraha ya muda mrefu wakiongozwa na Carrick pamoja na Fletcher.
 
Ina maana hata uwezekano wa kumpata Ander Herrera kwa mkopo toka PSG pia imeshindikana?
Top 4 bado matumaini ni madogo sana bila kuimarisha eneo la kiungo.
Jombaa uko serious? Kwa kikosi chetu hatuhitaji mtu wa ziada kukaa top 4.

Manchester City pekee ndiye mwenye uhakika na top 4 mpaka sasa. Waliobaki wote lolote linaweza kutokea.

Chelsea ndani ya michezo yake 4 iliyopita kadondosha points 7. Nadhani hapa unaweza kuelewa ni namna gani mtu anaweza kupoteana ndani ya mwezi mmoja tu.
 
Bruno usajili wake ulikamilika tu majira ya baridi ila alikuwepo ktk mipango ya timu ktk majira kiangazi ni viogozi tu walishindwa kukubaliana awali.

Paul Scholes ujio wake kama unakumbuka vizuri viungo wetu wote walipata majeraha ya muda mrefu wakiongozwa na Carrick pamoja na Fletcher.
Mkuu Paul Scholes aliwakuta Carrick na Fletcher? Au cjakuelewa.
 
  1. Wachezaji wote wanaovumishiwa kuondoka ndani ya dirisha hili hawana umuhimu ndani ya kikosi hivyo kuondoka kwao halitokuwa ni jambo la kujutia.
  2. Kuondoka kwao kutasababisha gharama za mishahara zipungue kwa miezi sita ijayo, kwa mfano dili la martial takribani waandishi wote wamekubaliana ya kwamba sevilla watalipa euro millioni 4 au 6 za mshahara wake, hivyo ukijumlisha na wachezaji wengineo wanaovumishiwa kuondoka upo uwezekano wa klabu kuokoa hadi euro millioni 15 au zaidi kwa miezi 6. Tuombee dili za jones au bailly, van de beek na lingard zifanikiwe.
  3. Pia kuondoka kwao kutafungua fursa ya kusajiliwa mchezaji mwengine kama uongozi utapenda kufanya hivyo.
  4. Ralf rangnick kwa nyakati tofauti alikuwa anagusia juu ya ukubwa wa kikosi alichonacho kinavyompa tabu kwenye ufanyaji wa maamuzi, nikiangalia hii hamisha hamisha ya wachezaji inanifanya niamini ya kwamba rangnick ni klopp mwengine, huenda wote wawili hawapendi kumanage kundi kubwa la wachezaji wenye viwango vinavyoshabihiana.
  5. Siku chache baada ya kumalizika kwa michuano inayojumuisha mataifa ya kiarabu, ralf alimsifia sana hannibal mejibr na akagusia ya kwamba anategemea kumuingiza kikosi cha kwanza pindi atakaporudi kwenye michuano ya Afrika, nikawa najiuliza hii ndoto itawezekana vipi ikiwa hawa waliopo wameshindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza na hapa nawazungumzia donny na lingard, tetesi zilizopo ni kwamba klabu inajiandaa kuwaruhusu wachezaji hao wawili kuondoka na mpaka muda huu hakuna tetesi zote zinazotaja wachezaji watakaoziba nafasi zao. Je Hannibal ndiye mrithi wa nafasi ya donny na lingard pindi watakapoondoka hivyo tutegemee kumuona akiwa benchi kuanzia mwezi ujao na baada ya hannibal atafuata nani kwa wale vijana wa academy?
  6. muandishi david ornstein mwanzoni mwa wiki hii aliandika taarifa zinazohusu mipango ya klabu ya kutafuta kocha mpya na amekwenda mbali zaidi kwa kusema ya kwamba mipango hiyo itaanza karibuni akiwa na maana ya kuanzia february, amemtaja pochettino, ten hag, enrique na laportegue kuwa ni target lengwa zaidi. Wewe msomaji unavutiwa na yupi kati ya hao?
  7. gazeti la the sun na mengineyo siku mbili baadae nao wakaja na taarifa za ndaaaani kabisa kutoka manchester united, eti wanasema ya kwamba klabu imeamua kusitisha mpango wa kutafuta kocha mwengine kwa sababu wana imani na ralf rangnick na anachokifanya. Nikacheka na hapo hapo nikaikumbuka comment ya Volatility aliyesema klabu inatufanyia ujanja kwa kutwambia ya kwamba ralf utakapomaliza msimu atakuwa mshauri jambo ambalo haliingii akilini. Je wewe msomaji upo upande wa david ornstein au upo upande wa gazeti la the sun na mtandao wa football90.

DAEMUSHIN
DAEMUSIN.

Mzoweyeni huyo mwanakemia wa zamani wa kiarabu kwa siku chache.
 

  1. Ralf rangnick kwa nyakati tofauti alikuwa anagusia juu ya ukubwa wa kikosi alichonacho kinavyompa tabu kwenye ufanyaji wa maamuzi, nikiangalia hii hamisha hamisha ya wachezaji inanifanya niamini ya kwamba rangnick ni klopp mwengine, huenda wote wawili hawapendi kumanage kundi kubwa la wachezaji wenye viwango vinavyoshabihiana.
Kikosi kikiwa kikubwa sana kama chetu maana yake unakuwa na kundi kubwa la fringe players.

Hawa wanatengeneza blind belief uamini kama una kikosi kipana ila kiuhalisia unaweza kukuta una wachezaji 11 tu unaowaamini zaidi.

Makocha wengi wazuri huwa hawapendi kufanya kazi na kundi kubwa sana la wachezaji hasa hasa wakienda sana ni wachezaji 26 tu. Wanaojazia nafasi ni vijana wadogo u-20.
 
Nilikuwa najiuliza inakuwaje Fred anaanza Brazil kwa recent performance yake ila nimepata jibu kuwa Brazil hawana watu kabisa zama hizi.
Brazil ya sasa hivi hata Uingereza wana timu nzuri kuzidi wao.

Kikosi chao cha kwanza wachezaji 5 wanaoanza panga pangua wanacheza PL.

Miaka hii ni ngumu kupata namba timu za taifa za ulaya kuliko timu za amerika kusini.

Can you imagine mchezaji kama Coutinho bado anaitwa timu ya taifa na anacheza.
 
Back
Top Bottom