Kwa jinsi tulivyocheza jana tushukuru tumepata hata hiyo point 1. Manchester United kwasasa haipo levels za Man. City wala Liverpool kwa soka la uwanjani, United imebaki kuwa timu kubwa yenye wachezaji wenye majina makubwa lakini kitu kinachofanyika uwanjani ni 0. Timu yetu sasa hivi inategemea mpira wa bahati sana ni mechi chache tunashinda kwa kucheza mpira wa hadhi ya United.
Hii droo siyo mbaya sana kwa kile walichokifanya wachezaji jana, ukiangalia kuanzia game ya Norwich ni vitimu tulivyotakiwa kupiga siyo chini ya goli 3.
Kama Rangnick alivyosema kuibadilisha timu kiuchezaji siyo suala la muda mfupi, ukizingatia alipokuja hakupata muda mrefu wa ku-train na timu na baada ya Carrington kufungwa nahisi pia imeyumbisha timu kidogo.