Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Akii nahisi hii timu imelogwa ... hakuna kocha anae itaka hii timu !!
Mimi nakomalia kwenye DNA tusiipotezee DNA ya timu yetu .. na mwelekeo sahihi uko kwa Brendan Rodgers.. naamini sana mfumo wake wa kupress
... cha muhimu si mpira wa kupress? mbinu anazo ..
Akishindwa tutajaribu msimu unao fata !! Tuwe tunajaribu jaribu makocha mpaka rooney atapo komaa kuifunza timu yetu

DNA ni jambo la muhimu sana kwa timu yetu .. na hawa malejendarii ushauri wao ni wa kuzingatiwa sana maana wanaijua timu yetu nje ndani
 
DNA lazima ifatwe

Rooney au wamrudishe tu mwenyewe Ole sosha

 
Mchezaji wa zamani wa United Patrice Evra amemshukuru Ole Gunnar Solskjaer kwa kazi yake na amewapa kitisho wachezaji wa Manchester United akisema "ninakuja nyuma yenu"

Evra ameandika katika mtandao wa instagram "
" Asante rafiki yangu kwa kutufanya tuiamini tena Manchester United. Kwa bahati mbaya usipopata matokeo watu husahau mazuri uliyoyafanya. Kwa wachezaji wote wa Manchester United ninakuja, tuonane katika mechi na Arsenal ". Evra alikuwa mchezaji mwenzake na Solskjaer wakati wa msimu wa mwisho wa Ole akichezea Manchester United. Wote kwa pamoja walikuwa chini ya Sir Alex Ferguson.

#KitengeSports
 
Umpe timu evra kweli timu yetu imekuwa Kama Namungo
 
Pamoja na yote ila kajitahidi sana kutengeneza kikosi hata ile kuingia top four consecutive two season ilikuwa imeanza kusahaulika.

Atleast kocha mpya sasa atakuwa na sehemu ya kuanzia.
 
Makombe mengi - Jose

Points nyingi - Jose

Least goals conceded - Jose

Highest xG - Jose

Higher winning rate - Jose

Kutopoteza ugenini mechi nyingi - Jose

Kwanini media zinamlabel Jose kama destroyer wa United hiyo ni siri yao
 
Makocha wengi waliohusishwa na united wameitolea nje isipokua Pochettino.

Tuchel alisema ni ngumu sana kumanage PSG kwa sababu siyo tu unatakiwa kuwa mlezi wa mastar wa pale bali unatakiwa kuwalea na ndugu na marafiki zao.

Nafikiri hilo linamkumba Pochettino pia. So haondoki kwakua mkewe yupo London anaondoka kwakua kuisimamia timu yenye mastar wengi vile ni mzigo. Kingine ni namna PSG inapata ushindi wake huku inashindwa kupata clean sheet.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…