Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Waingereza ni wachezaji wanaofanya vizuri msimu mmoja, unaofuatia wanakata moto.

Hapo united, nioneshe muingereza anaefika levels za Bruno? Halafu angalia bei zao.

Ukienda nchi zingine unapata wachezaji quality kwa bei nafuu. Ila tupo busy kununua waingereza kwa bei kubwa.

Maguire akacheze Aston Villa, Bissaka aende Crystal Palace, Shaw aende Arsenal huko, McTomminay aende hata Blackburn. Hawa ni wa kucheza vitimu vya ajabu. Sio wavae badge ya timu kama Man Utd.
 
Tatizo kubwa sana ni incompetent coaching staffs. Ole ni mweupe sana tena sana.

Hajui team selection, game management, formation etc. Wachezaji wameanguka viwango sana.

Martial, Maguire, Sancho, Shaw.

Wengine wanakoseshwa nafasi mtu kama DVB, Baily wana uwezo mkubwa sana wa kuisaidia timu ila huyu mpuuzi bado anawaweka bechi.

Ferguson astaafu rasmi, hatuhitaji influence yake tena kwenye team.
 
Hii class ya 92 ni wapuuzi wote. Wakae kimya.
 
Pogba na yeye ikiwezekana aondoke january,,asimalize hata msimu.
Tatizo ni kocha na sio Pogba.

Wachezaji haohao wanafanya vizuri national team ila wakija kwetu wanakuwa magalasa.

Toka enzi za kina Lukaku sahivi Pogba. Lindelof, Bruno au CR7 wakiwa national team ni tofauti sana na wakiwa kwetu.
 
Ukiangalia perfomance ya Baily huwezi kuamini ni mchezaji anayesugua benchi mbele ya maguire.
Maguire angekuwa anawekwa bench, sahivi tungesahau kama kulikuwa na kocha alieitwa Ole alishawahi fundisha United.
 
Jana kwanza credit zangu kwa mkuu wa Majeshi Baily sijawahi kuwa na mashaka nae hata kama ana mistakes zake lakini hafikii ujinga wa captain hewa jana kaupiga mwingi katusave sana pia.
NI mda tuangalia combination mpya ya mabeki sasa ila ole hapana asee bado sitaki kuamini moto aliokuwa nao Don na Sancho umeishia hapa United kuna sehemu hawatendei haki hawa watu kwakweli.
 
Mpe heshimaye babu, anza na Sir
 
Pogba na yeye ikiwezekana aondoke january,,asimalize hata msimu.
NYUMA YA PAZIA: SIR ALEX ALITUONYA KUHUSU POGBA NA YULE BWANA KIBONGE



INAKERA sana. Sidhani kama ametuonyesha heshima yoyote ile kama nikiamua kusema kweli. Nina furaha kwamba kama wanasoka wakiendelea kufanya hivi ni bora wasifanyie mambo haya kwetu,” alisema Sir Alex Ferguson huku sura yake ikiwa nyekundu akiwaka kwa hasira kali mbele ya vyombo vya habari.

Ni miezi 132 sasa imepita. Ilikuwa mnamo Julai 2012 wakati Sir Alex alipokuwa akimshutumu kinda Paul Pogba kwamba alikuwa amesaini Juventus muda mrefu uliopita ingawa yeye na wakala wake, Mino Raiola walikuwa wamemficha na walikuwa wanajifanya wapo katika mazungumzo ya mkataba mpya na Manchester United.

Sir Alex alikuwa ameshtukia dili. Kilichobaki kilikuwa historia. Pogba alisaini Juventus Turin. Akageuka kuwa staa mkubwa. Baadaye akarudi Old Trafford kwa pesa nyingi. Mpaka leo sijajua kama Sir Alex aliridhika kuona Jose Mourinho na mabosi wake wakivunja rekodi ya uhamisho wa dunia 2016 kumrudisha Pogba, Old Trafford. Na kama Sir Alex alitabiri kwamba wachezaji wenye tabia kama za Pogba wakae mbali na Old Trafford na bado hakusikilizwa, basi huenda jinamizi la Pogba limerudi tena Old Trafford. Miaka kumi na ushee sasa hivi na United imejikuta katika mtego uleule. Tuliambiwa tusikilize wazee. Paul Labile Pogba mpaka sasa hajasaini mkataba mpya Manchester United. Mkataba wake unakaribia kumalizika mwishoni mwa msimu. Jana nilikuwa nasoma mahala kwamba Manchester United wameweka mezani mshahara wa Pauni 400,000 kwa wiki. Utamfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi Ligi Kuu ya England.

Swali ni je atasaini? Bado sijaamini. Nyuma yake ana mtu fulani hivi kibonge mpenda pesa anayeishi Monaco katika jumba la kifahari akitengeneza noti kwa vurugu kupitia dili kama hizi. Mino Raiola. Sina uhakika Raiola anawaza nini.

Wakati Pogba akiondoka 2012, ilidaiwa kwamba alikuwa amechoka kusubiri kumuona Paul Scholes akizeeka. Alidai kwamba alikuwa anaondoka kwa sababu za kisoka. Kumbuka kwamba aliondoka bure licha ya United kumkomaza.

Nadhani Raiola aliichungulia pesa mbele ya safari. Alikiangalia kipaji cha Pogba, akamnong’oneza asisaini mkataba mpya. Nadhani walitengewa kitita na Juventus. Akasaini bure Juventus. Baadaye akageuka kuwa staa mkubwa.


Kwa sasa sijui Raiola ana mawazo gani. Amefanikiwa kukaribia kuifikisha United kule ambako aliifikisha 2012. Kuwa na bidhaa adimu isiyo na mkataba. Kuna uwezekano mkubwa Pogba asisaini mkataba na United kisha akaondoka bure msimu ujao. Mpaka sasa Raiola anachukiwa pale Milan. Ametoka kufanikisha dili la uhamisho wa bure kwa mteja wake Gigi Donnarumma mwenye miaka 22 tu. Milan imemlea vilivyo lakini Raiola kafanikiwa kumshawishi asisaini mkataba mpya mpaka ameenda bure PSG.

Swali kwa Pogba ni je, kuna uwezekano akiondoka bure akalipwa Pauni 500,000 kwa wiki mahala? Inawezekana. Pogba ni mchezaji mkubwa. Manchester United watakubali aondoke bure mwakani akiwa na umri wa miaka 29? Ni swali linalofikirisha. Vipi kama Pogba alikataa dau lao la Pauni 400,000 kwa wiki? Vyovyote ilivyo Mino Raiola ametulia tu. Ana bahati kwamba ana kila sababu ya kutulia. Pogba ameishia pazuri. Aliuwasha moto katika michuano ya Euro kiasi kwamba United wametamani kuendelea kuwa naye hata kama kuna watu ambao mioyo yao imegawanyika.

Lakini pia ametengeneza kombinesheni nzuri na Bruno Fernandes. Alikuwa na msimu mzuri wakati akiipeleka Manchester United katika Top Four na kuifikisha katika fainali za Europa ambapo walifungwa na Villarreal ya Hispania. Hapa anaigawanya mioyo ya United.

Kuna kina Roy Keane na waandamizi wengine wa United wamekuwa wakimpa presha Ole Gunnar Solskjaer aachane na Pogba. Lakini unapokumbuka mambo aliyofanya Euro unajiuliza mara mbilimbili ni wapi unaweza kumpata Pogba mwingine kirahisi katika dunia ya leo. Yote haya Raiola na Pogba hawajali. Wameiweka United katika kona ambayo Sir Alex aliwahi kuionya kuhusu aina ya wachezaji kama Pogba. Kwa sasa hata United ikiamua kumuuza Pogba haiwezi kuwa na nyodo kwa sababu upande wa kina Pogba ndio umeshika mpini. United wameshika makali. Na hakuna kitu ambacho kina Keane watachukia kama kumuona Pogba akiondoka na kitita cha Pauni 400,000 kwa wiki katika mkataba mwingine wa miaka minne au mitano ambao amewekewa mezani kwa sasa. Kina Keane watang’ata meno kwa hasira kali. Hii inatokana na ukweli kwamba licha ya Pogba kuwaweka United katika kona nzuri kwa sasa, lakini kuna wakati anaudhi. Kuna wakati fomu yake inapotea na mara nyingi anajikuta akibadilisha staili ya nywele zaidi kuliko kufunga mabao.

Timu pekee ambayo inaweza kumchukua Pogba kwa sasa ni PSG. Wale mapacha wa Hispania, Real Madrid na Barcelona hawana kitu. Ni PSG tu ndio ambayo inaweza kumrudisha nyumbani Pogba. Iwe kwa dirisha hili au kumchukua bure msimu ujao. Katika dirisha hili PSG imechukua wachezaji wengi wa bure. Kwa hiyo haitashangaza wakikwepa kuvunja kanuni za masuala ya matumizi ya pesa za Uefa hata kama wakimchukua Pogba. Kina Lionel Messi, Donnarumma na Sergio Ramos wote wamekwenda bure Paris. Watu wengine ambao wangeweza kumchukua Pogba ni Manchester City, lakini sioni uwezekano huo. Pep Guardiola hana uhusiano mzuri na Raiola. Lakini hapohapo City wana Kelvin De Bruyne. Wana Ilkay Gundogan. Hawana shida na Pogba.
 
Ferguson astaafu rasmi, hatuhitaji influence yake tena kwenye team.
Nilifikiri ni mimi tu nilikuwa na mtizamo huu pia. Naamini moja sbb inayofanya huyu mpumbavu Ole aendelee na kazi yake behind the scene Fergie anafanya kazi kama unofficial technical advisor ana ushawishi mkubwa sana ktk ofisi ya Ed Woodward.

I wish mtu atayechukua nafasi ya Ed Woodward aondoe hii influence ya hawa ma-legend ni kama wanataka timu iongozwe na mtu wanayeweza kumpa maelekezo watakavyo.

Umewahi ku-imagine kama Chelsea wangekuwa na huu upumbavu wa nguvu ya ushawishi wa ma-legend isingekuwa rahisi Frank Lampard kufutwa kazi maana kila mtu angemtetea.
 
100%
 
Hakika Jombaa. Ila huyu kilaza Ole atatuchelewesha sana.
 
Telles mimi ananiuma roho sana yule jamaa
 
Maguire ana matatizo mengi sana ukiondoa recklessness.

Maguire ana tatizo kubwa la positioning kitu ambacho huwafanya wenzake wafanye makosa pia.

Hana tactical awareness kama defenders wengine ambao ni last defenders.

Ni captain lakini hana leadership yoyote zaidi ya kuwa na mwili mkubwa tu kuliko wachezaji wengine wote uwanjani.

Hawezi kuresist pressing hata ya mtu mmoja.

Kifupi Lindelof huwa anajitahidi sana kuficha makosa ya huyu mwamba.

Angalia mechi ambazo Lindelof amecheza na Bailly ana cleansheet nyingi kuliko walizocheza na Maguire kwenye timu ya taifa always Lindelof ni man of the match katika timu yenye kundi kubwa la wachezaji average with loads of clean sheets.
 
Tatizo ni kocha na sio Pogba.

Wachezaji haohao wanafanya vizuri national team ila wakija kwetu wanakuwa magalasa.

Toka enzi za kina Lukaku sahivi Pogba. Lindelof, Bruno au CR7 wakiwa national team ni tofauti sana na wakiwa kwetu.
Mbona hata wachezaji wetu wa kingereza wanafanya vizuri kwenye timu zao za taifa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…