Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hata Norwich huwa wanacheza kwa pattern ya kueleweka kuliko man United.

Ni heri Ole angemrejesha Rene Moulisten kwenye coaching staff akawaondoa Carrick na Kierian Mackena.

Timu gani duniani inayocheza hovyo kama united kwa sasa ?.

Mbeya kwanza wanacheza mpira mzuri kuliko Manchester United.
 
Mbeya kwanza mbali ivyo simba sports club inacheza mpira mzuri kuliko united yangu
 
Kocha mzima kabisa anakuja kwenye press anasema kuna aina fulani ya defensive anashindwa kuzifungua ili apate goli yani kauza mbinu za kivita kweupeee.
Ni sawa nchi iseme sisi ukija na askari wa anga unatupiga utuuwe maana upande huo tu dhoofu ilihali.
 
Borrusia Dortmund CEO Hans- Joachim Watzke alipokuwa akihojiwa na kituo cha habari kinachoitwa Sport 1 amedai ya kwamba moja kati ya sababu kubwa iliomfanya jadon sancho ashinikize usajili wa kuelekea manchester united ni kule kukoseshwa nafasi ya uhakika (kipaombele) cha kucheza timu ya taifa licha ya kufanya vizuri sana alipokuwa bundesliga (Dortmund) kitakwimu.
===============
kwani huko manchester united ukimuondoa harry maguire kuna mchezaji mwengine wa kiengereza mwenye uhakika wa kucheza kila mechi ya timu ya taifa (najua atatajwa luke shaw aliyerudishwa msimu huu kikosini).

halafu kama kucheza premier league inaweza kuwa sababu kuu ya kucheza timu ya taifa ya england mbona alexander arnold hapewi nafasi haliyakuwa kitakwimu ni bora zaidi kuliko trippier, tumuache gareth southgate na balaa lake la 3-4-3

zamani tuliambiwa england walikuwa na kizazi cha dhahabu kilichokuwa na uwezo wa kuwapa mafanikio jambo ambalo ukikaa ukilifikiria utagundua ya kwamba hilo suala halina ukweli wowote (na mimi niliuamini uzushi huu) .

ukweli ni kwamba baadhi ya maeneo waingereza walikuwa na wachezaji wazuri sana waliokuwa na uwezo wa kugombania namba taifa lolote ila kuna baadhi ya maeneo walikuwa hawana wachezaji wenye viwango vya uhakika ndio maana walikuwa wanasumbuka kuvuka hata robo fainali especially pindi inapotokezea mchezaji fulani amekosekana au amecheza chini ya kiwango.
  • goalkeeper walikuwa ni kawaida sana (david james, paul robinson, robert green)
  • mpinzani wa gary neville alikuwa ni danny mills, wes brown, phil neville (wote hao ni wachezaji wenye viwango vya kawaida sana)
  • mpinzani wa ashley cole alikuwa ni wayne bridge (fullback wa kawaida sana)
  • walinzi wa kati walijaaliwa kuwa na kizazi bora sana hilo halina ubishi
  • DM hawakuwa naye, baadae alikuja michael carrick ila hakupewa nafasi
  • playmaker walijaaliwa kizazi bora sana (lampard, gerrard, scholes)
  • winga (beckham na joe cole pekee ndio wenye ubora), ila hao wengine wakiemo darius vassel na kieron dyer walikuwa na kiwango cha wastani
  • mshambuliaji walijaaliwa kizazi bora (michael owen, wayne rooney, alan shearer, andy cole, robbie fowler)


kizazi hiki kilichoanzia world cup ya 2018 wamejaaliwa kuwa na kundi kubwa la vijana wenye vipaji kwa kila eneo (position), eneo pekee walilonyimwa mchezaji mwenye kiwango bora ni namba 8, laiti kama wangelikuwa na mchezaji mmoja anayefikiwa kiwango cha scholes, lampard au gerrard pengine tungelikuwa tunazungumza hadithi nyengine.

kwa miaka 10 hii waingereza wataendelea kuzalisha kundi kubwa sana la vijana wenye ari ya kucheza mpira kutokana na mikakati bora walioiwekana na kuitekeleza, jukumu lililobakia ni la benchi la ufundi wanatakiwa kuhakikisha wanaunganisha wachezaji hawa na kutengeneza strucuture inayoeleweka ya kiuchezaji kama walivyo spain haijalishi ni kocha yupi ameletwa kikosini.
 
Sir Alex Ferguson on the player he wished #mufc signed: "In reality, you have to say, the only one that always comes to my mind and that's Gascoigne. He was absolutely fantastic. I think if we'd have got him, he would have had a great career, I really do."

manutd |
#GGMU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…