Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hivi kweli Messi ndio tumeshindwa kumpata..
Tungempata mauzo ya Jersey tu yalitosha kulipa mshahara wake vizuri tu.
Ishu ya jersey huwa kuna porojo nyingi sana.

Hiko hivi..Adidas huwa wanatupa mzigo(mpunga) fixed kwa mwaka...mfano £80m..wakishatupa hii fedha kazi ya kutengeneza na kuuza jezi ni ya kwao na fedha wanachukua wao sio sisi.

So hii ya kusema tutarudisha fedha ya usajili kwa kuuza jezi ni hapana..labda kama hiyo hela tunaongea na Adidas ili wao nao waweke mzigo kwenye huo usajili ili kuboost mauzo ya jezi na fedha zao zirudi na faida..kitu ambacho pia FFP(Financial Fair Play) sidhani kama watakifumbia macho.
 
CM ni mediflder aina gani mkuu?
CM ni centre mediflder.
Maana hata CDM au attacking mediflder wote ni central mediflder.
Sasa ulimaanisha CM ni nn?
CDM siyo Central midfielder kwa maana ya kuwa box to box.

Mfano mzuri wa CM ni Toni Kroos, Paul Pogba, Mateo kovacic, Marco Verrati, Bastian Shweinsteiger, Ikay Gundogan, Marcelo Sabitzer Joao Moutinho.

Kati ya hilo kundi umeona kuna CDM hapo ?
 
Wewe tutajie hao uliowaona.
 
Hivi kweli Messi ndio tumeshindwa kumpata..
Tungempata mauzo ya Jersey tu yalitosha kulipa mshahara wake vizuri tu.
Bora tumemkosa, hata mimi mwanzo nilikuwa natamani aje OT ila ukiangalia uhalisia angekuja kwenye timu yetu yeye ndiyo angekuwa mfalme pale na ingeleta shida kuja kumpata mchezaji wa level zake ili asijione yeye ndiyo yeye katika timu. Ni kama ishu ya Pogba mwanzo alitusumbua sana ila kwa ujio wa Bruno imesaidia kumuweka sawa na kutokujiona yupo juu ya klabu.

Messi ni mchezaji mkubwa sana kucheza kwenye timu yetu hii, ni lazima ukubali hili. Timu anayoenda anakutana na World class players karibia kikosi kizima, the likes of Neymar (ana rekodi yake matata) Mbappe, Ramos. Huko kunamfaa zaidi au timu nyingine ni Man. City (nimefurahi wamemkosa).
 
Kwa hili nakuunga miguu na mikono mkuu.
 
Still wachezaji wetu kuna wasiostahili kuwepo kwenye kikosi na wengine mishahara yao haiendani na viwango vyao.
 
CDM siyo Central midfielder kwa maana ya kuwa box to box.

Mfano mzuri wa CM ni Toni Kroos, Paul Pogba, Mateo kovacic, Marco Verrati, Bastian Shweinsteiger, Ikay Gundogan, Marcelo Sabitzer Joao Moutinho.

Kati ya hilo kundi umeona kuna CDM hapo ?
Mkuu unaposema centre mediflder.
Bado hujachambuwa ni yupi?

Centre mediflder
Either attacking
Or defensive

Wote ni centre mediflders.( viungo wa kati)

Unatakiwa useme mediflder wa aina gani..
Cm

Ni sawa useme neno DRIVER.

wapo madereva wa Lori,bus,,,ili kuwatambuwa lazima useme Lori driver.
Au bus driver..

Centre mediflder ni kiungo wa kati kwa kiswahili.
Bado hujaelezea ni kati wapi anacheza..
Mediflders wote Attacking na defensive wote ni centre mediflders.
 
Me nafikiri man u wanahitaji kiungo mchezeshaji mfano verrati anavyo cheza psg... jorginyo anavyocheza chelsea...modric anavyo cheza Madrid....tiago pale liverpool hawa wote wanautafaut na fred na mctomnay pale man u hawana uwezo mkubwa wa kupiga pasi na kuichezesha timu vizur lakn kwenye ukabaji wapo vizuri zaid
 
inamaana hatusajili tena ? kwahiyo kam pogba na bruno wote watakuwa wanaanza basi scot au fred mmoja atakuwa anacheza namba 6 ! bora fred
 
Hujui unacho kiandika....fred na tom ni wachezeshaji? Au hao uliowataja na bruno wanatofauti gani katka roles on the pitch..
 
Ni kwl mkuu Fred na macc Tommy hawana viwango bora ktk man u.

Tatizo linaanzia kwa pogba yupo slow sana.
Anasababisha udhaifu mkubwa ktk kiungo cha chini.
Anatakiwa kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kutoa pasi za macho kama alivyokuwa Michael Carrick enzi zake..

Fred ili awe bora lazima umchezeshe na Mac Tommy.
Ukimchezesha peke yake yeyote kati ya hao wana floppy..

Lazima tupate mtu DM wa uhakika tena mwenye uwezo mkubwa kucheza na dimba..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…