Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Babu apige kelele asaidiwe DM anunuliwe.
Sio kila msimu tunaanza tukijua kuna pengo ambalo yeye anachukulia kama sababu ya kutofanya vizuri.
Inakuaje tunashindwa kumalizia hii kazi kwa kutoa 30-50$ kununua DM?
tuna wachezaji 33 waliopo kikosini kivyovyote patahitajika kwanza kuondolewa kwa baadhi ya wachezaji kwa ofa sahihi ndipo klabu iangalie upande mwengine wa usajili.

muandishi samuel luckhurst anasema upo uwezekano wa kusajiliwa mchezaji wa tatu ndani ya dirisha hili ila swali linabaki ni eneo lipi litakalopewa kipaombele, hapo ndipo unapokuja umuhimu wa kuondoa wachezaji wasiohitajika ili kukaribisha usajili mwengine, kwa mfano tunahitaji mlinzi wa kulia (trippier) lakini hili litawezekana pale tu klabu itakapokwishafahamu mustakabali wa diogo dalot, haitowezekana kwa klabu kumsajili trippier huku diogo dalot akiendelea kubaki kikosini.

kuhusu DM taarifa zinadai Ole anampenda zaidi lile toto la kiengereza aliyewekewa thamani ya paundi millioni 70 kwenda juu, klabu pia inafuatilia kwa umakini wachezaji wengineo wanaotajwa hadharani na wasiotajwa (tuna mtandao mkubwa wa scouting)
Imagine tulianza kumfuatilia saul tokea nyakati za david moyez lakini maamuzi yakawa ya kijinga

tusubirie kuanzia tarehe 20 ndipo tutakapofahamu muelekeo wetu dirishani
 
Ndio maana mkafungwa final mzee.....yani mchezaji mzuri humpimi kwa magoli na assist?? toka lini? ingekuwa hivyo Messi asingekuwa maarufu maana magoli ndio yanamuweka juu,

kuna jamaa apojui hapo record ya Messi kwanini wasingeweka ametuliza vozuri mpira mara 12358 ila wameweka amescore magoli mangapi....

Pia ingekuwa hivyo Chelsea wasingeenda toa paund mil 100 kwa Lukaku ambaye control hana ila anamagoli 20+ kila msimu
 
Henderson
dean henderson amepewa mapumziko nafikiri alipata corona hivyo upo uwezekano mkubwa wa kuanza ligi na david degea
cavani bado amepewa mapumziko, upo uwezekano wa kuanza ligi huku mshambuliaji akiwa ni greenwood au anthony martial.

kama tutacheza kwa nidhamu kwa dakika 90 za kila mechi kama walivyofanya liverpool misimu miwili iliopita tuna uwezo wa kufanya makubwa bila ya kuangalia maadui wetu wamejipangaje, mechi nyingi tunacheza huku morali ya kuwadhibiti maadui ikiwa ni ndogo (tunazichukulia mechi ni rahisi)

PTER ana maneno yake ya kiengereza anapenda kuyatumia pindi anapomzungumzia Ole na timu yake
 
We jamaa si uwe comedian tu.


Striker huwa haitaji mambo mengi, halafu nani kakuambia mpira siyo statistics?

Watu wangekuwa wanashinda basi mechi kwa kuupiga mwingi na siyo magoli.

Bruno Fernandes atawakera sana. "IN A LEAGUE OF HIS OWN." Dadeeki!!!
 
barcelona sijui walipatwa na ugonjwa gani uliosababisha kupotea kwa akili za kiuongozi, eti griezmann analipwa takribani euro laki 6 kwa wiki, frankie dejong analipwa takribani euro laki 4.

leo mashabiki wameamua komzomea griezmann pindi alipokuwa anawasili viwanja vya mazoezi, wanaamini uwepo wake ndio sababu ya klabu kushindwa kuafikiana na kanuni zilizowekwa na la liga.
 
Nimejaribu kupanga first eleven yetu bila kuangalia fitness na injury..yaani kama tusipo sajili tena our strongest XI itakuwa ndo hiyo..sio kikosi cha kucheza game za ufunguzi za ligi or something.

Swali langu ni kuwa ni kikosi kinachoweza kutupa ubingwa chini ya mbinu za Ole??.
 
Hivi hizo kanunu za La Liga zinasemaje?
 
Nimesema makocha wenye akili kubwa ndio wanajua vigezo vya kuchukua mchezaji ,hao wakina ole si average manager tu ,..

Lukaku ni jipu lingine kama Chelsea wakimchukua basi wanaenda kupigwa mchana kweupe ,...

Pale Chelsea namkubala Werner ,aisee kama hujui ,uchezaji wa Werner ndio modern football ,anakosa magoli lakin movement zake kwenye uwanjan unakosa sababu ya kutomweka first eleven ...

Huwezi kucheze na Mtu hajui kucontrol mpira ,hawezi kuficha mpira,akipewa pasi timu nzima inakuwa na wasiwasi kwan anapoteza chapu ,yeye ni kubutua tu ,hakuna kocha kwenye akili timamu anaweza kumkubali Mtu wa namna hio unless wachezaji wenzake wamfiche ....

Nowadays namba sio kigezo cha kumsajili mchezaji ,narudia tena anafanyiwa observation live on pitch ...
 
tuna wachezaji 33 waliopo kikosini kivyovyote patahitajika kwanza kuondolewa kwa baadhi ya wachezaji kwa ofa sahihi ndipo klabu iangalie upande mwengine wa usajili.
Vizuri,ila nilitamani tupate mchezaji sahihi mapema ili azoeane na wenzake kabla ligi haijaanza halafu tuanze kutafuta soko la wasiouzika wetu kama italazimu.
 
Mkuu maswala ya kuaangalia Google anamagoli ,sijui assist ndio kimempoteza samata ...

Mpira sio kusubili utafuniwe wewe umalize mpira ,ni udambwi udambwi mwingi ...

Mpira wa kubutua butua tu kama kina lukaku ni wa kizaman na unaenda kuisha soon ,..

Na lukaku kama anaenda Chelsea basi anapotea soon,ile sio timu ya kusubili ushushiwe mpira ubutue golin ,..

Ndio maana aguero hakufit kwenye mfumo wa pep ,ila zaman alikuwa star ,kwan mifumo ya mipira inabadili ..

Na makocha wakubwa tu ndio wanajua hilo ,morihno mpira umemshinda kwasababu kama hizo ...

Modern football ,play as team ,defend as team ,attack as team ,trust me kocha atakayepata wachezaji wa kufiti huo mfumo ,hakuna team itakayoweza kupita hapo ...
 
Nowadays namba sio kigezo cha kumsajili mchezaji ,narudia tena anafanyiwa observation live on pitch .
upo sahihi lakini pia wanachunguza na takwimu zake za huko uwanjani, hivi karibuni niliwahi kusoma taarifa inayohusu uchunguzi wa rafael varane pamoja na walinzi wengine waliokuwa wakifuatiliwa na benchi la ufundi (pau torres na jules kounde).

man utd walimuangalia rafael varane kwa mechi mbili tu na mechi zote hizo alicheza ovyo kwa kufanya mistake (blunders), kama benchi la ufundi, scouting na wataalamu wa data (data analysts) wangelimuhukumu varane kwa hizo mechi mbili za ndani ya uwanja walizomshuhudia bila ya shaka wasingelifikia hatua ya kumsajili.

je walirudi wapi?
bila ya shaka walirudi kwenye takwimu zenye kuonyesha uzuri wake na madhaifu yake ndipo wakafikia maamuzi ya kumsajili
 
kuhusu DM taarifa zinadai Ole anampenda zaidi lile toto la kiengereza aliyewekewa thamani ya paundi millioni 70 kwenda juu,
Hapa ndipo huwa nakosa imani na Ole kama serikali iliyopo madarakani.
Inawezekana vipi talent zote yeye anaona england tu licha ya kwamba tuna timu kubwa ya scout dunia nzima kasoro tanzania tu?
Hili dili likitokea kweli,na endapo Dean akachaguliwa kuwa namba moja wetu,tutakuwa na wachezaji 7 wa kiingereza ndani ya kikosi chetu cha kwanza!
Dean Henderson
Aaron Wanbisaka/Trippier
Maguire
Shaw
Rice
Sancho
Rashford
 
Hamia huku tujue moja naona moyo wako uko huku ndiyo maana hubanduki kwenye uzi huu
 
Nasi pia tujiangalie na uchumba tunaolazimisha kwa labile maana inaelekea kuharibu structure ya mishahara ya timu na matokeo yake tutakuwa tunavutia kwa pesa na sio historia nzuri au mapenzi kwa klabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…