Manchester United (Red Devils) | Special Thread

usajili wa jadon sancho hauwezi kuathiri nguvu yetu ya usajili msimu huu, sancho atasaini mkataba wa miaka 5 na kwa mujibu wa makubaliano kati ya timu mbili husika borussia watapokea takribani paundi millioni 15 kwa kila mwaka.

tusisahau msimu uliopita thamani ya sancho ilifikia euro millioni 100 hadi millioni 120, uvumilivu wa mwaka mmoja umepelekea thamani ya sancho ipungue mpaka kufikiria euro millioni 85.
wanaosema tumefanya biashara kichaa wajitathmini, kwa miaka 8 sasa hatujawahi kushuhudia biashara mfano wa hii.

ukija kwa upande wa camavinga wenyewe wamemrate thamani ya euro millioni 100 lakini kwa mujibu wa taarifa za jana ofa ya kwanza inayotarajiwa kuambatanishwa ni euro millioni 30 tu.

real madrid wanataka euro millioni 60 hadi 70 kwa rafael varane lakini klabu haina nia ya kuvuka euro millioni 40.
tuendeleee kutafuna kachumbari, nyama zipo chini.
 
Pogba to PSG?..

Ikija offer wewe kama wewe ungekubali kumtoa?
 
PSG midfields
  1. marco verratti
  2. idrissa gueye
  3. ander herrera
  4. paredes
  5. danillo
  6. georginio wijnaldum
  7. raphinha
  8. angel dimaria
  9. maquinhos
nitashangazwa sana na uamuzi wa camavinga kama atakubali kujiunga na PSG kwa sababu zinazoelezwa kwenye vyombo vya habari, sidhani kama ni sehemu sahihi kwake yeye kwa wakati huuu anaohitaji zaidi dakika za kutosha pamoja na malezi bora ya ndani na nje ya uwanja.

wachezaji wenye umri mfano wake wanatakiwa kuangazia zaidi maisha yao ya ndani ya uwanja kuliko kile wanachoingiza kwenye account zao za kibenki na bahati nzuri Man united tuna uzoefu mkubwa sana wa kulea vijana mfano wake kwa takribani nusu karne.

kama ataikataa manchester united basi ni bora aende arsenal

 
Dunia inazunguka haraka sana,siku hizi mchezaji anapendelea kuichezea psg badala ya man utd!
Anyway,tufosi dili ya huyu dogo aje OT hata kama kwa kumuiba,no way out.
Muda si mrefu tutaanza kuwa kama maswahiba wetu arsenal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…