Mtu wa namna hiyo pale United tulimpata ila Ole kwa ujinga wake mwenyewe akamwacha akaenda.
Ander Hererra ndiyo mchezaji aliyekuwa na discipline ya hali ya juu sana uwanjani kuliko mchezaji yoyote wa United kumshuhudia post Ferguson Era,
Alikuwa tayari kucheza namba yoyote uwanjani kufanya kazi chafu yoyote uwanjani ili timu ishinde.
Mourinho alimpenda sana Herrera kwa kazi kama hizo, wachezaji aina ya Herrera na Park siyo lazima acheze mechi zote msimu mzima wao wana mechi zao maalumu na mechi hizo ndiyo decisive kwenye kuamua hatima ya msimu wako kwenye ligi.
Herrera alifaa kuwa captain wa united siyo kuacha aondoke kwa free transfer.