Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Tungekuwa serious kidogo tu,tungebeba EPL msimu huu..
Kuna kitu kama umegundua Ole anatumia mbinu ambazo haziendani na aina ya wachezaji alionao kikosini. Mechi nyingi anazifanya zionekane ngumu bila sababu ya msingi.

Kwa aina ya wachezaji tulionao inapaswa tucheze offensively zaidi na sio kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza. Tukikaba sana huwa tunashambulika kirahisi sana na tuna ukuta mbovu sana.

Kwa maoni yangu anapaswa awe anamtumia mmoja tu kukaba kati ya Fred au Scott juu namba 8 awe anacheza Paul na juu yake namba 10 shimoni Bruno kama kawaida mwisho Cavani upande mmoja Rashford na mwingine Greewood.
 
Imefikia point sasa hawa wachezaji wa team pinzani waende kwa Bruno awape somo la jinsi ya kupiga penati.
Yaani waache kujifunza kw wachezaji wanaoshinda magoli ya video,waende kw huyo mchezaji zwazwa anachojua ni kupga penalt tu.
 
True

Game kibao tu tumezifanya ngumu kwa kucheza kwa mentality ya kujilindalinda zaidi..
 
Martial na Rashid wanatatizo la kushindwa kumanage pressure ya kuhitajika kufunga. badala ya kucheza mpira wanafilia kufunga. ukimuangalia cavan anavyocheza waweza sema hafai kukaa pale mbele, hana haraka, he is enjoying kuwa fit and playing some passing football. when the real chance to score comes he takes it, and scores.
 
England wana watoto walio moto sio poa

SAKA

FODEN

MOUNT

GREENWOOD
Hawa waingereza mwisho miaka 25 tu. Huwa wanaanza moto ila usiwaamini kufika mbali. Sina takwimu za kitafiti kutetea hoja yangu ila sababu kubwa nahisi wanakuzwa mno na vyombo vyao vya habari kuliko uwezo wao halisi.

Kuna kipindi (2008 ~ 2012) walikuwa na Tom Cleverley, Jack Wilshere, Daniel Welbeck, Daniel Sturridge, Theo Walcott, Jack Rodwell, n.k na wote hawa walikuwa wamezaliwa mwaka 1989 ~ 1992 sawa sawa na hawa wa sasa waliozaliwa mwaka 1999 ~ 2002. Ila sasa hivi wapo vitimu vidogo hata namba hawana.
 
Basi mwambie tu atoe Hilo goli la penati iwe 1:2
 
Hata mm nikipewa kikosi nitakipanga hivi, kila siku nmekuwa nikiwaambia watu hivi hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…