Chifu, kama wewe ni mfuasi wa soka..huwezi kuja na kauli kama hiyo...
Siyo jambo rahisi kwa timu kupata meneja mpya na benchi la ufundi jipya, halafu timu iperform vilevile kama ilivyocheza kipindi cha nyuma...hilo jambo siyo rahisi hata kidogo...
David anahitaji muda...wachezaji wanahitaji muda wa kuweza kuelewa mfumo mpya wa David na benchi lake la ufundi....
Hutakuwa humtendei haki kocha, kwa kumwona hafai baada ya games 8 za ligi na 2 za UCL....
Ni sawa kabisa kujisikia hivyo, pengine kutokana na kuzoea kucheka kila mara...lakini ukumbuke katika soka kuna kucheka, kulia na kutabasamu...sasa fahamu sasa timu inapita katika kipindi kigumu...kipindi ambacho shabiki wa kweli ni budi kuwa sambamba na timu na benchi zima la ufundi....
Man United ni timu kubwa...hiki ni kipindi cha mpito...ambacho kinaweza kuwa hata mwaka 1 ama miaka 2..lakini timu itatulia na kurudi katika fomu yake...
Unakumbuka msimu ambao United haikushinda hata kombe moja chini ya SAF?