Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Furgusson hakuwa na timu nzuri kama hii lakini alikuwa akibeba makombe
Zama zimebadilika..Fergie kwa recruitment iliyokuwa inafanyika kipindi chake cha mwisho angekula spana mpaka akubali mwenyewe.

Sema good thing ni kwamba Babu asingekubali upuuzi wa kina Martial na wapuuzi wenzake..that's a thing for sure
 
Safi sana Pep.
 
Mkuu unatakiwa ufikirie kwa kina.


Ole kucheza Jana na Double six hasa wakiwa defensive iliisaidia sn Utd na kuifanya utd kuwa salama na kina Maguire Ku relax. Ilikua ni good approach ambayo sote tunapaswa kumsifu Ole kwa hilo. Maana approach hiyo iliwapa nafasi kina James, Greenwood, Bruno na Rashford Ku press so high kitu ambacho kiliivuruga kabisa Chelsea na kuondoa passing accuracy na ujasiri na kuwapa shida kwa karibu kipindi chote cha kwanza. Kwahiyo Ole alikua sahihi kabisa kufanya na kwa approach hii ata Man City mnaweza kumfunga. Najua kila game ina plan yake na approach kulingana na aina ya uchezaji wa timu lkn isifike mahala tukamuona Ole kwa kufanya hivi anaharibu timu.


Yaani huweza kucheza na Chelsea kwa sasa yenye wastani wa possession wa asilimia 69 kwa game 8 uwawekee single six.... Utayumba sn
 
Ole ni mwalimu mzuri ameweza Ku expose weakness za Chelsea na Tuchel. Tumpe heshima yake ktk hilo. Amekuja darajani na approach na Tactics ambazo zimefanya kz na Chelsea had to suffer the whole first half. Ktk game 9 alizocheza Tuchel hajakutana na kikwazo kigumu km jana. Yaani ata Spurs na Mourinho walishindwa na ata ATM na Simeon walishidwa lkn Ole kafanikiwa sn. Tumpe heshima yake
 
Angekua Antony Taylor au yule mpuuzi alotishiwa maisha Mike dean hii game mngeshinda. Wao ndio hua hawaoni haya kuonesha mahaba ya waziwazi kwenu.

Chri Cavanagh was fair mno.
 
Bruno Fernandes' game by numbers against Chelsea:

20 x possession lost (most)
4 x dribbled past (joint-most)
1 chance created
0 shots on target
0 take-ons completed
Bruno Fernandez alikuwa targeted na wachezaji wawili wa chelsea Kante na Kovacic asingeweza kufanya vizuri katika mazingira kama hayo hasa ukizingatia Fred na Scot siyo midfielder wenye uwezo mkubwa wa kuposses mpira.
 
Bruno Fernandez alikuwa targeted na wachezaji wawili wa chelsea Kante na Kovacic asingeweza kufanya vizuri katika mazingira kama hayo hasa ukizingatia Fred na Scot siyo midfielder wenye uwezo mkubwa wa kuposses mpira.
Kante na Kovacic hawakua wanamlenga Bruno.

Ole alimuweka Bruno hapo juu acheze nyuma ya Rashford ili kuwavuruga Kante na Kovacic ambao Mara nyingi mashambulizi ya Chelsea huanzia kwao. Na Bruno alifanikiwa hilo hadi hao viungo wakawa wanapoteza pasi.


Na Fred na McTomnay hawa walichezaja chini kutibua mipango ya kina Meson Mount na Zyench au Odoi. Na mipira yote iliyokua inaelekea kwa Mount au Zyench hawa kina Fred waliidhibiti na kuipush Chelsea nyuma kabisa.


Kwahiyo wachezaji wa UTD walifanya kile ambacho Ole alikua kawaelekeza
 
Zama zimebadilika..Fergie kwa recruitment iliyokuwa inafanyika kipindi chake cha mwisho angekula spana mpaka akubali mwenyewe.
hahahahaaaaaaaa sema jamaaa alikuwa ni nunda (mbishi).
fergie ukimungusha msimu mmoja atainuka tena unaofuata au utakaofuata.

huyu wa kwetu anaingia msimu wa tatu huu na ameshaachwa kwa alama 13, dalili ya kuinuka anatupa kwa muda then anarudi tena nyuma.

mzee wa the boys
next match:
crystal palace = walitufunga mechi ya kwanza
man city.

halafu mbona tunacheza mechi 3 mfululizo ugenini, au hii ratiba niliyoangalia ina makosa
 
Lakini uliona jinsi Bruno kila akipata mpira hao kina Kovacic walikuwa wanakifanya ?

Nafikri Ole anatakiwa kusajili Central Midfielder mzuri zaidi ili kuwezesha timu iwe na ball retention nzuri.

Lakini pia apunguze uoga hao kina Fred na Scot wawe wana advance juu zaidi au mmojawapo kuipa balance attacking yetu.

Siyo kila wanapobanwa washambuliaji wetu warudishe mpira beyond
 
Kuna vichezaji flani flani tunavyo pale man u vinakera sn, mwanzo alikuwa Fellaini na Lingard now vimebaki hivi viwili na sidhani kama vitaondolewa labda tubadili kocha.
Izi mechi za kamkumbe kamkumbe pogba ndio pengo lake laonekana pale.....
 
Kocha siye aliyekuwa akifanya usajili. Yeye aliagiza supu ya kuku kaletewa ya samaki. Usajili wa Fred ungefanywa vema lisingeendelea kuwepo pengo lililopelekea Man kumsajili Fernandes.
Fred
mourinho hakuwahi kumuhitaji fred
point yangu ni kuw pep guardiola nd alimtaka fred ila morinho alifanya mbinu ili amuharibie mwenzie sio kwamba alimuhitaji kwa matumizi yake. Kma alivofanya kwa sanchez maan cty nd walikuwa na nafasi kubwa na ilidhihirika maan tunmjua sanchez timu alizocheza morinho asingeiweza falsafa yao. ko point yangu kama pep alimtaka fred kwahyo usidhani wachezaji wa cty kwamba wa ajabu sana ila wana kocha bor.
 
Zama zimebadilika..Fergie kwa recruitment iliyokuwa inafanyika kipindi chake cha mwisho angekula spana mpaka akubali mwenyewe.

Sema good thing ni kwamba Babu asingekubali upuuzi wa kina Martial na wapuuzi wenzake..that's a thing for sure
Usijidanganye ndugu fergie alikuwa anaweza kushindana na timu yoyote ile hadi sasa. Em fikiria alichoamua kufanya mwishoni aliwamotivate tom cleverly na carrick kujiona Xavi na Iniesta halafu akawa mbele ana magame changer rooney na mwenzie Van Persie. Sometimes huhitaji kikosi kikubwa sana kushinda mataji. unatak kunambia henderson na wijnadium wana maajabu gani sana mpaka wakabeba kwa gap la rekodi. Klop ananikumbusha sana fergie times motivate wachezaji wa kawaida kucheza role flani halafu sajili magame changer then boom.
 
Bado hajafukuzwa tu...
ana mkataba wa miaka 2.
kuwa mvumilivu, tupo kwenye muelekeo bora.
dirisha lijalo tutasajili wachezaji watatu wenye ubora then tunakuwa tittle contender
  1. no striker, cavan anapewa mkataba mwengine
  2. jack grealish
  3. sancho
  4. beki wa kati mwenye umri mdogo, Ole hayupo tayari kumuacha lindelof na maguire
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…