Tukiondoa dhana ya ushabiki,game kati ya man utd na Liverpool ni moja kati ya game ngumu ambazo huwa nazishuhudia msimu hadi msimu. Pamoja na kupoteza form yao,bado wale wajinga Liverpool wanatishia kutawala mechi,kushinda mechi na kuchukua ndoo kabisa. Na kusema kweli hili la mwisho linanikera zaidi,i heri pep atusaidie msimu huu
Liverpool alikuwa ana performance 150% wakati united tukiwa na 70%,hivyo kushuka kwa Liverpool wamerudi 90-95% wakati man utd wamepanda form kufikia 80-90% ya form yao. Kimsingi uchezaji wa Liverpool umebaki ule ule kasoro ni kukosa target nyingi kama ilivyokuwa msimu jana.
Tatizo kubwa la man utd ni kukosa muunganiko mzuri kitimu matokeo yake tunategemea Bruno ameamka na kiwango gani siku hiyo. Yaani kiurahisi tu ni kwamba united bado ni timu ya kutegemea baadhi ya wachezaji wako form timu ifanye vizuri au sivyo tunapoteana. Kwa Liverpool mfumo ndio unacheza.
Pamoja na hayo yote,Liverpool wamekuwa wanaelewa roho wanayoingia nayo vijana wa united hivyo na kwao wanahisi sio game rahisi kama kucheza na arsenal na Chelsea.
United tuna nafasi yetu kushinda hii game ikiwa tukiwa wazuri kuanzia kwenye kiungo cha juu na Marcus akiacha uchoyo wake. Kitakacho tofautisha matokeo ni ubora wa Bruno na thiago kwenye eneo la kiungo.
Come on red devils
GGMU