Ole alipewa kazi ya kuirudisha identity ya United.
Inabidi tuifahamu identity ya United kwanza. Iliasisiwa lini na nani?
Halafu tuangalie kama anachofanya Ole ni kurudisha identity ya United.
Swali zuri mkuu nitajaribu kuangalia mambo machache ambayo kwangu ni positive.
1. Kujenga timu ambayo ipo tayari kuitumikia jezi na sio mahala pa kustaafia.
Angalia Man U miaka nenda miaka rudi hatusifiki kwa kusajili masuper star, bali wachezaji wanaojitolea muda wote, niliandika humu jukwaani mwaka ama miaka 2 iliopita, Man U ilikuwa inashika nafasi ya pili kutoka mwisho kwa kukimbia uwanjani, wachezaji wengi waliridhika na walikuwa hawajitumi.
Je tuangalie Kikosi chetu sasa hivi, timu gani inaweza kusema inakimbia kuliko sisi? Tuna wachezaji wengi wanakaba mpaka kivuli, kuna Fred, Mc tominay, Bissaka, james, lindelof etc. Tumecheza Na Rb leipzig na falsafa zao za ku press, matokeo yake tuliwa overun kwenye mchezo wao wenyewe.
Usajili wetu toka Ole aje umezingatia Pia Hili, so far hakuna mchezaji hata mmoja unaesema ameflop, wengi wameleta Instant impact kuanzia James, Maguire, Bissaka, Bruno, VDB, Telles, Cavani etc. Yote hii ni kutafuta Wachezaji wanaotaka Kuchezea timu badala ya kuangalia majina.
2. Kupromote vijana.
So far tuna academy players wengi tu kikosi chetu, na vijana wengine wanapewa nafasi, tunamuona Tuanzebe, Greenwood, Williams, Rashford na wengine wengi toka academy wakipewa Nafasi, na Highlight kubwa msimu huu ni mechi vs Psg ambayo tulikuwa na Majeruhi wengi na kikosi kujaa Academy players, Tuanzebe vs Neymar na Mbape, Rashford goli la ushindi, Pogba pasi ya ushindi, mc tominay akidominate kati etc.
3. Kupunguza mishahara mikubwa
Wachezaji wengi waliosajiliwa kipindi cha Ole wana mishahara ya kawaida. Bruno na Vdb rumors wanapata 100k per week, maguire around 180k, bissaka around 50 to 70k etc. Wachezaji wakisajiliwa mishahara midogo, wataongezewa kutokana na perfomance zao, leo hii hata Bruno akiongezewa Mkataba na kupewa mshahara mzuri hata sisi mashabiki hatutapiga kelele. Hii issue ilianza toka Woodward ateuliwe ambaye alikuwa akijimwambafy na Hela, sasa hivi tenure ya Ole tunaanza kuziba mashimo.
4.discipline na Dressing room
Sasa hivi timu yote ni kitu kimoja, wachezaji wana furaha, hakuna Hata mchezaji mmoja ambaye unaweza ukasema yupo juu ya wengine, yoyote anaweza kaa benchi, yoyote anaweza kuanza.
5. Depth
Japo bado tuna tatizo la winga ya kulia, ila tume improve sana kwenye depth, leo hii pogba, shaw, matic na wengineo wanaweza kuwa nje ya timu lakini usione pengo, Telles anacheza as if yeye ndio chaguo la kwanza, Tunaona VDB akicheza vizuri kuziba nafasi ya Bruno ama Pogba, Bailly na Tuanzebe katikati, tuna makipa kama watatu wa ukweli, midfield wa kutosha etc. Depth ilikuwa identity yetu kubwa Chini ya fergie.
Na nyengine ya Moja moto moja Baridi, Timu pinzani zimeanza kusema tunabebwa, sijazisikia hizi kauli toka Fergie astaafu, hii ni dalili nzuri tunarudi top.