Mimi binafsi Fred asingekuwa na kadi ya njano hakupaswa kutoka, ila nilisapoti kutoka sababu ya muda wowote angeweza kula umeme (Mike Dean sio mtu mzuri)
Kwenye sub ya Fred kutoka na Cavani kuingia pia ni wazo uzuri ukizingatia tulikuwa tunahitaji goli shida inakuja kwa Ole anapokutana na timu kubwa kipaumbele chake cha kwanza angalau apate hata point 1
Pogba alichoka, huwa yupo reckless sana kwenye ukabaji especially maeneo kama ndani ya 18. Bruno pia alichoka, lakini uzuri wa Bruno anaweza kuwa off dakika 85, lakini dakika 5 akafanya jambo
Watu wataendelea kumponda Ole sababu ya makosa kama haya
Ninahisi Pogba asingesababisha penati, Ole angemtoa yeye. Ila kumtoa baada ya tuta ungeweza kuonekana anamtoa sababu ya kutoa boko. Kiujumla Pogba ilibidi atolewe kabla hata ya tuta, maana alionesha kuchoka mapema tu