Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hawa ni wazee wa mechi kubwa kubwa za UEFA. Hizi zingine wanakamilisha tu. Mambo yao ni ya juu!
 
Ole bhana

Pogba amechoka naongea na jamaa pembeni, nasema Pogba atolewe... mara paap TUTA (msimu huu Pogba anasababisha TUTA mara ya pili kizembe tu)

Halafu anakuja kumtoa Bruno (ambaye muda wowote anasababisha kitu) na kumwacha Pogba ambaye ana ball dance nyingi kuliko kufanya kitu uwanjani
Kwanza alipaswa amtoe Fred aingie Cavani ili Rashford ahamie kushoto.

Substitution hii ingefanya kazi kwa ufanisi kuliko kumtoa Fred na kuleta Matic kisha Greenwood over Cavani
 
Kwanza alipaswa amtoe Fred aingie Cavani ili Rashford ahamie kushoto.

Substitution hii ingefanya kazi kwa ufanisi kuliko kumtoa Fred na kuleta Matic kisha Greenwood over Cavani
Alichokosea tangu mwanzo ni kumuweka pogba kama winga,kingine kumtoa fred ilikua sahihi maana alikua na yellow tayar so mda wowote angeifanya team tubaki8
 
Huyu kocha kwakweli mm sina imani nae kabisa ni mbahatishaji mno hamna kocha humu, yn ana uwezo mdogo sana kwakweli, badala atoe pogba aingize Donny anatoa Bruno badala atoe Rashford aingize Cavani anatoa Greenwood, hzo ni sub nyepesi kabisa hata mm nmeziona kadri mchezo ulivyokuwa unaendelea.

So mm kuanzia leo sina imani kabisa cz nshamuona ana bahatisha tuu na hatutafika popote na kocha huyu, hayo ni mawazo yangu cwezi kumlazimisha mtu kuamini ninachoamini mm japo Ole atabaki kuwa legend ila kwenye ukocha HAPANA.
 
Ukiskia walivyokuwa wanajisifia bada ya kufunga kibonde wa ujeruman
Yalimpiga mvimba macho Leipzig yakaona yana timu
Yes link up play haikuwepo kabisa.

Cavani bado hajazoeana na wenzake naona uchezaji wake ni kama anakimbia kimbia tu uwanjani.
Pogba hakuwa na VPN
Kama alikunayo basi ilisoma Thailand😂😂😂😂
 
Alichokosea tangu mwanzo ni kumuweka pogba kama winga,kingine kumtoa fred ilikua sahihi maana alikua na yellow tayar so mda wowote angeifanya team tubaki8
Yes alipaswa amtoe Fred kisha aingie Cavani ili Pogba arudi kwenye central Midfield.

Option Nyingine angemtoa Fred akaingia Daniel James kushoto kulikuwa kama hakuna mtu anayecheza kungepunguza wachezaji wa Arsenal centre na Bellerin asingekuwa anapanda tena.

Anyway tumepoteza game tujipange upya
 
Mimi binafsi Fred asingekuwa na kadi ya njano hakupaswa kutoka, ila nilisapoti kutoka sababu ya muda wowote angeweza kula umeme (Mike Dean sio mtu mzuri)

Kwenye sub ya Fred kutoka na Cavani kuingia pia ni wazo uzuri ukizingatia tulikuwa tunahitaji goli shida inakuja kwa Ole anapokutana na timu kubwa kipaumbele chake cha kwanza angalau apate hata point 1

Pogba alichoka, huwa yupo reckless sana kwenye ukabaji especially maeneo kama ndani ya 18. Bruno pia alichoka, lakini uzuri wa Bruno anaweza kuwa off dakika 85, lakini dakika 5 akafanya jambo

Watu wataendelea kumponda Ole sababu ya makosa kama haya

Ninahisi Pogba asingesababisha penati, Ole angemtoa yeye. Ila kumtoa baada ya tuta ungeweza kuonekana anamtoa sababu ya kutoa boko. Kiujumla Pogba ilibidi atolewe kabla hata ya tuta, maana alionesha kuchoka mapema tu
Kwanza alipaswa amtoe Fred aingie Cavani ili Rashford ahamie kushoto.

Substitution hii ingefanya kazi kwa ufanisi kuliko kumtoa Fred na kuleta Matic kisha Greenwood over Cavani
 
inakera sana kufungwa na timu ndogo kama arsenal tatizo la leo ni pogba na kocha hivi cavani tulimchukua wa nini kama hatuwezi kumuanzisha?pogba kachemka sana leo lakini kocha hakumtoa angefanya maamuzi mapema wala asingeleta upuuzi aliofannya tumefungwa sababu ya kocha
Ukiachana na faulo iliyosababisha goli Pogba hakuwa mbaya kivile, kwa nini tusimzungumzie akina Fernandez waliokuwa wanazunguka tu uwanjani?
 
Na mimi baada ya kuchunguza mwenendo wa team mechi kadhaa naungana na wale wasiokuwa na imani na kocha Olegunar.

Huyu mzee ni mbahatishaji tu, leo tumepoteza kijinga sababu ya selection yake kumpanga pogba pembeni. Full backs za arsenal zilikuwa free sana hasa first half.
Wakuu Bavaria ,The best 007 . Naungana nanyi.
 
Back
Top Bottom