Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ole mjanja sana kinachosikitisha siku tukiwa tumefungwa game inaelekea mwisho ndo unaona anamuinua VDB....sasa sijui hapo anamtengenezea confidence au ndo anaiua kabisa
Hii Midfield mnataka nani aanze na nani akae benchi ?
1.Bruno Fernandez
2.Paul Pogba
3.Donny Van De Beek

Kwa vyovyote iwavyo hawa watu hawawezi kuanza pamoja katika mechi moja labda kwa kulazimisha sana.

Tusiwe kama mashabiki ya Chelsea na Arsenal ambayo kila siku yanalaumu starting x ya Mwalimu.

Mimi ni kati ya watu ambao kabla hata Bruno hajasajiliwa nilitaka Donny asajiliwe but with midfield depth tuliyonayo ni ngumu kuwatumia wote mechi moja.

Man city kwenye midfield last season au hata msimu waliotwaa ubingwa walikuwa na
1. David Silva
2. Bernardo Silva
3. Ikay Gundogan
4. Fabian Delphi
5. Kelvin De Bruyne

Lakini hakuna hata mmoja aliyewahi kulalamika juu ya kukaa benchi kwa hao leo Donny kakaa benchi tuko mechi ya tano tu ya ligi tunaanza kupiga kelele ?

Mbona hatulalamiki Pogba kuanzia benchi kumpisha Juan Mata ?
 
DVB KUKAA BENCHI, SHIDA IKO WAPI?




ILIANZIA kwa Paul Pogba. Walau yeye alikuwa anajua kipindi benchi lilipomhusu huko Old Trafford.
Hata wikiendi iliyopita alipoanzia benchi dhidi ya Chelsea wapo walioshangaa na wapo ambao hawakushangazwa.
Kinachoshangaza ni Donny van de Beek. Kuna shida gani? Bila shaka, hata yeye mwenyewe atakuwa anakuna kichwa kutafuta namna gani ya kufanya ili kuanza kupata nafasi ya kucheza kwenye timu.
Ole Gunnar Solskjaer alimfanyia ngumu Pogba kumfanya acheze kwenye kiwango bora. Alimwaanzishia benchi kwenye mechi nne mfululizo akiwa na maana ya kumtia hasira ili atakapopata nafasi aonyeshe uwepo wake uwanjani.
Jumamosi iliyopita Pogba na Van de Beek, wote walianzia benchi. Kitu kilichowashangaza zaidi ni kuona Solskjaer amemwaanzisha Daniel James. Kwenye mchezo ambao ulitarajia Man United kuwa na huduma bora ya wachezaji wake bora ndani ya uwanja ili kuwadhibiti Chelsea walionekana kwenda Old Trafford kutafuta sare, bado Solskjaer alichaguo kuwaweka nje wachezaji hao wawili.

Heri kwake Pogba yanaweza kuwa ni maisha ya kawaida. Kwa Van de Beek mambo yanaweza kuwa magumu. Kucheza dakika 61 kwenye Ligi Kuu England hadi sasa kwa timu hiyo alijiunga nayo kwa mapenzi makubwa, akiondoka Ajax alikokuwa nyota mwenye hadhi yake, inaibua mashaka na maswali mengi.
Katika mechi ambayo wengi walitamani kuona kitu gani Van De Beek atafanya kwa kukabiliana na timu ngumu kwenye ligi, Solskjaer aliamua kuanza na Juan Mata na Scott McTominay.
Na hata Mata alipoonekana kuchoka, Pogba ndiye aliyeingia na kumwaacha Van de Beek kwenye benchi akiwa mpweke. Solskjaer alimwambia Van De Beek kwamba nyakati zake zitakuja, lakini si kwa ushawishi wa kumtumia kwenye mechi za Kombe la Ligi tu.
Advertisement
Mbaya zaidi, wakati akiwa kama yatima jukwaani, timu yake ya zamani inacheza mechi na kushinda 13-0.
Bila ya shaka, si muda mrefu atayaona maisha ya Old Trafford machungu na kujilaumu kutua kwenye timu hiyo.
Patrice Evra hivi karibuni amehoji. Van De Beek alisajiliwa wa kazi gani? Kwa maana timu inacheza, inashindwa kufanya vizuri huku mchezaji huyo akiwekwa tu benchi na wakati mwingine anapewa dakika nne za kucheza.
Solskjaer kama hakuwa na ufahamu atamtumiaje Van De Beek asingefanya usajili wake.
Staa huyo ni muhimu kwa taifa lake na bado mchanga, hivyo anahitaji kujenga kisaikolojia kwa kuaminiwa na kupewa mechi kuliko kumvuruga akiwa kwenye umri mdogo huo. Ukizingatia hata pesa iliyotumika kunasa saini yake si ndogo.
Solskjaer hawaoni makocha wenzake Frank Lampard na Mikel Arteta. Hata Pep Guardiola na Jose Mourinho.
Wamekuwa wakitoa nafasi kwa wachezaji wao wapya kucheza. Sasa hii leo utawezaje kukosoa kiwango cha Van De Beek kwenye ligi kama kuchezeshwi? Solskjaer awaambia mashabiki wa Man United, nini shida ya Van de Beek.
Man United imekusanya pointi saba tu kwenye mechi tano ilizocheza kwenye ligi hadi sasa, imeshinda mbili, sare moja na vichapo viwili. Mashabiki wanahitaji kuona wachezaji wao wote mahiri wakipewa nafasi ya kucheza ili hata kama watashindwa kupata matokeo mazuri isiwe lawama za nani kacheza na nani hakucheza. Solskjaer hapaswi kukiharibu hiki kipaji cha Van De Beek ambacho dunia itapenda kukiona kwa miaka mingi ijayo.
 
Ferran Torres hajaanza hata mechi moja.

Hakim Ziyech hahaanza hata mechi moja

Why kwa Donny iibue kelele?
 
Watu wanaongea Sana khs VDB,,,,
The kid is very talented, Hakuna ubishi khs hilo, ana touches flan ambazo Ni htr kwa lango la adui , na wastan wake wa assist Ni mzuri !!!
Binafsi napenda apate more minutes,,,

Tukumbuke it's just beginning, tuna mechi nyingi za ligi, FA, Carabao na UEFA!
Atacheza tu !!!

Kuimanage club Kama MU fc Ni presha kubwa, mda wote wamiliki na fans wanataka matokeo chanya, kinyume chake watahoji Sana , ndio hoja za baadhi ya wachezaji kwa nn hawatumiki !!!!

We believe in Ole,,,, ! Tumpe muda wakuu

#GGM
 
Ukilalamikia kwanini VDB hachezi una matatizo kidogo...
Ligi imechezwa mechi ngapi?
Ana uzoefu na ligi kiasi gani?(Inatakiwa azoee taratibu)
Alisajiliwa wa kazi gani? ( Uliwahi jiuliza akiumia Bruno nani atacheza?)

Tuache kuwa watu wa lawama jamani
Nashagaa shabiki wa soka jusema kwa nini mchezaji flani aanzi. Hv tunaona Pogba anavyokuwa effective akitokea bench? Mpira ni dk 90+. Anaweza akaanza afu akatoka au akaanzia benchi afu akamalizia

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Mashabiki wa Man Utd inabidi tutambue ya kuwa haiwezekani kucheza zaidi ya players 11 uwanjani. Ligi tumechacgeza match tano tuu tunalalmika VdB hachezi?

Nilichokiona watu wanalalamika kuanza kwa James lakini wanatumia kivuli cha VdB kukosa minutes. Ingekua kaanza let say Rashy kushoto then Cavani upfront watu wasingelalamika VdB kukosa kucheza.

Wazee Ole naye ni binadamu, hawezi kuwa right kila siku na kuturidhisha mashabiki wote.

Kuna ligi, UEFA, Carabao na Fa naamini VdB atacheza tuu.
 
★Haka kajamaa kananiudhi kweli yani nikama Mourinho na Lukaku nilikuwa napata hasira mpaka natoka Jasho★
Ole mjanja sana kinachosikitisha siku tukiwa tumefungwa game inaelekea mwisho ndo unaona anamuinua VDB....sasa sijui hapo anamtengenezea confidence au ndo anaiua kabisa
 
★Sisi tunachotaka ni kila mtu acheze hakuna aliesema kuwa tunataka wacheze wote hapana kwani kubadikishana haiwezekani Mkuu huyu anacheza mechi hii hata akifururiza mechi mbili afu mwingine nae anacheza mechi zijazo mbona simple tu hata hao unao watolea mfano Man city Guardiola alikuwa anafanya hivyo pia★
 
★Mkuu sisi sio Chelsea pia sisi tuna strategies zetu kama timu sasa sizani kama majirani wakifanya fyongo na sisi tunafatisha hapana sisi hatupo hivyo kama wao walimchukua Hakim Ziyech kama Pambo ni swala lao binafsi halituhusu hata kidogo na usitake kutuambia kuwa Ole anafatisha Timu pinzani inachofanya Tumenunua mtu ataftiwe nafasi ajimwaye mwaye tuone fyongo lake.

Wengine wanasema ooh tusimlaumu Ole kwanza ndio Msimu umeanza Tumecheza mechi tano tu kwani tulimchukua ili acheze baada ya mechi 20 au 13 hapana. Kama hapana inamaana hata ile mechi ya kwanza angecheza tu★
Ferran Torres hajaanza hata mechi moja.

Hakim Ziyech hahaanza hata mechi moja

Why kwa Donny iibue kelele?
 
★Me kuhusu Ole kumpa muda hapa UNITED Sipingani na wewe Hata mbuyu ulianza kama mchicha ila swala la huyu dogo (DvB) hata sifikirii kumpa muda kwakweli tumoe muda anamuweka Benchi kama ananiskia tutaelewana vibaya asee
 
★Hata hizo dakika anaingiaga Pogba za mwisho DvB kaingia mala ngapi???★
Nashagaa shabiki wa soka jusema kwa nini mchezaji flani aanzi. Hv tunaona Pogba anavyokuwa effective akitokea bench? Mpira ni dk 90+. Anaweza akaanza afu akatoka au akaanzia benchi afu akamalizia

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
★Lets take a watch kwenye hizo Carabao,FA na CL tusipinge sana swala la kuwa benchi★
 
Nashagaa shabiki wa soka jusema kwa nini mchezaji flani aanzi. Hv tunaona Pogba anavyokuwa effective akitokea bench? Mpira ni dk 90+. Anaweza akaanza afu akatoka au akaanzia benchi afu akamalizia

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
Hatuongelei kuanza au kuingia sub, hapa tunaongelea kwnn juzi hakumchezesha lkn pia kuna katabia anataka kukaanzisha ka kumuingiza vdb dk 4 au 6 kabla ya mpira kuisha, ss km alikuwa co chaguo alimsajili kwa nn? Au ndiyo tuamini wanachosema wadau kwmb management ya man u mbovu na haimpi kocha machaguo yake.
 
★Me kuhusu Ole kumpa muda hapa UNITED Sipingani na wewe Hata mbuyu ulianza kama mchicha ila swala la huyu dogo (DvB) hata sifikirii kumpa muda kwakweli tumoe muda anamuweka Benchi kama ananiskia tutaelewana vibaya asee
Ataadopt mfumo taratibu mkuuu !!! Shaka ondoa ! Hata Telles, Edinson, Facundo hawatapangwa Kama sisi fans tunavyotaka, Kuna mda watakuwa regular, na pia kuna mda wataanzia bench na kuna muda hawatapangwa kabisa !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…