Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Katika hili swala mnakosea mno mnapo generalize kwa sababu hata humu pia wapo watoto na watu wazima baadhi wanabehave kama watoto kwenye majukwaa yetu.
Mashabiki wa Arsenal na chelsea humu JF kama vitoto vya primary school..
 
Sikatai mkuu mfumo huo upo, ila ndio mfumo ambao tunaupigia kelele mwaka wa 7 huu sababu umefeli man Utd. Tunamtumia Mata kama winga wa kulia hivyo timu yetu inakuwa haina Width na tunategemea mashambulizi yatoke kushoto sababu mata sio natural winga na muda mwingi anacheza kati.

DVB tukimchezesha pembeni tutakuwa kama tunajitekenya na kucheka wenyewe hatutasolve jambo lolote na Mistake ile ile toka LVG, Mou hadi Ole itakuwa inaendelea.

Ndio maana unaona Kocha na hata mashabiki wanataka sana Sancho aje Man UTD sababu yeye ndio solution kwa upande wa Kulia.

Ili timu ifanye vizuri inabidi iwe haitabiriki, kulia unatengeneza, kushoto unatengeneza na hata Katikati unatengeneza.

Kabla ya Bruno kuja tulikuwa tu One dimension tunatumia kushoto Rashford na Martial, Akaja Bruno angalau tukaongeza wigo kati tupo vizuri na kushoto vizuri, anatakiwa aje wa kulia Sasa na sio VDB ambaye atatupa wigo mpana tena tuwe timu hatari kutokea upande wowote ule, hapo ndio utaona Man UTD kama ya zamani tuliozoea.

Timu kubwa kama Man utd inacheza mechi 60+ kwa mwaka, wote hao watapata nafasi kucheza mechi 40 na zaidi hata wasipocheza pamoja.
 
Ila mm kwa kweli bado namuota haaland yn ile pesa man u wanayoambiwa walipe kwa Sancho ni bora tulipe kwa haaland, naona kabisa utd tunamhitaji haaland kuliko hata huyo Sancho.
 
Hiyo 45Minutes iko wapi?
Dar-es-salaam mkuu, info zao hizo hapo kwenye screenshot.

Au unaweza kuwacheki Dauda Sport Store (Maduka ya Shaffih Dauda) maduka yao yapo Dar na Dodoma. Utachagua lililo karibu na wewe. Pia maduka yote mikoani wanatuma.

Ila kwa Dauda Sport Store bei ni TZS. 30K
 
Ila mm kwa kweli bado namuota haaland yn ile pesa man u wanayoambiwa walipe kwa Sancho ni bora tulipe kwa haaland, naona kabisa utd tunamhitaji haaland kuliko hata huyo Sancho.
Tunahitaji Winga wa kulia kuliko namba yoyote uwanjani, Haaland hafungi bila kutengenezewa na Haaland hafungi bila kuwa na Mawinga ambao wanatengeneza Nafasi, zile movement pale mbele ambazo watu wanafanya na kuwavuta Mabeki pembeni ndio mianya ambayo wafungaji wazuri wanaitumia kufunga, mfano Mzuri Liverpool.

Unapokuwa na timu isio na movement na kutumia wachezaji wa kawaida pembeni hata striker kwake inakuwa ngumu maana muda wote anakuwa na mtu ana mmark yule striker bila kuogopa wa pembeni.

Pale dortmund hata Batshuayi alionekana mtu sababu ya mifumo kama hii.
 
Modern football imegeuka na kuwa backs 2&3 ndo wapiga hzo krosi.
 
Sawa mkuu,,wacha tuone
 
Modern football imegeuka na kuwa backs 2&3 ndo wapiga hzo krosi.
Hata Sancho sio winga wa kizamani wa kupiga cross, ni inside forward ambaye akipata mpira anaingia ndani. Ni wachezaji wawili tu duniani msimu uliopita ambao wana goli zaidi ya 20 na Assist zaidi ya 20, Messi na Sancho. Hivyo Sancho anaweza kumfanya Wan Bissaka akawa mzuri vile vile kwa run zake compare na Mtu kama Mata Ama Greenwood ambao ni mzigo kwake.
 
TRUE
 
Unachowàambia Man U wenzako ndiyo nilikiandika ila wakaona kwakua mimi nashabikia Arsenal nimekuja kuwavurugia uzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…