Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Team bado sanaa hiiii... Kocha tia Maj tia Maj
 
Avunje kibubu aje Zidane tu
 
Pendekezo lako mbona kama tulisajili msimu uliopita au usajili tuliofanya haujatick ?
 
Kwa sasa n best coach in Europe
Kwahiyo kuna siku na Ole atakuwa best coach in Europe tuwe na subira.

Kwa squad yetu msimu huu Ole kajitahidi sana tena sana

Nafikiri ukiondoa Liverpool team yetu msimu huu inafuatia kwa kufungwa mara chache zaidi.

Tunapaswa tuimarishe striking force na backup players kwenye maeneo muhimu tutafanya vizuri zaidi.
 
Mkuu hiv unajua ole huwa ana bahatisha... yaan hajui afanyalo.. example game ya Chelsea
 
Yani Ed atoe tena hela kwenye hiyo nafasi
, hawezi. Mwaka juzi katoa hela kumnunua Dalot, mwaka jana Bissaka, mwaka huu ataangalia nafasi nyingine

Mwaka jana, wakati wanamchukua walijua AWB ni right back wa aina gani, old school

Kwa msimu huu wa usajili kwa mtazamo wangu, United watafute Striker, Kiungo mshambuliaji, na winger. Ingekuwa timu hazilii njaa na hii Corona tungesema tutafute beki wa kati mwenye pace ili am compliment Maguire. Anyway tunaweza kuendelea kumtazama Tuanzebe

Nafasi nyingine tunayohitaji kusajili ni kipa, au tumrudishe Henderson. De gea amefanya makosa mengi sana, unahitaji kipa asiyefanya makosa au anayefanya makosa machache sana kama unataka ubingwa

Kuna uwezekano Romero akaondoka, ali mind sana juzi kuwekwa benchi, na ana haki zote za ku mind... Inaonesha kocha hamuamini maana mechi za cup competition zote zilikuwa zake

Matokeo ya mbio za top 4 pia yatatoa dira ya wachezaji gani tutakaowasajili. Kesho ni kesho aisee.
Haujatick..tunahitaji RB wa kueleweka
 
Time will tell
naunga mkono usajili wa mkopo ila kumsajili permanent itakuwa ni zaidi ya gamble na sababu kubwa ni hali yake ya kiafya (coman amekuwa na takwimu mbovu za kiafya).

nyuma ya pazia inasemekana bayern munich walikataa mabadilishano ya wachezaji dhidi ya man city kwenye dili la usajili wa leroy sane, hii ni tafsiri tosha ya kwamba bado bayern wanamuhitaji coman kwenye kikosi chao.

sidhani kama watakuwa tayari kutegemea huduma ya leroy sane(anayetoka kwenye injury) na gnabry pekee kwenye harakati zao za kuwania ufalme wa europe msimu ujao., tusisahau ivan perisic ameshakuwa mkongwe kiumri na phelipe coutinho mustakabali wake na bayern ni zero

wanahitaji wawe na squad depth for every position kama tunavyohitaji sisi....

ngoja tuone, pengine huu ni mtego wa kuwafanya dortmund wawe na khofu (jamaa wamekataa kushusha thamani ya jadon sancho)
 
Hata mimi nilishangaa sana Romero kukaa benchi.
 
Yaani nikiona TAA anavyocheza,then nikimcheki Bissaka wetu napata kichefu chefu kabisa..Labda abadilike aisee

Dalot huyo ni wakuuzwa tu,project imefeli hiyo..

Hii Ligi ishakuwa ngumu..inabidi uwe na kikosi chenye uwezo wa juu kila sehemu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…