Kuanzia dk ya 70 S'ton walitukimbiza sana, ule mpira aliocheza Bissaka nilijua lazima utafanya kitu, hii game United walishatoka mchezoni kwa presha ya kuzimiliki points 3 kutubakisha top 4. Mipira mingi iliyokufa huwa ina madhara sana, kwa muda ule kila mchezaji nina hakika aliomba game iishe hata mimi nilibaki nikitetemeka, kabla Bissaka hajafanya maamuzi kuucheza ule mpira niliomba bora upite ilikuwa ni rahisi kuzuia kuliko kona ambayo wachezaji wanajipanga na ukiangalia tayari tulikuwa tuna cha kupoteza hivyo presha ilikuwa kubwa.
Hatimaye kamba, nilitegemea lingetokea hili, maswali ninayojiuliza;
Kwanini refa alipeleka game mpaka 98 wakati ziliongezwa 5, najua kama dk 2 kwenye hizo 5 zilitumika pia mpira ukiwa umesimama ila bado ilipaswa kuisha 95
Kwanini Solskjaer hakufanya sub ya Williams?
Yote kwa yote hii ndiyo sehemu ya mchezo ila kiukweli hatukupaswa kupitia sehemu hii muda huu, naamini hii itawapa nguvu sana wapinzani.