Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Popular opinion....Watu wengi wanaichukia United kwa sababu ya mateso iliyowahi kuwapatia hasa kipindi cha Sir Alex Ferguson. Babu alipostaafu ikawa Neema na ndereko kwa hawa wapinzani. Mara hii kuiona tena United ikiwa na kila dalili za kurejesha zama zake, inawauma sana watu zaidi ya kisu cha ngariba. Tusiwanyanyapae,(hawana Covid-19)...ni ndugu zetu wenye majeraha mengi rohoni, deep down wanatamani lingekuwa chama lao ila ndo hivyo tena.

Manchester United ni zaidi ya FC, ni Imani katika Soccer, ni alama ya Ushujaa na ushindi iliyo kwenye DNA ya wafuasi wake.

Win or lose, we are forever UNITED.
Na tutaingia sokoni kushusha vifaa vikali..This time around watapata tabu kweli kweli
 
Official: Bruno Fernandes is the Premier League Player of the Month for June #mufc
IMG-20200710-WA0057.jpg
 
Soma iyoo mkuu acha uvivu nimekuwekea hapo screen shot 201 meetings u have been defeated 83 times so there u can do a private calculation to know how many games u won and how many games went to draw.
Games played 201.Out of those,Man U won 83,Arsenal X games and neither won nor lose against the other in Y games.
We only have to find out one of the variable(X or Y) in order to clear the air btn us.
Bring it on,I'm eagerly waiting.
 
Games played 201.Out of those,Man U won 83,Arsenal X games and neither won nor lose against the other in Y games.
We only have to find out one of the variable(X or Y) in order to clear the air btn us.
Bring it on,I'm eagerly waiting.
Listen my friend there's no any football club in England which has most defeated Man United.
 
POGBA, UNITED IMEISHA HIYOOOO...


VIJANA wa mjini wanasema imeisha hiyooo. Ndio, kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amefuta mpango wa kuachana na wababe hao wa Old Trafford.
Pogba, ambaye amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu na Real Madrid na Juventus, amefunguka kuwa anataka kuendelea kubaki Old Trafford na kwamba, ubora wa kikosi hicho umekuwa ukimpa mzuka zaidi.
Pia, amesema kutua kwa kiungo Bruno Fernandez kumetoa mchango mkubwa kwenye kikosi cha Kocha Ole Gunnar Solskjaer, na anafurahia kucheza sambamba na Mreno huyo.
Kutokana na hilo, Pogba amesema kwa sasa yupo tayari kuanzisha mazungumzo kwa ajili ya mkataba mpya ili kuendelea kukipiga kwa muda mrefu huko Old Trafford.
Pogba, ambaye mkataba wake wa sasa umebakiza mwaka mmoja kukiwa na kipengele kinachoipa United nafasi ya kumuongezea mwaka mmoja zaidi, huku Solskjaer akifichua juzi kuwa Mfaransa huyo atakuwepo katika kikosi hicho kwa muda mrefu.
Awali, kulikuwa na mvutano mkubwa baina ya mabosi wa Man United na wakala wa Pogba, Mino Raiola ambaye alikaririwa akisema kuwa mteja wake hana furaha na kikosi cha United na anafikiria kumtafutia makazi mapya.
Hata hivyo, imebainika kuwa Pogba aliyenaswa kwa dau la pauni 89 milioni mwaka 2016 anafurahia kucheza sambamba na Bruno ambaye ujio wake umeifanya Man United kuimarika zaidi na kuifanya kupata matokeo mazuri tofauti na mambo yalivyokuwa awali.
Kombinesheni ya Bruno na Pogba imeifanya Man United kuwa moto kwelikweli ikicheza mechi 16 bila kupoteza huku ikipiga soka la kuvutia na kuonyesha mwanga wa kurejea kwa kikosi kama kile cha enzi za Sir Alex Ferguson.
Hata hivyo, Man United watalazimika kumtengea Pogba mshahara wa maana zaidi ya anaolipwa sasa wa Pauni 290,000 kwa wiki na bonasi nyingine kibao.
Tayari Solskjaer amefichua kuwa Nemanja Matic na Scott McTominay wamesaini mikataba mipya ya kuendelea kukipiga Old Trafford.
“Natambua tangu Pogba amerejea baada ya kupona majeraha amekuwa kwenye kiwango bora na atazidi kuwa bora zaidi. Kwa sasa anafurahia kucheza soka la kiwango chake, tutaona atatupeleka wapi wakati huu tukiwa kwenye vita ya kuwania nafasi nne za juu,” alisema Solskjaer.
Wakati Pogba akitoa habari njema kwa mashabiki wa Man United, mabosi wa klabu hiyo wako kwenye harakati ya kuongeza mastaa wapya huku majina ya nahodha wa Aston Villa, Jack Grealish na winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho yakiwa kwenye rada.
 
Marefa including wa VAR wa EPL wanachekesha sana, Jana badala ya Bruno kupewa red card kwa kumchezea vibaya , dangerous foul beki wa Aston Villa eti walipewa penalti. Kuna uhalifu mkubwa sana ndani ya mpira. Man U wameanza kubebwa kama enzi za Fergusson
 
Marefa including wa VAR wa EPL wanachekesha sana, Jana badala ya Bruno kupewa red card kwa kumchezea vibaya , dangerous foul beki wa Aston Villa eti walipewa penalti. Kuna uhalifu mkubwa sana ndani ya mpira. Man U wameanza kubebwa kama enzi za Fergusson
Hii inaonyesha ni hofu inaingia.
 
Yan kushinda mshinde nyie sisi hatujafanya chochote, hata tulipokutana mkajisifu mmetufunga,bado nyie wenyewe mtuletee watukanaji kwenye jukwaa letu?

Tukutane kwenye hiyo mechi yetu. Mtalamba lolo
 
Marefa including wa VAR wa EPL wanachekesha sana, Jana badala ya Bruno kupewa red card kwa kumchezea vibaya , dangerous foul beki wa Aston Villa eti walipewa penalti. Kuna uhalifu mkubwa sana ndani ya mpira. Man U wameanza kubebwa kama enzi za Fergusson
Unachekesha km Morinyo
 
Back
Top Bottom