Manchester United (Red Devils) | Special Thread

@Chusa utamsikia akisema"Hii ndo timu yetu,huyu ndo kocha wetu na hawa ndo wachezaji wetu"..Hahaha
 
Ushaanza kumpamba sasa OGS Bado ana muda wakujipanga Kurejesha Furaha ilopotea pale OT katuangusha Mechi ngapi mpaka unaanza kumpa sifa kama hizo.
mechi 10 zilizopita OLE na benchi lake la ufundi wamejirekebisha sana kutokana na makosa waliokuwa wakiyafanya mara kwa mara hususani kwenye mechi ndogo.

wakati ligi kuu ya uingereza inaanza (mechi dhidi ya chelsea) eneo la kiungo alikuwepo nemanja matic pamoja na juan mata lakini hao wote walianzia benchi ili kutoa nafasi kwa mmoja wao (kati ya jesse lingard au andreas perreira)

mechi nne za mwanzo Ole alikuwa analazimisha paul pogba acheze chini (namba 8) zaidi pamoja na scott mctominay nafasi ambayo ulikuwepo uwezekano wa kumtumia nemanja matic then paul pogba acheze namba 10 au juan mata, kinyume chake alikuwa anamtumia andreas perreira au jesse lingard.

baadae paul pogba akapata majeruhi, kuumia kwa pogba pia ndio ulikuwa mwanzo wa fred kurudi kwenye kikosi baada ya harusi na ishu nyenginezo (match fitness) na ilikuwa ni mechi ya 5 kama nitakuwa nipo sahihi, cha ajabu ole akaendeleza tabia ile ile ya kumbeba perreira na lingard na hatimaye fred akaendelea kukaa benchi.

mechi ya arsenal paul pogba akarudi tena kwenye kikosi cha kwanza baada ya kupona majeruhi, OLE na benchi lake la ufundi wakaendelea kulazimisha jesse lingard na andreas wawemo kwenye kikosi cha kwanza huku benchi letu wakiwepo juan mata, fred na nemanja matic ambao hao wote wana ubora mkubwa kuliko wawili hao





mechi iliofuata tunapoteza dhidi ya newcastle united na kwa mara nyengine tena andres perreira anacheza mbele ya nemanja matic, kwa ufupi mpaka tunafika mwezi oktoba hakuna hata mechi moja ambayo OLE na benchi lake la ufundi waliacha kuwatumia andreas perreira au jesse lingard kwenye kikosi cha kwanza, baadae matic na paul pogba wakapata injury.

nilichojifunza ni kwamba tokea mwanzo (dirisha kubwa la usajili) bwana ole alishaweka akili yake kwa wachezaji wawili (andreas perreira na jesse lingard) waongoze jahazi la kiungo mshambuliaji ndio maana paul pogba akashushwa chini zaidi, ila baada ya kuona wachezaji hao wameshindwa kufikia matarajio makubwa aliyoyaweka kupitia wachezaji hao na paul pogba kuendelea kuwa majeruhi ndipo alipoamua dirisha dogo la usajili amrudie bruno fernandez.

sasa jiulize tokea bruno fernandez asajiliwe hao wahuni wawili wameanza mechi ngapi?
bado naamini zile mechi tulizopoteza point kizembe dhidi ya timu ndogo kama tungelianza na midfield ya pogba, mata, scott na matic/ fred tungelipata ushindi.
 
Hivi ikitokea hadi Aprili 03 maambukizi yakawa bado hayajadhibitiwa kwa kiasi cha kutosha,kuna uwezekano ligi ikaahirishwa?
Na je ikiahirishwa mshindi au anayeshuka daraja watampata kwa vigezo gani?
Tukijiuliza maswali mengi tunaweza kuwa vichaa..

ushajiuliza corona ikiendelea hivi hivi bila kukoma itakuwaje kwenye mambo mengine??..achana na soka,kwenye maisha ya kawaida
 
Tukijiuliza maswali mengi tunaweza kuwa vichaa..

ushajiuliza corona ikiendelea hivi hivi bila kukoma itakuwaje kwenye mambo mengine??..achana na soka,kwenye maisha ya kawaida
Niliulizia soka sababu hapa ndio mahala sahihi pa kuongelea soka...kuna uzi wa FRANC THE GREAT pamoja na nyuzi kibao zinaongelea athari za corona kwenye kila nyanja.
Asante kwa jibu lako mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…