Manchester United (Red Devils) | Special Thread

TUWAZOMEE:WOOOHHHH
TUWACHEKEE:
HAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHA
 
Ole anastahili lawama kubwa.

Mosi anaridhika na kikosi chake wakati ni wazi tunahitaji 3 classic players.

Pili Jose asingekubali huu upuuzi wa kumtetea CEO kwa uzembe na angesema hadharani.

Tatu RW ni tatizo la muda mrefu sana sijui kwanini tangu Moyes hadi sasa bado tuna sua sua

Nne Ilikuwa ni ujinga wa kiwango cha SGR kubadili kocha kila mara.Matokeo yake kila tukibadili kocha tunaanza upya kuanzia mfumo na aina ya wachezaji kwaajili ya mfumo mpya.

Tano Pogba ni mchezaji mzuri sana lakini kama anataka kuondoka nadhani ni vyema akaachiwa aondoke mapema.Sioni mantiki ya kuendelea na Pogba wakati wapo wachezaji wengine wengi tungeweza kuwa nunua kwa fedha za mauzo yake.

Mwisho nadhani tuendelee na hii project ya Ole labda tunaweza kufurukuta mwakani hasa tukizingatia aina ya wachezaji alionunua wote wako vizuri pia kiwango cha Fred kimepanda kipindi chake.

Tusikate tamaa msimu huu ni Liverpool hilo halina mjadala tena.

Mashabiki kindaki ndaki wa Man tuendelee ku support team yetu.
 
Hivi kwa Manchester United hii tulitegemea kupata matokeo kwa Liverpool au ndio mpira unadunda ehh
Ni Chelsea tu ndio amekubali kuwa kibonde wetu.

Ni ajabu kwa timu mbovu kama hii ya Ole tangu dirisha limefunguliwa hadi sasa haijanunua mchezaji wa maana halafu unamsikia Ole akijipa matumaini naye ataijenga MUFC kama Klopp alivyoijenga LiVAR.

Timu haina DM na wala husikii ikitafuta DM wa maana, timu tajiri inahesabia pesa mfukoni. Liver na ubora wake wote baada ya dirisha kufunguliwa tu wamevuta chombo,MUFC yangu ipo ipo tu.😂😂
 
Kwa hiyo Mkuu tusisajili striker mpaka tutakaposajili wing back wazuri, mpaka tutakaposajili viungo wachezeshaji wazuri
hapo inategemea kipaombele cha mwalimu husika, dirisha lililopita mwalimu aliamua kuingia sokoni kwa lengo la kuimarisha safu ya ulinzi na alitumia takribani paundi millioni 130 kwa wachezaji wawili (wan bissaka na maguire), kwake aliamini eneo linalotusumbua zaidi ni ulinzi huku akijibebesha matumani viungo wake (pogba, perreira, lingard, fred) watazidi kuimarika

ukiniuliza mimi kipaombele changu cha kwanza itakuwa ni viungo wachezeshaji japo wawili pamoja na winga, kiupande wangu naliona tatizo kwenye maeneo hayo

nikikuuliza wewe huenda kipaombele chako utaniambia tatizo letu kubwa tunalopaswa kulitatua ni striker mfano wa haaland ndipo tuangalie nafasi nyenginezo.

mwenye maamuzi ya mwisho anabaki kuwa ni mwalimu husika na ndiye anayefahamu hali ya kifedha iliopo klabuni.

huwezi jua pengine ole alimuhitaji haaland na hata bruno fernandez lakini tatizo ni hela.
 
Funy, jamaa wanafurahia kuifunga one of the weakest Man Utd in many years.... The weakest team without their 3 best players

Funny Klop aliponda Man Utd ku defend deep na kufanya counter attack, kitu alichofanya yeye hususani kwenye goli la pili

Funny Klop aliwahi kusema itakapofika wakati anatakiwa kununua mchezaji kwa pound milioni 70,80.....100 ataachana na soka kabisa (wakati Pogba amenunukiwa), Baada ya mwaka akamnunua VVD, beki kwa kiasi cha kuvunja rekodi

Maisha bila unafiki yanawezekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeacha kuishabikia Arsenal kwa hiyari yangu mwenyewe, naenda kula maisha Manyumbu huko
 
De gea alkua na mzuka wa ajabu sana,asingetoka langoni ile counter ilkua offside.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu kuna watu wanaona sawa hata tusipopata striker

Sent using Jamii Forums mobile app

Sijawahi kuwa na imani na martial mzembe sana halafu timu inashida sana eneo kiungo naonaga makocha wengi huwa wanaanza kujenga kiungo na mabek hii timu na uongozi sijui wanawaza nini yaani lingard na perreira wanaweza kuwa wabunifu wetu?
 
Duuuu! Hii kauli ya kishujaa sana
It true hii looserpool ya kawaida mno, huwezi ifananisha na Great Manchester United ya Sir Alex, jinsi Manchester ilivyo mbovu ilipaswa looserpool washinde goli hata 8 - 0
Yaani hata Sir Alex uko alipo anashangaa kwann looserpool wanaongoza ligi? Nafikiri mwisho wa dunia umekaribia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
√Tunahitaji RW(Proper right winger au mshambuliaji wa kutokea kulia),,Tunahitaji Kiungo mchezachaji(x2) given pogba is leaving,,Tunahitaji Kiungo mkabaji,,Tunahitaji deadly straiker..Tofauti na hapo hakuna tutakachokifanya zaidi za kuzurura nafasi ya saba na ya nane huko..

√We lack some qualities baadhi ya maeneo,ambayo hayo maeneo ni crusial sana..Tutamlaumu tu Martial ila hakuna mipira ya kueleweka inayomfikia..Perreira mechi nzima katoa key pass moja tu ya maana..Wtf

√Fred my MOTM
 
Liver wako vizuri lakini wameshasajili takumi lakini nyie bado mpo kwenye tetesi tu
 
Hivi kipindi liver ipo mbovu man u alishawahi kumpiga liver 8?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…